Jinsi gani binadamu walizungumza enzi za kale?

Chanzo cha picha, Getty Images
Jinsi gani binadamu walizungumza enzi za kale? Tsubamé, mwenye miaka 8, London, Uingereza.
'Curious Kids' ni mfululizo wa makala ambapo wataalam hujibu maswali ambayo watoto huuliza kuhusu ulimwengu.
Enzi za kale wakati mwingine inachukuliwa kama miaka ya zamani sana. Ilianza yapata miaka milioni 3 iliyopita na ilidumu hadi miaka 40,000 iliyopita.
Ni kipindi hiki wakati mwingine hufahamika kama enzi ya mawe kwa sababu kipindi hicho mababu zetu walitengeneza vifaa vyao kutokana na mawe.
Binadamu kama sisi, aina ya Homo sapiens, walionekana muda mrefu baada ya kuanza kwa enzi hii, karibu miaka 200,000 iliyopita.
Enzi hii ya mawe ilianza pale aina mbalimbali za manyani zilipoanza kutengeneza vitu rahisi kwa kukata vipande vya mawe kutoka kwenye vipande vikubwa vya mwamba.
Manyani hawa walisimama wima kidogo walipotembea, na hiyo ilimaanisha kuwa mikono yao ilikuwa huru kufanya mambo mengine, kama vile kutengeneza vitu.
Hawa manyani wa awali walikuwa na akili ndogo, si tofauti na ubongo wa sokwe, na hawakuwa wanazungumza.
Manyani wengine waliotembea wima walijitokeza baadaye enzi hiyo. Walikuwa wakipewa majina kama vile ‘Homo habilis’ au ‘Homo erectus’.
Spishi hizi ziliishi Afrika karibu miaka milioni 1 hadi 2 iliyopita, kwa muda mrefu kabla ya watu kama sisi kuwepo.
Walikuwa na akili nyingi kuliko manyani wa awali kabisa, lakini akili zao zilikuwa ndogo kuliko zetu.
Hawakuwa hodari kama sisi na hawakuzungumza, hata kama walikuwa na sauti.
Karibu miaka 400,000 iliyopita, aina tatu ambazo zilikuwa na akili nyingi zaidi kuliko manyani wa awali kabisa waliokuwa wanyofu yaani waliweza kusimama wima waliishi wakati mmoja.
Hawa waliitwa Neanderthals, Denisovans na aina ya mapema ya Homo sapiens - mababu zetu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Neanderthals na Denisovans waliishi nje ya Afrika katika sehemu ya dunia inayojulikana kama Eurasia, ambayo ni pamoja na Ulaya.
Kidogo inajulikana kuhusu Denisovans, lakini kuhusu 100,000 miaka iliyopita, Neanderthals walikuwa na mikuki ya mbao na baadhi ya zana rahisi zilizotengenezwa kutokana na mifupa ya wanyama kama vile kulungu mbali na zana zao za mawe.
Baadhi ya watu wanadhani kwamba kwa sababu ya ujasiri, akili zao nyingi na uwezo wao wa kutengeneza zana tofauti na zile zitokanazo na mawe, Neanderthals waliweza kuzungumza. Lakini hayo ni kudhania tu. Binadamu wa mwisho wa Wananderthal walifariki yapata miaka 40,000 iliyopita.
Watu kama sisi
Binadamu wa kwanza aliishi Afrika. Takriban miaka 200,000 iliyopita, manyani wa awali aina ya Homo sapiens walibadilika katika kile tunachokiita sasa binadamu wa kisasa.
Binadamu hawa wa siku hizi walikuwa na akili kama tulivyo sasa, na wangeweza kuongea kwa kutumia lugha kama tunavyofanya leo.
"Homo sapiens" inamaanisha "binadamu wenye hekima". Mwishoni mwa enzi ya kale maarufu kama ya mawe, karibu miaka 60,000 iliyopita, watu walisafiri nje ya Afrika na hatimaye kuenea duniani kote.
Mwishoni mwa enzi ya kale maarufu kama ya mawe, karibu miaka 60,000 iliyopita, watu walisafiri nje ya Afrika na hatimaye kuenea duniani kote.

Mwanzoni, hata mababu zetu aina ya Homo sapiens pia nao walitenegeneza zana na vitu kutokana na mawe, lakini kuwa na uwezo wa kuzungumza, pengine walitumia lugha yao kufundisha (maarifa yao) kwa kila mmoja.
Baada ya muda, wao kujifunza kutengeneza aina mbalimbali za zana kwa mawe, miti, mifupa, na ngozi.
Walikuwa na nguo, viatu, na kutengeneza makazi yao na kuwinda pamoja kwa ajili ya kutafuta chakula.
Miaka 40,000 iliyopita, na pengine hata mapema zaidi, binadamu wa kisasa walichora picha kwenye kuta za pango. Kungekuwa na lugha chache sana enzi ya kale ya mawe kuliko ilivyo leo. Lakini lugha ambazo zingekuwepo zingekuwa kama lugha zetu za kisasa.
Watu wangezungumza katika sentensi zenye nomino na vitenzi, hata kama maneno waliyoyatumia yangekuwa tofauti, kama vile, wanavyosema, maneno ya Kijapani ni tofauti na maneno ya Kiingereza au Kifaransa.
Lugha mbalimbali
Lugha zingekuwa tofauti kati ya makabila. Watu wanaweza kuwa waliona ni vigumu kuzungumza na mtu kutoka kabila jingine, kama vile tunapokwenda mapumzikoni nchi nyingine, wakati mwingine tuna wakati mgumu kuelewa lugha.
Lugha zingekuwa na maneno machache kuliko tunavyofanya leo kwa sababu hazikuhitaji maneno kwa mambo mengine kama vile televisheni, magari, au kompyuta.

Chanzo cha picha, SPL
Lakini kama sisi, binadamu wa kisasa miaka 200,000 iliyopita angehesabu mambo. Wangekuwa na maneno "mama" na "baba" au "dada" na "kaka".
Walikuwa na majina kwa wanyama na mimea, wangeweza kufanya mipango, kusema "tafadhali" na "kushukuru", na wangeweza kuwa na majina kwa kila mmoja.
Binadamu wa siku za mwanzo huenda aliongelea mambo mengi yale yale tunayoyazungumzia: Nini cha kula, rafiki zao walikuwa akina nani na kadhalika.
Wazazi wangezungumza kuhusu watoto wao na watoto wangecheza na kila mmoja, pengine kuzungumza wakati wote kama watoto wanavyofanya leo.
Pia wangeimba nyimbo miongoni mwao.
Huenda walikuwa watu wa kale wa enzi ya mawe lakini walikuwa wa kisasa linapokuja suala la kuongea.












