Muhammadu Buhari: Maisha ya rais wa zamani wa Nigeria katika picha

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
- Author, Wedaeli Chibelushi
- Nafasi, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Maisha ya Muhammadu Buhari yaliangazia mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini Nigeria katika miongo mitano iliyopita - na mara nyingi alijipata katikati ya matukio.
Rais huyo wa zamani wa Nigeria, ambaye alifariki Jumapili akiwa na umri wa miaka 82, alikua kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo baada ya mapinduzi, aliwahi kufungwa jela na utawala mpya wa kijeshi, kabla ajipange upya miongo kadhaa baadaye kushinda urais katika uchaguzi wa kidemokrasia.
Mara nyingi alipigwa picha akiwa amevaliamiwani nyeusi au miwani kubwa, yenye fremu nyeusi, kofia ya kitamaduni ya zanna na tabasamu kubwa, ambayo ilikuwa sehemu kubwa ya maisha ya Buhari yaliyoangaziwa hadharani.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Buhari - katika picha hii ya 1977 alikuwa na Mfalme wa Uswidi Sweden Carl XVI Gustaf na Sheikh Ahmed Zaki Yamani wa Saudi Arabia mwaka 1977 - alianza taaluma yake ya kijeshi punde alipotoka shule.
Wakati pich ahii ilipopigwa, Buhari alikuwa mepiga hatua nakupandishwa che hadi kuwa kamanda wa kijeshi wa kikanda.
Miaka kadhaa baadaye, mwaka1983, wanajeshi walimpindua rais Shehu Shagari aliyekuwa madarakani wakati huo .

Chanzo cha picha, Sygma via Getty Images
Ingawa Buhari alishikilia nafasi ya kiongozi wa kijeshi, alipinga madai kwamba alipanga mapinduzi hayo, akisema kuwa aliwekwa madarakani na makamanda wa ngazi ya juu ambao walitaka mti atakayeshikilia nafasi hiyo kwa niaba yao. Hata hivyo madai ya Buhari kuwa na jukumu katika mapinduzi hayo ya kijeshi yaliibuka.
Baada ya kuongoza kwa mkono wa chuma kwa takriban miaka miwili, kukabiliana vikali dhidi ya ufisadi na ukiukwaji mbalimbali wa haki za binadamu, Buhari mwenyewe aliondolewa madarakani. Utawala mpya wa kijeshi ilimweka chini ya kizuizi cha nyumbani kwa miaka mitatu.
Mwaka 2003, baada ya kujitenga na siasa kwa miongo kadhaa, Buhari aliamua kutafuta nafasi nyingine ya kuongoza nchi.
Wakati huo, aliomba nafasi ya juu kupitia uchaguzi wa kidemokrasia - akigombea kupitia chama cha All Nigerian Peoples Party (ANPP).

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Katika picha hii anaonekana (upande wa kulia) akiwa na mgombea mwenza wake Chuba Okadigbo (kushoto) pamoja na mwenyekiti wa ANPP Don Etiebet.
Buhari alishindwa uchaguzi huo na Olusegun Obasanjo mwaka 2003, na alijaribu tena kuwania urais mwaka 2007 na 2011 lakini hakufanikiwa.
Licha ya kushindwa huko aliendelea kujiimarisha kisiasa na kupata uungwaji mkono wa vijana kwa ahadi ya kukabiliana na ufisadi na ukosefu wa usalama.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Buhari alipata maarufu mkubwa katika eneo la kaskazini mwa Nigeria alikozaliwa

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Katika bango lililo na picha yake katika mji wa Kaduna wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015, linasomeka: wanyeji watampigia kura "Baba" tu ikimuashiria Buhari.
Buhari hatimaye alishinda uchaguzi wa 2015, na kumuondoa rais aliyekuwa madarakani wakati huo Goodluck Jonathan.
Aliandikisha historia ya kuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu.

Chanzo cha picha, Red Media Africa
Baada ya hatimaye kuchukua hatmu ya uongozi, muhula wa kwanza wa Buhari ulikumbwa na msukosuko. Uchumi wa nchi ulidorora kwa mara ya kwanza katika muongo mmoja na mizozo ya usalama ikaongezeka.
Wakati mke wa Buhari - katika picha hapo chini - alipokosoa utawala wake hadharani, rais alionyesha kughadhabishwa kwake na kauli hiyo na kumjibu mke wake kuwa jukumu lake ni la jikoni.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Licha ya kukabiliwa na changamoto katik amhula wake wa kwanza, Buhari alichaguliwa tena mwaka 2019.
Kama rais wa mojawapo ya mataifa ya Afrika yenye uchumi mkubwa , alisafiri duniani kote, akihudhuria mikutano ya hadhi ya hali ya juu na kukutana na wakuu wenzake wa nchi.

Chanzo cha picha, John Stillwell/Getty Images
Buhari alilakiwa na Malkia Elizabeth katika mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola mnamo 2015.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Mapema mwaka wa 2015, alikaribishwa Ikulu ya White House na Rais wa wakati huo wa Marekani Barack Obama.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na mnamo 2018, Buhari alikuwa kiongozi wa kwanza kutoka eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara kukutana na Rais Donald Trump huko Washington.

Chanzo cha picha, Hindustan Times via Getty Images
Kufuatia kifo chake, katika kliniki moja mjini London, Buhari anakumbukwa na baadhi ya watu kama mtu aliyevunja ahadi zake za kampeni na kuponda upinzani.
Kwa wengine, alikuwa bingwa wa utaratibu ambaye alijaribu kila awezalo kufiki amalengo yake katikati ya mfumo usiofanya kazi wa kisiasa.
Katika kumuenzi mpinzani wake wa zamani, Jonathan alimuelezea Buhari kama mtu ambaye "alijitolea katika kujitolea kwake kwa wajibu wake na alitumikia nchi kwa tabia na hisia kubwa ya uzalendo".

Chanzo cha picha, Reuters












