Mwaka Mpya katika Urusi ya Putin - hakuna kitu cha kawaida

Rais Vladimir Putin akitoa hotuba yake ya mwaka mpya akiwa amezungukwa na watu waliovalia sare

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Vladimir Putin akitoa hotuba yake ya mwaka mpya akiwa amezungukwa na watu waliovalia sare

Saa katika Mnara wa Spassky wa Kremlin inagonga usiku wa manane. Wimbo wa taifa wa Urusi unacheza.

Kisha runinga ya Channel One itaanza 2023 kwa wimbo wa pop: "Mimi ni Mrusi na nitaenda mbali kabisa...mimi ni Mrusi, licha ya ulimwengu."

Ifuatayo Juu ya Pops (ya kizalendo): "Nilizaliwa katika Umoja wa Kisovyeti, nilifanywa katika USSR!" Ninabadilisha chaneli.

Katika karamu ya Mwaka Mpya wa Russia-1, mmoja wa waandishi maarufu wa habari za vita wa kituo hicho ameshikilia glasi ya shampeni, kuangazia 2023 na kuomba "habari njema zaidi kuliko mbaya kutoka vitani".

Walioketi pamoja naye ni wanaume waliovalia mavazi ya kijeshi.

Afisa aliyeteuliwa na Moscow kutoka Ukraine inayokaliwa na Urusi anatangaza: "Nawatakia amani nyote. Lakini amani itakuja tu baada ya ushindi wetu."

Uafuatilia shamra shamra zza sherehe za mwaka huu kwenye Televisheni ya Kirusi ni hisia mseto tufanye sherehe na tushinde katika uwanja wa vita.

Hii si hali ya kawaida ya TV kwa mkesha wa Mwaka Mpya nchini Urusi.

Kisha tena, huu sio usiku wa Mwaka Mpya wa kawaida.

Hali ya "Kawaida" ilitoweka miezi 10 iliyopita wakati Urusi ilipozindua oparesheni ya uvamizi kamili wa Ukraine.

Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hakukuwa na kitu cha "kawaida" kuhusu hotuba ya Mwaka Mpya ya Vladimir Putin kwa watu wa Urusi.

Kwa hotuba yake ya kila mwaka rais kawaida husimama peke yake nje ya Kremlin.

Mwaka huu, waliosimama nyuma yake, walikuwa wanaume na wanawake waliovalia sare za kivita.

Katika hotuba yake mwaka jana, kiongozi wa Kremlin alisema kwamba "Mkesha wa Mwaka Mpya umejaa furaha na hisia za furaha".

Mawazo mazuri ya furaha yalikuwa haba wakati huu.

Rais Putin alitumia hotuba hiyo kukuza ukweli mbadala wa Kremlin: kwamba katika mzozo huu Urusi ni shujaa na Ukraine na ulimwengu wa Magharibi ni wabaya.

"Kwa miaka mingi, wasomi wa Magharibi walituhakikishia kwa unafiki nia yao ya amani ... lakini kwa kweli, waliwahimiza Wanazi mamboleo kwa kila njia," Rais Putin alisema.

"Kutetea Nchi yetu ni jukumu takatifu tunalodaiwa na mababu zetu na vizazi."

Wakati Kremlin inazungumzia kuhusu "kutetea Nchi yetu ya asili", kumbuka kuwa ni Urusi iliyovamia Ukraine. Si kinyume chake.

N

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Urusi anadai kuwa nchi yake inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na matukio makubwa ya 2022: "Ulikuwa mwaka wa... hatua muhimu kuelekea uhuru kamili wa Urusi.

" "Tunaweka msingi wa mustakabali wetu wa pamoja, uhuru wetu wa kweli."

Madai kwamba, katika vita hivi, Urusi inapigania mamlaka na uhuru wake ni ya kutatanisha, kusema kweli.

Kwanza kabisa, Urusi kwa muda mrefu imekuwa taifa huru, huru. Hata kama unakubali dhana ya Vladimir Putin kwamba Urusi haijawahi kupata "uhuru kamili" swali linatokea: kwa nini isiwe hivyo?

Bw Putin amekuwa madarakani kwa miaka 23. Muda wa kutosha, ambao ungemwezesha kufikia hilo azma hiyo.

Kitu kingine ambacho Rais Putin anafanya katika hotuba yake ya mwaka mpya ni kuwagawanya Warusi, kuna wale wanaounga mkono "operesheni yake maalum ya kijeshi" na wale wasiounga mkono oparesheni hiyo.

"Ulikuwa mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi," kiongozi wa Kremlin alisema, "na akaweka mstari wazi kati ya ujasiri na ushujaa, kwa upande mmoja, na usaliti na woga kwa upande mwingine ..."

Mnamo 2023 tunaweza kuona Kremlin ikichora mstari huu kwa uwazi zaidi.

Mamlaka ya Urusi imeelekeza rasilimali zote za nchi kwa "operesheni maalum ya kijeshi".

Hakuna nafasi ya mjadala au majadiliano: serikali inatarajia umma kukusanyika na kumuunga mkono rais.

Wale Warusi ambao hawatafanya hivyo watafanywa wajihisi kuwa wanasaliti Nchi yao ya asilia.