Meli za kubeba ndege za kivita za Marekani zaonekana zikielekea Mashariki ya kati
Tunatumia zana zinazopatikana kufuatilia safari za ndege kama Flightradar24 ili kuangalia mienendo ya hivi punde ya ndege za kijeshi za Marekani huku Washington ikiendelea kuimarisha vikosi vyake katika Mashariki ya Kati.
Muhtasari
Wanasheria walaani hukumu 'hafifu' dhidi ya wanajeshi wa Cameroon waliowaua raia 21
Wanasheria walaani hukumu 'hafifu' dhidi ya wanajeshi wa Cameroon waliowaua raia 21
Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Maelezo ya picha, Mzozo katika eneo la Anglophone umedumu kwa karibu muongo mmoja
Wanajeshi watatu wa Cameroon wamehukumiwa kifungo jela kwa kuhusika katika mauaji ya takriban raia 21 katika eneo lenye matatizo la lugha ya Kiingereza nchini humo.
Vifungo vya jela kwa uhalifu huo, ambao ulifanyika miaka sita iliyopita katika eneo la Kaskazini Magharibi, ni kati ya miaka mitano hadi 10 kwa kila mtu.
Mahakama ya kijeshi hapo awali iliwapata wanajeshi hao na hatia ya mauaji, uchomaji moto na uharibifu - jambo ambalo ni nadra sana katika nchi ambapo wanajeshi ni nadra kuhukumiwa kwa uhalifu dhidi ya raia.
Hata hivyo, mawakili wa waathiriwa waliambia BBC kuwa wamesikitishwa na urefu wa vifungo vya jela vilivyotolewa siku ya Alhamisi, na kuwaita "isiyo na maana".
Meli ya kivita ya USS Gerald R Ford imeonekana ikipitia Mlango-Bahari wa Gibraltar
Chanzo cha picha, David Parody
Maelezo ya picha, BBC Verify pia ilizungumza na mpiga picha, David Parody, ambaye alisema picha hizo zilipigwa leo.
BBC Verify imethibitisha picha zilizopigwa leo asubuhi na kuchapishwa kwenye X zinazoonyesha shehena ya ndege ya Marekani USS Gerald R Ford ikipitia Mlango-Bahari wa Gibraltar.
Picha hizo - zilizochukuliwa kutoka Gibraltar - zinaonyesha meli kubwa zaidi ya kivita duniani ikiwa inaelekea mashariki kutoka Atlantiki hadi Mediterania.
Pia tumethibitisha kwa kutumia ufuatiliaji wa meli kwamba moja ya meli katika kundi la meli za kubeba ndege za kivita za Ford, USS Mahan, ilipitia njia hiyo.
Katika picha hii ya kwanza meli ya kubeba ndege za kivita inaonekana kwa mbali ikipita karibu na milima ya.
Tulitumia ufuatiliaji wa meli ili kuthibitisha meli nyingine mbili kwenye picha pia zilikuwa katika eneo hilo wakati huo.
Urusi na Iran katika mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Lavrov na mwenzake wa Iran Araqch
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilitangaza Ijumaa (tarehe 20 Februari) kupitia chaneli yake ya Telegram kwamba Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amezungumza na mwenzake wa Iran, Abbas Araghchi kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi alisema jana kuwa shambulio la Marekani dhidi ya Iran litakuwa na madhara makubwa.
Pia alisema: "Ninafuatilia kwa karibu hisia za nchi za Ghuba ya Kiarabu katika eneo hilo.
Hakuna anayetaka kuzidisha mvutano. Kila mtu anajua kwamba hii ni kucheza na moto."
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, kushadidi mivutano hiyo kunabatilisha hatua chanya zilizopigwa katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kuboresha uhusiano wa Iran na nchi jirani hususan Saudi Arabia.
Waziri wa Mafuta wa Iran: Ushirikiano wa mafuta na gesi na Marekani unawezekana
Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa Mafuta wa Iran amesema "kila kitu kinawezekana" kuhusiana na uwezekano wa ushirikiano kati ya Tehran na Washington katika nyanja za mafuta na gesi.
Katika mahojiano na Shirika la Habari la ILNA, Mohsen Paknejad hatahivyo hakutaja muda wa kuanza kwa ushirikiano huo.
Hamid Ghanbari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya kiuchumi pia siku chache zilizopita alisema: "Maslahi ya pamoja katika nyanja za mafuta na gesi, nyanja za pamoja, uwekezaji wa madini na hata ununuzi wa ndege yamejumuishwa katika mazungumzo na Marekani."
