Tetesi za soka Ulaya: Chelsea yagoma kumuuza Cole Palmer

Muda wa kusoma: Dakika 1

Chelsea wanamwona kiungo mshambuliaji Cole Palmer, 23, kama mchezaji "asiyeguswa" licha ya kuhusishwa na Manchester United, na wanamchukulia mchezaji huyo wa England aliye na mkataba hadi 2033 kuwa mhimili mkubwa wa mustakabali wa klabu hiyo. (Sky Sports)

Brighton wamekataa ofa kutoka Nottingham Forest kwa ajili ya beki wake wa England mwenye umri wa miaka 34, Lewis Dunk. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Chelsea Raheem Sterling anatarajiwa kuondoka kabla ya dirisha la usajili wa majira ya baridi kufungwa, huku pande zote zikifanya mazungumzo ya kufanikisha kuondoka kwa mchezaji huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 31. (Fabrizio Romano)

West Ham wanaangalia uwezekano wa kuwasajili kwa mkopo kipa wa Tottenham kutoka Czech, Antonin Kinsky, 22, na beki wa Chelsea kutoka Ufaransa, Axel Disasi, 27. Hata hivyo, ili ifanikiwe, Hammers watalazimika kumrejesha beki wa Brazil Igor Julio, 27, Brighton. (Guardian)

Wawakilishi wa kipa wa Manchester United mwenye umri wa miaka 29, Andre Onana, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Trabzonspor, wamefanya mazungumzo kuhusu kurejea kwa mlinda mlango huyo wa Cameroon katika klabu yake ya zamani Inter Milan majira ya kiangazi. (Mail)

Wolves wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo kiungo wa England mwenye umri wa miaka 25, Angel Gomes, kutoka klabu ya Ufaransa Marseille. (Talksport)

Mshambuliaji wa Auxerre Lassine Sinayoko anasakwa na pia na Wolves, huku klabu za Championship, Coventry City na Middlesbrough nazo zikionesha nia ya kumsajili mchezaji huyo wa Mali mwenye umri wa miaka 26. (Football Insider)

Burnley wako kwenye mazungumzo na West Ham kuhusu kumsajili kwa mkopo kiungo wa England mwenye umri wa miaka 31, James Ward-Prowse. (Telegraph)

Sunderland wamepuuza taarifa zinazodai kuwa mshambuliaji wa Hispania mwenye umri wa miaka 20, Eliezer Mayenda, anaweza kuruhusiwa kuhamia Paris FC. (The I paper)