Putin anafikiria nini na anapanga nini?

G

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Rais Putin ameazimia kuendelea na vita licha kushindwa kijeshi katika Ukraine

Ni swali ambalo tumekuwa tukiuliza kwa miezi kadhaa sasa, hata kabla ya uvamizi wa Urusi katika Ukraine.

Putin anafikiria nini na anapanga nini?

Wacha nikanushwe wazi. Sina uwezo wa kuifahamu hali ya baadaye ya Ukraine. Wala sina mawasiliano ya moja kwa moja na Putin

Rais wa zamani wa Marekani George W Bush wakati mmoja aliwahi kusema kuwa anaweza kumtizama Putin machoni '' na kuelewa hisia za roho yake'' . Tazama jinsi uhusiano baina ya Urusi na Magharibi ulipoishia.

Kwahiyo, kuingia akilini mwa kiongozi wa Kremlin ni kazi ngumu. Lakini ni muhimu kujaribu. Labda kuliko ilivyowahi kutokea wakati wowote ule, kufuatia maonyesho ya hivi karibuni ya nyuklia yaliyofanywa na Moscow.

Hapana shaka kwamba rais wa Urusi anakabiliwa na shinikizo. Mpango p wake wa kile kinachoitwa ''opresheni maalum ya kijeshi" ikatika Ukraine umemuendea vibaya. Ulitakiwa kudumu kwa siku chache. Lakini tuko karibu miezi minane na mwisho wake hauonekani.

Kremlin inakiri "kunakoonekana " kwa vikosi vya Urusi katika wiki za hivi karibuni ambapo urusi imekuwa ikipoteza maeneo katika Ukraine ambayo ilikuwa imeyachukua awali kufuatia uvamizi.

Idadi ya wanajeshi wa ardhini, mwezi uliopita alitangaza kuwaandaa kwa ajili ya vita, kitu amacho alisistiza kuwa atakifanya. Wakati huo huo, vikwazo vinaendelea kuathiri uchumi wa Urusi.

Kwahiyo, tukirejea katika hali ya fikra za Putin. Tutakuwa tunafikiria alikosea, kwamba uamuzi wake ulikuwa ni kosa la kimsingi ?

Usifikirie hivyo.

G

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Vikosi vya Urusi vililazimishwa kuchukua uamizi wa aibu wa kurudi nyuma kutoka karibu maeneo yote ya jimbo la Kaskazini-mashariki la Ukraine la Kharkiv mwezi Septemba.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuongezeka kwa mashambulio ya wiki hi ya makombora ya Urusi wiki hii kunaonyesha Kremlin imebaini kuwa isingependa kufanya mambo yawe mabaya zaidi baina yake na Kyiv.

Pamoja na Magharibi, pia?

"Anajaribu kuepuka makabiliano ya moja kwa moja na Magharibi, lakini wakati huo huo anajiandaaa kwa ajili ya hilo ," anaamini mwanasiasa huru mkongwe Grigory Yavlinsky. Ninahofia zaidi uwezekano wa mzozo wa nyuklia. Na, la pili , ninahofia vita visivyomalizika"

Lakini "vita visivyomalizika" vinahitaji raslimali zisizomalizika. Hicho ni kitu ambacho Urusi inaonekana haina. Wimbi la mashambulizi ya makombora katika miji ya Ukraine ni kuonyesha usanii wa vikosi, lakini Moscow inaweza kuendeleza mashambulio ya aina hii kwa muda gani?

"Unaweza kuendelea kumimina makombora haya kwa siku, wiki kadhaa , miezi? Wataalamu wenye wanashaka na hilo kwamba tuna makombora ya kutosha" anasema Bw Remchukov.

"Pia kwa mtizamo wa kijesh, hakuna yeyote aliyewahi kusema kile ambacho kitakuwa ishara ya ushindi kamili wa [Urusi]? Ni ipi ishara ya ushindi?Katika mwaka 1945 lilikuw ani bango juu ya Berlin. Ni kipi kigezo cha mafanikio sasa? [Bango] juu ya Kyiv? juu ya Kherson? Juu ya Kharkiv? Sijui. Hakuna mtu anyejua. "Hata haiko wazi kwamba hata Vladimir Putin anajua''.

Mwezi Februari, lengo la Kremlin lilionekana kuwa ni ushindi wa haraka, kuwarejesha majirani Ukraine katika uzio wa Moscow bila vita vya muda mrefu. Alikosea mahesabu.

Alipuuza sio azma ya jeshi la Ukraine na watu wake ya kuiltetea ardhi yao, lakini pia uwezo wa jeshi lake mwenyewe.

Anafikiria nini sasa? je mpango wa sasa wa Putin kuimarisha udhibiti wa eneo la Ukraine ambalo anadai amelitwaa na halafu amalize mzozo? au ameazimia kusonga mbele hadi Ukraien yote irejee chini ya ushawishi wa Kremlin?

Wiki hiii rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev aliandika: " taifa la Ukraine katika muundo wake wa sasa...litakuwa tisho la wazi na la moja kwa moja kwa Urusi. Ninaamini lengo la hatua za hali yetu ya baadaye linapaswa kuwa ni kukamilisha uvunjwaji wa utawal wa kisiasa wa Ukraine."

Kama maneno ya Medvedev yanaelezea fikra za rais Putin, tarajia vita vya muda mrefu na vya umwagaji damu.

G

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jeshi la Urusi linasema linataka kuwaingiza jeshini wanajeshi 300,000 wa akiba-lakini inaonekana kuna ongezeko kubwa la upinzani wa kuvuka mpaka kuingia Ukraine

Lakini ,ni dhahiri kwamba vitendo vya Putin nje ya nchi vina athari nyumbani. Kwa miaka mingi Kremlin ilijenga picha ya Putin kama ''Bw Utulivui'', ikiutia moyo umma wa Warusi kuamini kuwa ili mradi yuko madarakani watakuwa salama. Hilo ni gumu kuaminika.

"Mkataba wa awali kati ya Putin na jamii ulikuwa kwamba 'Nitawalinda," anasema Bw Remchukov.

"Kwa miaka mingi alionekana kama mtu 'wa kuaminika'. Kuna aina gani ya kuaminika iliyopo pale leo? Thana imeisha. Hakuna cha kuaminika. Waandishi wangu hawajui iwapo wataitwa kujiunga na jeshi watakapofika nyumbani leo ."