Pia alisema kuwa Marekani haikunufaika kiuchumi katika makubaliano ya awali ya nyuklia, lakini "wakati huu, ili makubaliano hayo yawe endelevu, ni muhimu Marekani pia iweze kunufaika katika maeneo yenye faida kubwa na za haraka kiuchumi."
Mbunge wa Tunisia afungwa miezi minane jela kwa kumdhihaki rais
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais Kais Saied ameshutumiwa kwa kuminya uhuru wa kisiasa
Mahakama ya Tunisia imemhukumu mbunge mmoja kifungo cha miezi minane jela kutokana na kuchapisha mitandao ya kijamii akimkejeli Rais Kais Saied kufuatia mafuriko yaliyosababisha vifo vya hivi karibuni.
Ahmed Saidani alikamatwa mapema mwezi huu baada ya kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ziara za Saied katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko, akimtaja kuwa "kamanda mkuu wa usafi wa mazingira na mifereji ya maji ya mvua".
Alifungwa gerezani siku ya Alhamisi kwa mashtaka ya kuwatusi wengine kupitia mitandao ya mawasiliano, afisa wa mahakama alisema.
Wakili wa Saidani, Houssem Eddine Ben Attia, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mteja wake anafunguliwa mashitaka chini ya sheria ya mawasiliano dhidi ya "kuwadhuru wengine kupitia mitandao ya kijamii", kosa ambalo linaweza kuadhibiwa hadi miaka miwili jela.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa kile wanachoeleza kuwa ni kukithiri kwa ukandamizaji wa Saied dhidi ya wapinzani tangu aliposimamisha bunge la Tunisia mwaka 2021 na kuanza kutawala kwa amri.
Saidani, ambaye aliwahi kuwa mfuasi wa uimarishaji wa mamlaka ya Saied na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani, hivi karibuni amegeuka kuwa mkosoaji mkubwa wa rais.
Katika chapisho lake la Facebook, mbunge huyo alimkejeli rais kwa "kuchukua hobby ya kupiga picha na maskini " wakati akizuru maeneo yaliyofurika katika mji mkuu, Tunis na maeneo mengine ya nchi.
Ndege zaidi za Kijeshi za Marekani zaonekana zikielekea mashariki ya kati
Chanzo cha picha, FLIGHT RADAR24
Tunatumia
zana zinazopatikana hadharani za kufuatilia safari za ndege kama Flightradar24
ili kuangalia mienendo ya hivi punde ya ndege za kijeshi za Marekani huku
Washington ikiendelea kuimarisha vikosi vyake katika Mashariki ya Kati.
Rais
Donald Trump ameitaka Iran kuafikiana kuhusu mpango wake wa nyuklia na kuonya
kwamba vinginevyo "mambo mabaya yatatokea".
Hii ni
picha ya skrini kutoka Flightradar24 inayoonyesha ndege sita za kijeshi za
Marekani zikiingia na kutoka Mashariki ya Kati mwendo wa saa 10:00 GMT siku ya
Ijumaa.
Pamoja na safari za ndege za jeshi la anga pia nimeona ndege mbili za upelelezi za Jeshi la Wanamaji la Marekani P-8 Poseidon juu ya Mediterania - moja ikielekea magharibi kuelekea Gibraltar na nyingine nje ya pwani ya Crete.
Mpandaji milima Austria apatikana na hatia baada ya mpenzi wake kuganda hadi kufa kwenye mlima
Chanzo cha picha, Bergrettung Kals
Mpanda mlima
mmoja kutoka Austria amepatikana na hatia ya mauaji ya uzembe baada ya mpenzi
wake kuganda hadi kufa kwenye mlima mrefu zaidi nchini Austria mwaka jana.
Mwanamume
huyo, aliyetajwa kwa jina la Thomas P pekee kwa mujibu wa sheria za faragha za
Austria, amepewa kifungo cha miezi mitano ya adhabu ya mahakama ambayo
haitumiki isipokuwa uhalifu mwingine umefanywa ndani ya kipindi maalum na
kutozwa faini ya €9,600 (£8,400).
Mpenzi wake,
Kerstin G, alifariki kutokana na hypothermia (dharura ya matibabu inayotokea
wakati mwili unapoteza joto kwa kasi zaidi kuliko inavyoweza kuzalisha), wakati
wa safari ya kupanda mlima Grossglockner mnamo mwezi Januari mwaka 2025.
Katika
taarifa iliyotumwa kwa BBC, mahakama ilisema inachukulia rekodi safi ya awali
ya Thomas P na kupotea kwa mtu wa karibu naye "kuwa sababu za kupunguza
ukali wa kesi" hiyo.
