Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini Putin aliivamia Ukraine?
- Author, Paul Kirby
- Nafasi, BBC News
- Muda wa kusoma: Dakika 7
Wakati rais wa Urusi Vladimir Putin aliwatuma wanajeshi 200,000 nchini Ukraine, lengo lake lilikuwa kuchukua udhibiti wa mji mkuu wa Kyiv kwa kutumia siku kadhaa, kuipindua serikali ya Ukraine na kuirejesha chini ya ushawishi wa Urusi.
Miaka minne baadaye, Putin hajafanikiwa kufanya hilo, ila amedhibiti maeneo tano ya Urusi kufikia sasa.
Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akijaribu kutafuta suluhu ya kusitisha mpaigano ila bado hajafanikiwa.
Moscow bado inaitaka Ukraine kuipa sehemu ya ardhi yake, dai ambalo Kyiv haikubaliani nalo.
Mbona Putin aliivamia Ukraine?
Baada kutekeleza shambulio kubwa kuwahi kutokea Ulaya tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, Putin alitoa taarifa akitangaza azimio lake la "kulemaza uwezo wa Ukraine kijeshi na kinazi"
Urusi imekuwa ikiikashifu Ukraine kuwa taifa la kinazi.
Putin tayari amedhibiti eneo la Crimea nchini Ukraine, baada ya mapinduzi ya yaliyomuondoa rais aliegemea Urusi na nafasi hiyo kuchukuliwa na rais aliyeegemea upande wa magharibi.
Putin pia alichochea vita eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine, huku makundi yanayoiunga mkono Urusi yakidhibiti eneo hilo, na kuanzisha serikali mbadala inayoungwa mkono na Moscow.
Ila uvamizi wa mwaka wa 2022, ulikuwa mkubwa kwa na wa kiwango tofauti.
Putin alikuwa ameitambua eneo linalokaliwa na makundi ya waasi kama taifa huru. Kisha uvamizi ukaanza, na kusema kuwa wakaazi wa eneo hilo ambao wengi wao wanazungumza kirusi, wanahitaji kulindwa dhidi ya serikali ya Kyiv.
Siku moja baadaye, Putin aliiambia jeshi la Ukraine, "kuchukua sheria mikononi mwao" na kuwalenga "magenge, watumizi wa dawa za kulevya na wanazi" ambao wanaiendesha serikali ya Ukraine.
Aliongeza pendekezo lingine la kutaka Ukraine kutoegemea upande wowote. Aliishtumu jumuiya ya kujihami ya Nato, kwa kutaka kuwatuma wanajeshi wake karibu na mpaka wa Urusi na Ukraine.
Kiongozi huyo wa Urusi anapinga uwepo wa Ukraine kama taifa na kusema "Ukraine ya sasa ilitengenezwa na Urusi" baada ya mapinduzi ya kikomunisti ya mwaka wa 1917.
Mwaka wa 2021 Putin alisema " Warusi na raia wa Ukraine ni kitu kimoja" kuanzia Karne ya tisa. Katika mahojiano ya televisheni mwaka wa 2024 Putin alisema Ukraine ni taifa "bandia."
Semi zake zimefanya wengi kufikiri kuwa lengo lake la kuivamia Ukraine ni kuitokemeza na "kulifuta" taifa hilo kabisa.
Je, Putin anataka kumuondoa Zelensky?
Putin kwa muda mrefu amekuwa akitaka kumuondoa rais wa Ukraine anayeegemea upande wa magharibi, na Zelensky amekuwa akilengwa tangu kuanza kwa vita hivyo.
Wanajeshi wa Urusi walijaribu mara mbili kuingia ikulu ya Ukraine baada ya uvamizi wa Urusi, huku mshauri wa rais wa Ukraine akisema Urusi ilitaka kumuua rais huyo.
"Wanataka kuingamiza Ukraine kwa kumuua rais wa taifa."
Zelesnky awali alisema Putin alikuwa anamtaka Viktor Medvedchuk, tajiri anayeiunga mkono Urusi ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kuwa rais wa taifa hilo.
Kufikia sasa Putin hajakubali kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Zelensky, hku maafisa wake wakimwita "mtu wa kupotezewa"na "mpumbavu". Putin anasema Zelensky yuko madarakani kinyume cha sheria, semi ambayo imerejelewa na rais Trump pia.
Putin anasema kuahirishwa kwa uchaguzi wa Ukraine uliokuwa ufanyike mwezi Machi 2024, ni kinyume cha katiba, ila kulingana na Ukraine ni kutokana na vita vinavyoendelea.
Uchaguzi wa Putin uliofanyika mwaka wa 2024, umetiliwa shaka, kutokana na viongozi wa upinzani wa Urusi kuuawa wengine wakiwa wamezuiliwa gerezani.
Je, upanuzi wa NATO ndiyo wakulaumiwa?
Kwa miaka mingi Putin amekuwa akilalamikia upanuzi wa jumuiya ya kujihami wa Nato kuelekea mashariki, akisema ni tishio kwa usalama ,na iwapo Ukraine itajiunga na muungano huo, watakuwa "wamevuka mpaka."
Kabla ya uvamizi wa Urusi mwaka wa 2022, Putin alikuwa anataka Nato kuondoa na kutowatuma wanajeshi wa muungano huo katika mataifa ya kati na mashariki mwa Ulaya haswa mataifa yaliyojiunga na muungano huo baada ya mwaka wa 1997.
Ila Urusi ilianza vita baada ya kuingilia kijeshi Georgia mwaka wa 2008 na baadaye Crimea 2014.
Baada ya uvamizi wa Crimea,Nato ilianzisha vituo vyake vya kijeshi karibu na Urusi.
Nato imekuwa ikisisitiza kuwa lengo kuu la muungano huo ni kuwalinda mataifa wanachama. Uswidi na Finland wamejiunga na Nato miaka miwili iliyopita kutokana na vitisho kutoka kwa Urusi
Ukraine ilikuwa inataka kujiunga na Nato na umoja wa ulaya kabla ya uvamizi wa Urusi kutokea.
Vita hivi vitaishaje?
Njia sahihi ya vita hivi kumalizika ni kupitia mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande mbili zinazozozana.
Mwezi Agosti mwaka uliopita, Putin alialikwa katika kongamano moja katika jimbo la Alaska nchini Marekani, ila hakuna muafaka ulioafikiwa.
Mapema 2026, wajumbe wa Ukraine na Urusi wamekuwa wakifanya mazungumzo ila hawajaweza kupatana, Kyiv ikikataa matakwa ya Moscow.
Ikulu ya Kremlin imepinga vikali wito wa Trump wa kufanyika mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Putin na Zelensky, wakisema hakuna mazingira salama ya kufanya mkutano huo.
Urusi inasema mazungumzo ya moja kwa moja yanafaa kutatua "chanzo cha vita" ikirejelea matakwa yao ya awali kabla ya kuanza vita mwezi Machi mwaka wa 2022.
Kati ya matakwa ya Urusi; ni kwa Ukraine kutoegemea upande wowote, kupunguza jeshi lake na kusitisha azimio lake la kujiunga na Nato.
Urusi pia inataka maeneo waliyoyadhibiti kutoka kwa Ukraine, kutambuliwa rasmi kuwa sehemu ya Urusi ikiwemo Crimea na maeneo mengine manne.
Kyiv nayo imesema haiwezi kubali kutangaza maeneo yaliyochukuliwa kuwa sehemu ya Urusi.
Wakulaumiwa ni Zelensky?
Kabla ya kurejea katika ikulu ya White House, Trump alisema Zelensky ni wa kulaumiwa katika vita hivyo.
"Zelesnky hangeruhusu vita hivyo kuanza" Trump alisema mwezi Oktoba 2024.
Ila vita hivi vilianza mwaka wa 2014, wakati Putin alidhibiti eneo la Crimea, na makundi mengine ya Urusi kuchukua maeneo tofauti mashariki mwa Ukraine.
Wakati huu, Zelensky hakuwa amejiunga na siasa bado. Kisha Putin akaivamia Ukraine miaka minane baadaye.
Ila rais wa Marekani amekuwa akiyumbayumba katika msimamo wake katika vita hivi wakati mwingine akionekana kuwa mkali dhidi ya Urusi.
"Nilidhani tumevimaliza vita hivi, ila tukimaliza kuzungumza, Putin anaenda anatekeleza mashambulizi mengine ya roketi na kulenga mji wa Kyiv na kuuwa watu" Trump alisema mwezi uliopita.
