Kwa nini Marekani inakataa kuiunga mkono Israel katika kulipiza kisasi dhidi ya Iran?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ikulu ya White House imeionya Israel kuwa Marekani haitashiriki katika mashambulizi yoyote ya kulipiza kisasi dhidi ya Iran, kwa mujibu wa maafisa wakuu.
Zaidi ya ndege 300 zisizo na rubani na roketi zilirushwa dhidi ya Israel jana usiku, jambo ambalo Iran ilisema ni kujibu shambulio la Aprili 1 dhidi ya ubalozi mdogo nchini Syria.
Takribani silaha zote zilidunguliwa na wanajeshi wa Israel, Marekani na washirika wao kabla ya kufikia malengo yao.
Maafisa walisema Joe Biden aliitaka Israeli kuzingatia majibu yake "kwa uangalifu".
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumapili, afisa mkuu wa utawala alisema Biden alimwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu "kufikiri kwa makini na kwa mikakati" kuhusu jinsi majeshi yake yatajibu hatua hiyo ambayo haijawahi kushuhudiwa, na ambalo ni shambulio la kwanza la moja kwa moja lililofanywa na Iran nchini humo.
Afisa huyo aliongeza kuwa utawala wa Biden unaamini kuwa Israel "ilipatia" katika makabiliano hayo, ambayo yalianza wakati makamanda wakuu wa jeshi la Iran walipouawa katika jengo la ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria.
Takriban asilimia 99 ya makombora, ndege zisizo na rubani na makombora ya baharini yaliyorushwa wakati wa operesheni ya kulipiza kisasi ya Iran yalinaswa.
Ndege za Marekani na vyombo vya majini vilirusha makumi ya makombora kutoka Iran wakati shambulio hilo lilipotokea. Zaidi ya ndege 80 zisizo na rubani na takribani makombora sita yalitunguliwa na ndege na meli za Marekani au Jeshi la Anga la Iraq.
Mazungumzo kati ya Biden na Netanyahu yalifanyika wakati wa "janga" muda mfupi baada ya shambulio hilo, ambalo lilijumuisha takribani makombora 100 ya balestiki kuruka kwa wakati mmoja kuelekea Israeli.

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati wa simu hiyo, viongozi hao wawili walijadili "jinsi ya kufikiria juu ya mambo", na Bw Biden akisisitiza kwamba Israeli "imefanya vyema."
Katika mfululizo wa video zilizotangazwa kwenye mitandao ya Marekani mapema leo asubuhi, msemaji wa usalama wa taifa John Kirby alikariri kuwa Marekani imeweka wazi kwa Israel kwamba inataka kuepusha mzozo mkubwa.
Maafisa wakuu walisema ujumbe sawa na huo ulitumwa kwa Iran kupitia njia za kidiplomasia.
Bw Kirby na afisa huyo wote walisema Marekani itaendelea kuilinda Israel, lakini wakafutilia mbali jibu lolote la shambulizi kutoka kwa Israel.
Msimamo huu umekosolewa na baadhi ya wabunge wa Marekani na maafisa wa zamani wa vyama vyote viwili vya siasa.
Mwakilishi wa Ohio Republican Mike Turner, ambaye anahudumu kama mwenyekiti wa Kamati ya Ujasusi , alisema maoni ya Bw Kirby kuhusu utatuzi wa mzozo huo "yalikuwa mabaya".
"Tayari inafanya hali kuwa mbaya zaidi, na utawala unahitaji kujibu," aliiambia NBC.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia, John Bolton, ambaye alikuwa mshauri wa usalama wa taifa wakati wa Rais Donald Trump, alisema kuwa Marekani inapaswa kuungana na Israel ikiwa itachagua kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran.
Baada ya shambulio la Iran dhidi ya Israel, Spika wa Bunge Mike Johnson alisema shirika hilo "litajaribu tena" kutuma msaada wa kijeshi kwa Israel.
Majaribio ya hapo awali ya kutuma msaada zaidi kwa Israel yamekwama huku kukiwa na wito wa Kidemokrasia wa kutaka msaada huo ujumuishe pia misaada kwa Taiwan na Ukraine.