Ilisema pia
ilizingatia "mjadala wa umma kwenye mitandao ya kijamii, ambao ulikuwa
unamtia hatiani mshtakiwa".
Jaji,
Norbert Hofer, ambaye mwenyewe ni mpandaji milima mwenye uzoefu ambaye anafanya
kazi na timu za uokoaji milimani na helikopta huko Tyrol, alisema Thomas P
alikuwa Mpanda milima mzuri, lakini mpenzi wake hakuwa na uzoefu kama wake.
Alisema
wanandoa hao walipaswa kurudi nyuma kwani Kerstin G hakuwa na uzoefu wa kutosha
katika hali ya baridi kali.
Mahakama pia
ilisikiliza kutoka kwa Andrea B, mpenzi wa zamani wa Thomas P, ambaye alielezea
jinsi alivyomwacha peke yake katika ziara ya awali huko Grossglockner mnamo mwaka
2023.
Alisema
alikuwa amefika mwisho akihisi kizunguzungu na taa yake ya mbele ilikuwa
imezimwa.
Alisema
alikuwa akilia na kupiga kelele ghafla alipotoweka, akitembea mbele na kumwacha
nyuma.
Hamas yapiga kura kumchagua kiongozi mpya wa mpito, chanzo cha habari kimeiambia BBC
Chanzo cha picha, Reuters
Hamas
inafanya uchaguzi wa kiongozi mpya wa mpito, afisa mwandamizi wa Palestina
anayefahamu masuala ya kundi hilo la waasi ameiambia BBC.
Upigaji kura
unafanyika kote Gaza, Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na miongoni mwa wanachama
wa Hamas kwingineko.
Matokeo
yanaweza kuashiria mwelekeo ambao kundi hilo inakusudia kuchukua - hasa wakati
Marekani na wapatanishi wengine wanapojadili utawala wa Gaza baada ya vita,
juhudi za ujenzi upya na hali ya baadaye ya vikundi vyenye silaha huko.
Uchaguzi huo
unakuja baada ya viongozi wengi wakuu wa Hamas kuuawa katika mashambulizi ya
Israel kufuatia mashambulizi ya kundi hilo ya tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya
Israeli, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 251 walichukuliwa
mateka.
Watu huko
Gaza tayari wamepiga kura zao kwa siri, kulingana na chanzo hicho, lakini
haijulikani wazi kama mchakato huo umekamilika kwingineko.
Kiongozi
mpya atakapotangazwa, atashikilia wadhifa huo kwa mwaka mmoja.
Hamas
inatawala Ukanda wa Gaza na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa na uungwaji
mkono unaoongezeka katika eneo la Ukingo wa Magharibi, ingawa shughuli zake
huko zimezuiliwa sana na jeshi la Israeli na vikosi vya usalama vya Mamlaka ya
Palestina.
Mkataba wa
kusitisha mapigano unaoungwa mkono na Marekani huko Gaza ulianza kutekelezwa mnamo
mwezi Oktoba, na mazungumzo yanaendelea kuhusu awamu za baadaye za makubaliano
hayo.
Chanjo moja inaweza kukulinda dhidi ya kikohozi, mafua na homa, watafiti wanasema
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanjo moja
ya kupulizia puani inaweza kukulinda dhidi ya kikohozi, mafua, kamasi na aina
yote ya homa, pamoja na maambukizi ya bakteria kwenye mapafu, na pia inaweza
kupunguza mzio, wamesema watafiti wa Marekani.
Timu katika
Chuo Kikuu cha Stanford imefanya majaribio ya "chanjo yao ulimwengu
wote" kwa wanyama na bado inahitaji kufanya majaribio kwa binadamu.
Mtazamo wao
unaashiria "mabadiliko makubwa" ikilinganishwa na jinsi chanjo
zilivyobuniwa kwa zaidi ya miaka 200, wanasema.
Wataalamu
katika tasnia hiyo walisema utafiti huo ulikuwa "wa kusisimua sana"
licha ya kuwa katika hatua za awali na unaweza kuwa "hatua muhimu kufikiwa".
Chanjo za
sasa hufunza mwili kupambana na maambukizi aina moja. Chanjo ya surua hulinda
dhidi ya surua pekee na chanjo ya tetekuwanga hulinda dhidi ya tetekuwanga
pekee.
Hivi ndivyo
chanjo imekuwa ikifanyakazi tangu Edward Jenner alipoanzisha chanjo mwishoni
mwa karne ya 18.
Mbinu iliyoelezwa
katika jarida la Sayansi haifunzi mfumo wa kinga. Badala yake inaiga jinsi
seli za kinga zinavyowasiliana.
Inatolewa
kama dawa ya puani na huacha seli nyeupe za damu kwenye mapafu yetu -
zinazoitwa macrophages - zikiwa katika "tahadhari " na zikiwa tayari
kuanza kufanya kazi bila kujali ni maambukizi gani yanayojaribu kuingia.
Matokeo hayo
yalidumu kwa takriban miezi mitatu katika majaribio ya wanyama.
Watafiti
walionyesha kuwa hali hii ya utayari iliyoongezeka ilisababisha kupungua mara
100 hadi 1,000 kwa virusi vinavyoingia kwenye mapafu na kuingia mwilini.
Na kwa wale
walioingia kisiri, mfumo uliobaki wa kinga ulikuwa "tayari kuwakinga hawa wa
ndani kwa kasi kikubwa" alisema Profesa Bali Pulendran, profesa wa
mikrobiolojia na kinga mwilini huko Stanford.
Timu hiyo
ilionyesha kuwa chanjo hiyo pia inalinda dhidi ya aina mbili za bakteria
- Staphylococcus aureus na Acinetobacter baumannii.
Pulendran
aliiambia BBC: "Chanjo hii, tunayoiita chanjo ya ulimwengu wote, inatoa
mwitikio mpana zaidi ambao ni kinga sio tu kwa virusi vya mafua, sio virusi vya
Covid tu, sio virusi vya homa ya kawaida tu, bali dhidi ya karibu virusi vyote,
na bakteria wengi tofauti kama tulivyofanya majaribio, na hata vizio."
"Kanuni
ambayo chanjo hii inafanya kazi ni mabadiliko makubwa na kanuni ambayo chanjo
zote zimefanya kazi hadi sasa."
Jinsi
inavyoelekeza mfumo wa kinga kupambana na maambukizi pia ilionekana kupunguza
mwitikio wa vizio vya wadudu wa vumbi la nyumba - ambavyo ni kichocheo cha pumu
ya mzio.
"Huu ni
utafiti wa kusisimua sana," anasema Profesa Daniela Ferreira, profesa wa
chanjo katika Chuo Kikuu cha Oxford, ambaye hakuhusika katika utafiti huo.
Alisema
inaweza "kubadilisha jinsi tunavyowalinda watu kutokana na kikohozi cha
kawaida, mafua na maambukizo mengine ya kupumua" ikiwa matokeo
yatathibitishwa katika tafiti za wanadamu.
"Mojawapo
ya yenye tija" katika utafiti huo ilikuwa maelezo wazi ya jinsi aina hii
mpya ya chanjo inavyofanya kazi, aliongeza.
Ferreira
alisema utafiti huo "unaweza kuashiria kupigwa kwa hatua kubwa" ikitoa
ulinzi dhidi ya maambukizi ambayo "yamekuwa tatizo kubwa" kwetu sote.
Uingereza haijatoa ruhusa kwa Marekani kutumia kambi zake za kijeshi kushambulia Iran
Chanzo cha picha, Reuters
Serikali ya
Uingereza haijatoa ruhusa kwa Marekani kutumia kambi za kijeshi za Uingereza kama
sehemu ya kuunga mkono mashambulizi yanayoweza kutokea ya Marekani dhidi ya
Iran, BBC inafahamu hilo.
Siku za
nyuma, Marekani ilitumia kambi ya RAF Fairford, huko Gloucestershire, na eneo la nje ya
Uingereza la Diego Garcia, katika Bahari ya Hindi, kutekeleza mashambulizi
katika eneo la Mashariki ya Kati.
Gazeti la
Times linaripoti kwamba ukosoaji wa hivi karibuni wa Rais wa Marekani
Donald Trump kuhusu makubaliano ya Sir Keir Starmer ya kukabidhi
Visiwa vya Chagos kwa Mauritius na kukodisha tena kambi ya pamoja ya kijeshi
kati ya Uingereza na Marekani kulisababishwa na Uingereza kutotoa ruhusa ya
kutumia kambi hizo.
Msemaji wa
serikali ya Uingereza alisema: "Kama kawaida, hatutoi maoni yoyote kuhusu
masuala ya uendeshaji."
Marekani
imekuwa ikiishinikiza Iran kukubali kupunguza mpango wake wa nyuklia.
Imetishia
kufanya mashambulizi iwapo itashindwa kufanya hivyo na imepeleka meli, ndege za
kivita na zana zingine za kijeshi eneo hilo kwa ajili ya maandalizi ya
mashambulizi yanayoweza kufanyika.
Wakati huo
huo, hatua imeripotiwa kupigwa katika mazungumzo kati ya wapatanishi wa
Marekani na Iran nchini Uswisi.