Trump alitangaza ushuru zaidi kwa mataifa yanayoshirikiana kibiashara na Urusi, na kuiwekea India ushuru wa 25% zaidi kama adhabu ya kununua mafuta kutoka Urusi, ila baadaye akaondoa ushuru huo baada ya mazungumzo.
Kauli za Putin kuhusu "Wanazi" na "mauaji ya kimbari" nchini Ukraine ni za kweli?
Mwanzo wa uvamizi wa 2022, Putin alisema anawalinda watu walioko mashariki mwa Ukraine dhidi ya "kuonewa na mauji ya kimbari " wakati wa vita eneo hilo.
Zaidi ya watu 14,000 walifariki pande zote mbili wakiwa mstari wa mbele wa vita kati ya 2014- 2022.
Ila Urusi inasema wanazi wa Ukraine walikuwa wakitekeleza mauaji ya kimbari katika maeneo yanayokaliwa na Urusi, madai ambayo kansela wa Ujerumani alisema "si ya kweli."
Kauli za Urusi kwamba "Wanazi wako madarakani Kyiv" pia si sahihi.
Ukraine ya sasa haina viongozi wengi bungeni kutoka mrengo wa kulia. Kando na hayo Zelensky ni myahudi, na jamaa zake wengi waliuawa na wanazi katika vita vya pili vya dunia.
Putin anamshtumu Zelesnky kuwa "fedheha kwa wayahudi."
Putin alishtumiwa kwa uhalifu wa kivita katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu mwaka wa 2024, mashtaka ambayo ikulu ya Kremlin ilikataa.
Nani anaonekana kushinda vita hivi?
Takriban miaka minne tangu vita hivyo kuzuka, wanajeshi wa Urusi na Ukraine bado wako katika mstari wa mbele wakipigana.
Hakuna upande ambao umeonekana dhahiri kuwa unashinda vita hivyo.
Urusi imedhibiti maeneo manne ya kusini na mashariki mwa Ukraine.
Uchumi wa Urusi na Ukraine zote zimeathirika na vita hivyo.
Watu wangapi wamefariki katika vita hivi?
Maelfu ya watu wamefariki tangu vita hivyo kuanza mwaka 2022.
Rais wa Ukraine alisema amewapoteza wanajeshi 55,000 ila mtandao wa ualosses.org, unasema kuwa wanajeshi waliofariki ni zaidi ya 92,000.
Zaidi ya raia 14,500 wamepoteza maisha yao nchini Ukraine, kulingana na ripoti za Umoja wa Mataifa, huku maafa zaidi yakirekodiwa mwaka wa 2025.
Urusi haijaweka wazi idadi ya wanajeshi waliofariki, ila makadirio ya BBC inaashiria kuwa kati ya wanajeshi 243,000 hadi 352,000 wamefariki.
Zaidi ya raia millioni sita wa Ukraine wamekimbilia mataifa mengine kwa usalama wao.
Wakati wa uvamizi huo, Putin alisema hiyo si "vita" bali oparesheni spesheli ya kijeshi. Ila mwaka wa 2024 alikubali kuwa ni vita akidai kuwa ilianzishwa na Kyiv.
Mahusiano ya kihistoria kati ya Urusi na Ukraine
Putin bado anaamini kuwa Ukraine inafaa kusalia chini ya ushawishi wa Urusi, kutokana na historia ya mataifa hayo mawili.
Kuanzia mwaka wa 1922 hadi 1991, Ukraine ilikuwa sehemu ya muungano wa Soviet, na raia wengi wa Ukraine wanazungumza kirusi, haswa maeneo ya mashiriki ikiwemo Volodymyr Zelensky.
Warusi wengi wanaiona Crimea kama eneo lao. Eneo hilo lilichukuliwa na Catherine the Great mwaka wa 1783, na kupewa Ukraine na kiongozi wa muungano wa Soviet Khrushchev, mwaka wa 1954.
Kuanzia mwaka wa 1991, Ukraine imekuwa taifa huru. Iliacha kutumia silaha zake za nyuklia mwaka wa 1994 ili kupokea ulinzi dhidi ya Urusi.
Tangu vita hivyo kuanza, raia wengi wameipinga Urusi na hata Zelensky ameacha kutumia lugha ya kirusi mbele ya umma.
Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula