Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanakijiji walivyokimbilia kuchimba dhahabu iliyopatikana karibu na zizi la ng'ombe
- Author, Nomsa Maseko
- Akiripoti kutoka, Springs
- Author, Richard Kagoe
- Author, Natasha Booty
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Watu wengi wamekimbilia kuchimba dhahabu katika eneo la makazi duni mashariki mwa mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, baada ya tangazo kutolewa siku chache zilizopita kuwa kuna dhahabu eneo hilo.
Mkaazi mmoja wa eneo hilo lililoko karibu na eneo la migodi la Springs alisema alipata chembe chembe za dhahabu akiwa analima karibu na zizi la ngombe.
Makumi ya watu sasa wamehamia eneo hilo wakichimba karibu na zizi la ngombe wakiwa na matuamaini ya kutajirika.
Wakiwa wamejihami na mapanga na majembe, wamekuwa wakichambua udongo katika eneo linalofanana na eneo la awali Afrika Kusini ilichimba dhahabu na kujitajirisha mwongo mmoja uliopita.
Eneo la Springs hapo awali ilikuwa mji wa dhahabu na wenye shughuli nyingi, lakini migodi yake ilifungwa miaka kadhaa iliyopita kwa sababu kina cha mashimo yalikuwa ndefu sana na hatari.
Idara ya madini Afrika Kusini, imekosoa vikali uchimbaji uliofanyika wiki hii katika makaazi ya Springs eneo la Gugulethu, na kusema ni kinyume cha sheria kwani inaharibu mazingira.
Baadhi ya wale waliokuwa wakichimba dhahabu eneo hilo wameiambia BBC kuwa waliweza kupata dhahabu na kuuza katika soko zisizo rasmi.
Kemikali hatari kama Zenaki na sodium cyanide zinatumika ili kutenganisha dhahabu na mawe.
"Tunajua ni kinyume cha sheria, tunataka serikali itupe leseni ya kuchimba madini ili tufanye kazi na tulipe ushuru." Mwanaume mmoja aliambia BBC.
Alielezea kuwa yeye ni baba wa watoto wawili na anahitaji kupata pesa ili awasomeshe na kununua chakula.
Mwanaume mwingine aliiambia BBC kuwa " Hii ndio kazi pekee ninayoijua. Imetusaidia wengi wetu kutokamatwa tukifanya maovu au uhalifu"
Gramu moja ya dhahabu inauzwa dola 100.
Kipato cha chini cha mshahara nchini Afrika kusini ni dola 368
Wengi waliokuwa wanachimba dhahabu waliiambia BBC kuwa wanatokea taifa jirani la Lesotho.
Mwendo wa saa nane mchana muda wa shule unapokamilika, watoto wengi walianza kufika eneo hilo la migodi.
Walienda nyumbani kwanza kubadilisha sare ya shule na kufika eneo hilo kuwasaidia wazazi wao kuchimba dhahabu.
Tulipozuru eneo hilo kama BBC tulipata ardhi hio ikiwa si imara.
"Uchimbaji usio na udhibiti unaweza kusababisha ardhi kutokuwa imara, na kuweka jamii zilizo karibu na hasa watoto katika hatari kubwa ya kujeruhiwa au kupoteza maisha," wizara ya madini ilionya katika taarifa yake Jumanne.
Uchimbaji haramu ni jambo la kawaida Afrika Kusini, na watu wengi wamefariki kwa miaka mingi wakifanya kazi katika mazingira hatarishi.
Wiki iliyopita, Rais Cyril Ramaphosa alisema kwamba atawatuma jeshi kuwasaidia polisi kupambana na magenge ya wahalifu na wachimbaji haramu nchini humo.
Mamlaka zinawalaumu wachimbaji hao haramu wanaojulikana kama "zama zamas", ambao wamejihami, hawana utambulisho, rai awa kigeni wanaojihusisha na magenge ya wahalifu.
Ila hakuna dhibitisho kuwa hivi ndivyo hali ilivyo eneo la Springs.
Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula na kuhaririwa na Ambia Hirsi