Jinsi simu janja zinavyoathiri afya ya akili ya watoto

Kuwapa watoto simu katika umri mdogo kunaathiri afya zao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ikiwa unafikiri kuwapa simujanja au vishkwambi watoto katika umri mdogo itaongeza ujuzi wake au kuongeza uelewa wake wa ulimwengu wa kidigitali, basi unafikiri vibaya, Shirika lisilo la kiserikali la Marekani 'Sapien Labs' limeeleza.

Tangu 2016, shirika hili linafanya kazi juu ya dhamira ya kuelewa akili ya watu.

Katika kipindi cha Corona, wakati elimu ya watoto ilipoanza mtandaoni, mjadala ulizidi kuwa ni muda gani watoto wanapaswa kuwa kwenye simu?

Mjadala ulianzia kwenye faida na hasara.

Wakati huo huo, kulikuwa na video nyingi kwenye mitandao ya kijamii pia.

Je, kimesemwa nini katika ripoti hiyo?

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Sapien Labs, watoto wanapopewa simu janja katika umri mdogo, akili zao huanza kuonesha athari tofauti wanapobalehe.

Ripoti hii imeandaliwa baada ya kuzungumza na vijana 2,76,969 kutoka nchi 40 na utafiti huu ulifanyika katika mwezi wa Januari hadi Aprili mwaka huu.

India pia imejumuishwa katika nchi hizi 40.

Imesemwa katika ripoti hii kwamba asilimia 74 ya wanawake, ambao walipewa simu za kisasa wakiwa na umri wa miaka 6, walikuwa na matatizo ya afya ya akili katika ujana wao.

Kiwango cha wanawake hawa kilikuwa cha chini katika MCQ (Tathmini ya Afya ya Akili).

Kati ya wasichana waliopewa simu hizi wakiwa na umri wa miaka 10, asilimia 61 walipata alama za chini au duni kwenye MCQs.

Hali kama hiyo ilikuwa ya asilimia 61 ya wasichana wenye umri wa miaka 15.

Athari kwa watoto

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Chhavi (jina limebadilishwa) ana hadithi sawa na yeye ni mama wa mabinti wawili.

Kwa kawaida alikuwa na shughuli nyingi za nyumbani na ili binti yake asimsumbue sana, alimkabidhi binti yake mwenye umri wa miezi 22 simu ya kisasa.

Chhavi alimpa binti yake simu baada ya kuweka vibonzo kwenye YouTube na alianza kufanya kazi za nyumbani.

Mzunguko huu uliendelea hadi binti mkubwa aliporudi kutoka shuleni.

Ingawa Chhavi hakuwahi kufikiria kuwa simu iliyokabidhiwa mikononi mwa binti yake ingekuwa shida kwake.

Mwanasaikolojia Dk Pooja Shivam anasema kwamba Chhavi alipomleta binti yake, aliweza kuzungumza kulingana na umri wake kulikuwa na wasiwasi mwingi ndani yake.

Anasema, "Kwa saa saba hadi nane, alikuwa akikaa tu kwenye simu. Chhavi alimfikira kwenye YouTube. Lakini fikiria ni nini angekuwa anatazama kwenye YouTube kutoka hapo, tunaweza kukisia tu.

''Alikuwa akiogopa, alikuwa na wasiwasi. Wakati mgeni alikuja nyumbani, alizoea kuanza kupiga kelele, alikuwa akiogopa. Hii ni pamoja na kutozungumza na kuwa mkaidi. Baada ya hapo tulimtoa mtoto kwenye simu kisha ushauri ukaanza."

Wataalamu wanaamini kwamba siku hizi wazazi wanawapa simu mikononi watoto mithili ya pacifiers (chuchu ya plastiki) katika umri mdogo.

Madaktari wanasema kwamba wazazi wanapaswa kurekebisha saa za kuwapa watoto simu.

Chanzo cha picha, DISHANT_S

Athari kwa akili ya watoto

Kwa mujibu wa wanasaikolojia, vitu elfu kadhaa vinafikia ubongo wetu kupitia ishara.

Mtu anapotumia simu janja, anapata video na sauti, huku baadhi ya mambo kama hayo yanaingia akilini, jambo ambalo huleta msisimko na udadisi ndani yake. Na inafanya kazi kama sumaku.

Kwa hivyo katika hali kama hii, unafikiri kwamba nini kitatokea wakati mtoto anapata uzoefu wa namna hii?

Dk. Pankaj Kumar Verma pia anaendesha Kliniki ya masuala ya akili ya Rejuvenate.

Akijibu swali hili, anasema hata wakati wa Corona, tuliona kwa watoto kuwa na hasira kutokana na kuongezeka kwa muda wa kuwa kwenye skrini na kufungiwa tu majumbani, na pia kuwa wenye wasiwasi na mfadhaiko.

Anaeleza zaidi, “Ubongo tayari unakua kwa watoto wadogo. Hajui anachokiona ni kizuri au kibaya kwake. Pili, ikiwa anajisikia vizuri baada ya kutazama vibonzo, ubongo hutoa kemikali dopamine ambayo humfanya ajisikie furaha.

Mtindo wa kidijitali umefanya watoto wawe na uraibu kwa namna fulani.Athari yake pia itakuwa kwamba wakati anapaswa kusoma, kucheza, kuchanganyika na marafiki, basi anawasahau na kubaki amezama tu kwenye smartphone, ambayo inampa dopamine. Kwa njia hii anaishi katika ulimwengu wa bandia.

Katika hali kama hiyo, wanaingizwa katika hali ya akili kama hofu, kuchanganyikiwa, wasiwasi na inawaathiri kwa muda mrefu. Kwa upande mwingine, watoto ambao maendeleo yao hufanyika wakati wanaishi katika kitambaa cha kijamii, hawafanyi hivyo na hii ina athari mbaya kwao katika siku zijazo.

Nini kifanyike?

Mwaka jana, serikali kuu ilikuwa imetoa miongozo mipya na mikali kuhusu kampuni za mitandao ya kijamii.

Wakati huo huo, idadi ya watumiaji wa mtandao nchini India inaweza kuongezeka hadi milioni 900 mnamo 2025.

Wataalamu wanaamini kwamba teknolojia ina pande mbili. Ingawa inaweza kuwa chanzo kikubwa cha habari, pia ina madhara yake. Katika hali hiyo, ni muhimu sana kuitumia kwa usawa, ambayo mara nyingi watu husahau.

Wataalam hutoa ushauri huu kwa wazazi:

Waweke watoto wadogo mbali na simu janja.

Amua wakati wa kumpa mtoto simu au vishkwambi.

Ikiwa mtoto anabishana kuhusu rafiki mwingine kuwa na simu, basi zungumza naye na uelezee.

Ikiwa watoto wanapaswa kushikamana na marafiki zao, basi weka simu ya mezani nyumbani au umpe simu kama hiyo ya mkononi ili tu kuzungumza na kutuma ujumbe.

Ikiwa simu ni muhimu kwa masomo ya mtoto, basi udhibiti muda wa kuwa kwenye skrini ufanyike.

Kazi hutolewa mtandaoni shuleni, kwa hivyo nunua kichapishi cha wino (printer) kwa sababu itakuwa nafuu kwako kuliko hasara kwa mtoto.

Imesemwa katika ripoti hii kwamba kadiri watoto wanavyopata simu janja, ndivyo afya yao ya akili inavyoathiriwa.