Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Timu 6 za England na usiku wa rekodi Ligi ya Mabingwa leo
- Author, Sam Drury
- Nafasi, BBC Sport journalist
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Michezo ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya katika hatua ya makundi inahiitimishwa usiku wa leo ukitarajiwa msisimko mkubwa, huku timu 30 zikitarajia kujua hatima zao.
Timu sita kutoka Englad zinaweza kumaliza katika nafasi 8 za juu.
Arsenal tayari wamejihakikisha kuingia hatua ya 16 bora, ambapo watajiungana na Bayern Munich, lakini timu nyingine nyingi bado zina kazi ya kufanya kwenye msimamo wa kundi lenye timu 36 na lenye ushindani mkali.
Arsenal wanapewa nafasi kubwa kushinda mashindano haya kwa mara ya kwanza, huku Opta ikiwapa asilimia 31%, mbele ya Bayern (16.9%).
Timu nyingine za ligi kuu England zilizo kwenye nafasi ya nane bora ni Liverpool, Tottenham, Newcastle United, na Chelsea. Kubaki kwenye nafasi hizi kutawawezesha kuepuka michezo ya mtoano na kuingia moja kwa moja hatua ya 16 bora.
Manchester City, kwa sasa wako kwenye nafasi ya kucheza mtoano, wako nyuma ya Newcastle (7) na Chelsea (8) kwa tofauti ya mabao tu. Timu hizi tatu za England ni miongoni mwa timu nane zenye alama 13 kabla ya mechi za mwisho, huku michezo yote 18 ikianza muda mmoja saa 23:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa timu sita kutoka nchi moja kuingia hatua za mtoano.
Ubashiri wa Opta:
Arsenal: 31%
Bayern Munich: 16.9%
Manchester City: 8.8%
Barcelona: 8.1%
Liverpool: 8%
Arsenal inapigiwa chapuo kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya mwaka huu ikipewa asilimia 31%
Timu gani zimefuzu 16 bora?
Arsenal, vinara wa kundi akishinda mechi zote saba, wanahitaji alama moja tu nyumbani dhidi ya Kairat Almaty ili kujihakikisha kumaliza wa kwanza kwenye hatua ya sasa.
Kuhusu mpangilio wa hatua ya 16 bora, timu mbili za juu zitakutana na washindi wa mtoano kutoka timu zinazomaliza kati ya nafasi ya 15 hadi 18.
Bayern Munich watajihakikisha nafasi mbili za juu kama wataepuka kupoteza dhidi ya PSV Eindhoven.
Timu zinazomaliza katika nafasi mbili za juu pia zitaruhusiwa kucheza mechi ya pili nyumbani katika hatua zote kwenye kila raundi hadi fainali, ambayo itachezwa Budapest.
Timu zinazoishia kati ya nafasi ya 9 hadi 24 zitashiriki mtoano, hatua itakayochezwa mnamo 17/18 na 24/25 Februari, na kuamua timu nane zitakazojiunga na zile zilizofuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora.
Je, Mourinho na Conte kuviadhibu vilabu vyao za zamani?
Mechi za kuwania kupata nafasi 8 za juu zinaleta msisimko zaidi katyika hatua ya makundi kutokana na zinazowania nafasi hizo kuwa karibu karibu sana kwa alama.
Real Madrid (alama 15) na Liverpool (15), pamoja na Tottenham (14), zikishinda mechi zao za mwisho zitaingia moja kwa moja hatua ya 16 bora.
Spurs watacheza dhidi ya Eintracht Frankfurt, kibonde ambaye hajashinda mechi hata moja, watakutana huko Ujerumani.
Liverpool watakuwa nyumbani dhidi ya Qarabag, ambayo bado ina nafasi ndogo ya kuingia nane bora.
Real Madrid watacheza ugenini dhidi ya Benfica, klabu inayofundishwa na Jose Mourinho, kocha wa zamani wa Real. Benfica, iliyoshinda mechi 2 tu katika michezo saba, itahitaji kuifunga Real ili kupata nafasi ya kucheza hatua ya mtoano.
Chelsea watakutana na Napoli, wakiwa na Antonio Conte, kocha wao wa zamani, ambaye alishinda Serie A msimu uliopita. Napoli ipo nje ya nafasi za kucheza mtoani kwa tofauti ya mabao na wanahitaji kushinda.
Manchester City watakuwa nyumbani dhidi ya Galatasaray, huku Newcastle wakienda Paris kucheza dhidi ya PSG.
Tizo zote kuanzia nafasi ya 3 hadi ya 18 bado zina nafasi kuingia nane bora.
Licha ya timu 16 bado kuwania nafasi sita za juu zilizosalia, ni mechi mbili tu kati ya 18 ambazo zinazikutanisha timu zinazowania nafasi sita za juu zilizosalia ukiacha ya kwanza na ya pili. Newcastle dhidi ya PSG na Borussia Dortmund wakiwa nyumbani kukabiliana na Inter Milan.
Vita ya kucheza mtoano ama mchujo
Kuna vita ngumu sana kupata timu za kuingia mchujo. Ni timu nne pekee za Frankfurt, Slavia Prague, Villarreal na Kairat ambazo zimeondolewa. Lakini zilizosalia zote zinaweza kupata nafasi hiyo ya mchujo, timu zinazoshika nafasi ya 8 mpaka 24.
Alama tatu zinaitenganisha Marseille iliyo katika nafasi ya 19 na Ajax iliyo nafasi ya 32, huku hata Dortmund iliyo katika nafasi ya 16, alama mbili mbele ya timu hiyo ya Ufaransa na bado wakiwa na matumaini hafifu ya kumaliza katika nafasi ya nane bora, bado hawana uhakika wa kufuzu kwa hatua ya mtoano.
Ratiba za mechi za mwisho
- Ajax v Olympiacos
- Arsenal v Kairat Almaty
- Athletic Club v Sporting
- Atletico Madrid v Bodo/Glimt
- Barcelona v Copenhagen
- Bayer Leverkusen v Villarreal
- Benfica v Real Madrid
- Borussia Dortmund v Inter Milan
- Club Brugge v Marseille
- Eintracht Frankfurt v Tottenham
- Liverpool v Qarabag
- Manchester City v Galatasaray
- Monaco v Juventus
- Napoli v Chelsea
- PSV Eindhoven v Bayern Munich
- Pafos v Slavia Prague
- Paris St-Germain v Newcastle
- Union Saint-Gilloise v Atalanta
Mechi zote zitapigwa saa 23:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki