Chanjo moja
ya kupulizia puani inaweza kukulinda dhidi ya kikohozi, mafua, kamasi na aina
yote ya homa, pamoja na maambukizi ya bakteria kwenye mapafu, na pia inaweza
kupunguza mzio, wamesema watafiti wa Marekani.
Timu katika
Chuo Kikuu cha Stanford imefanya majaribio ya "chanjo yao ulimwengu
wote" kwa wanyama na bado inahitaji kufanya majaribio kwa binadamu.
Mtazamo wao
unaashiria "mabadiliko makubwa" ikilinganishwa na jinsi chanjo
zilivyobuniwa kwa zaidi ya miaka 200, wanasema.
Wataalamu
katika tasnia hiyo walisema utafiti huo ulikuwa "wa kusisimua sana"
licha ya kuwa katika hatua za awali na unaweza kuwa "hatua muhimu kufikiwa".
Chanjo za
sasa hufunza mwili kupambana na maambukizi aina moja. Chanjo ya surua hulinda
dhidi ya surua pekee na chanjo ya tetekuwanga hulinda dhidi ya tetekuwanga
pekee.
Hivi ndivyo
chanjo imekuwa ikifanyakazi tangu Edward Jenner alipoanzisha chanjo mwishoni
mwa karne ya 18.
Mbinu iliyoelezwa
katika jarida la Sayansi haifunzi mfumo wa kinga. Badala yake inaiga jinsi
seli za kinga zinavyowasiliana.
Inatolewa
kama dawa ya puani na huacha seli nyeupe za damu kwenye mapafu yetu -
zinazoitwa macrophages - zikiwa katika "tahadhari " na zikiwa tayari
kuanza kufanya kazi bila kujali ni maambukizi gani yanayojaribu kuingia.
Matokeo hayo
yalidumu kwa takriban miezi mitatu katika majaribio ya wanyama.
Watafiti
walionyesha kuwa hali hii ya utayari iliyoongezeka ilisababisha kupungua mara
100 hadi 1,000 kwa virusi vinavyoingia kwenye mapafu na kuingia mwilini.
Na kwa wale
walioingia kisiri, mfumo uliobaki wa kinga ulikuwa "tayari kuwakinga hawa wa
ndani kwa kasi kikubwa" alisema Profesa Bali Pulendran, profesa wa
mikrobiolojia na kinga mwilini huko Stanford.
Timu hiyo
ilionyesha kuwa chanjo hiyo pia inalinda dhidi ya aina mbili za bakteria
- Staphylococcus aureus na Acinetobacter baumannii.
Pulendran
aliiambia BBC: "Chanjo hii, tunayoiita chanjo ya ulimwengu wote, inatoa
mwitikio mpana zaidi ambao ni kinga sio tu kwa virusi vya mafua, sio virusi vya
Covid tu, sio virusi vya homa ya kawaida tu, bali dhidi ya karibu virusi vyote,
na bakteria wengi tofauti kama tulivyofanya majaribio, na hata vizio."
"Kanuni
ambayo chanjo hii inafanya kazi ni mabadiliko makubwa na kanuni ambayo chanjo
zote zimefanya kazi hadi sasa."
Jinsi
inavyoelekeza mfumo wa kinga kupambana na maambukizi pia ilionekana kupunguza
mwitikio wa vizio vya wadudu wa vumbi la nyumba - ambavyo ni kichocheo cha pumu
ya mzio.
"Huu ni
utafiti wa kusisimua sana," anasema Profesa Daniela Ferreira, profesa wa
chanjo katika Chuo Kikuu cha Oxford, ambaye hakuhusika katika utafiti huo.
Alisema
inaweza "kubadilisha jinsi tunavyowalinda watu kutokana na kikohozi cha
kawaida, mafua na maambukizo mengine ya kupumua" ikiwa matokeo
yatathibitishwa katika tafiti za wanadamu.
"Mojawapo
ya yenye tija" katika utafiti huo ilikuwa maelezo wazi ya jinsi aina hii
mpya ya chanjo inavyofanya kazi, aliongeza.
Ferreira
alisema utafiti huo "unaweza kuashiria kupigwa kwa hatua kubwa" ikitoa
ulinzi dhidi ya maambukizi ambayo "yamekuwa tatizo kubwa" kwetu sote.