Siku ya
Alhamisi, Trump alisema dunia itajua "ndani ya siku 10 zijazo" ikiwa
Marekani itafikia makubaliano na Iran au kuchukua hatua za kijeshi.
Msemaji wa
serikali ya Uingereza alisema: "Kuna mchakato wa kisiasa unaoendelea kati
ya Marekani na Iran, ambao Uingereza inaunga mkono."
"Iran
haipaswi kamwe kutengeneza silaha za nyuklia, na kipaumbele chetu ni usalama
katika eneo hilo."
Sir Keir
alizungumza na Trump kwa simu siku ya Jumanne, baada ya serikali ya Marekani kuunga
mkono rasmi makubaliano ya Chagos.
Interpol yafanya msako mkali dhidi ya ulaghai Afrika
Shirika la polisi wa kimataifa Interpol limesema vyombo
vya kutekeleza sheria kutoka nchi 16 za Afrika vimefanikiwa kupata zaidi ya
dola milioni 4.3 na kukamata watu 651, katika msako mkali dhidi ya ulaghai wa
kimataifa wa mtandaoni.
Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Interpol ilisema
hatua hiyo iliyopewa jina la Operesheni Red Card 2.0 ilichukua muda wa wiki
nane, kuanzia tarehe 8 Desemba 2025 hadi Januari 30 mwaka huo.
Baadhi ya nchi zilizoshiriki katika operesheni hiyo ni
pamoja na Angola, Cameroon, Côte d'Ivoire, Kenya, Nigeria na Zimbabwe.
Ikizungumzia kesi maalum, taarifa ya shirika hilo
ilionyesha kuwa polisi wa Nigeria walizuia njama za mtandao wa wahalifu za kuwalaghai
watu kupitia miradi ya uwekezaji yenye mavuno mengi.
Walifuta zaidi ya akaunti 1000 za ulaghai wa mitandao ya
kijamii na kugundua jengo linalotumika kama msingi wa uhalifu huo.
Wakati huo huo, maafisa wa utekelezaji wa sheria wa Kenya
na Ivory Coast walikamata mamia ya watu waliohusishwa na uwekezaji na miradi ya
mikopo ya simu, wakikamata vifaa kadhaa vilivyotumika katika shughuli hizo
haramu.
"Makundi haya ya uhalifu wa mtandao yanaleta madhara
makubwa ya kifedha na kisaikolojia kwa watu binafsi, biashara na jumuiya nzima
kwa ahadi zao za uongo," alisema Neal Jetton, Mkurugenzi wa Uhalifu wa shirika
la Interpol.
Interpol ilisema ilichangia kwa kushirikisha wengine
taarifa muhimu za kijasusi pamoja na ubadilishanaji habari kwa wakati halisi na
mafunzo juu ya matumizi ya zana za uchunguzi wa kidijitali.
Kwa ujumla, operesheni hiyo ilifichua ulaghai
unaohusishwa na hasara ya zaidi ya dola milioni 45 na kubaini zaidi ya
waathiriwa 1000, wengi wao kutoka Afrika.
Andrew aachiliwa huru baada ya kukamatwa kwa kwenda kinyume na maadili ya uongozi
Chanzo cha picha, Reuters
Andrew
Mountbatten-Windsor ameachiliwa huru huku uchunguzi ukiendelea kufuatia
kukamatwa kwake kwa tuhuma za utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma.
Mfalme
Charles III alisema "sheria lazima ichukue mkondo wake" akijibu
kukamatwa kwa Andrew na kwamba anaunga mkono polisi "na kutoa ushirikiano
wake kamili na wa dhati".
Polisi hapo
awali walisema walikuwa wakifikiria kumchunguza Andrew kuhusu madai
yanayohusiana na uhusiano wake na marehemu Jeffrey Epstein, mhalifu wa kingono
na walikuwa wakipitia madai kwamba wawili hao walishirikishana nyenzo za siri.
Mawasiliano
kati ya wawili hao yalionekana miongoni mwa sehemu ya faili zilizotolewa na
serikali ya Marekani.
Katika
taarifa iliyosasishwa Alhamisi jioni, Polisi wa Thames Valley walithibitisha
kwamba Andrew "ameachiliwa huru huku uchunguzi" ukiendelea.
Iliongeza kuwa msako uliokuwa unafanyika huko Norfolk sasa umekamilika.
Mwanamfalme
huyo wa zamani alipigwa picha akiwa amelala nyuma kwenye kiti cha nyuma cha
gari baada ya kutoka kituo cha polisi cha Aylsham.
Mwanawe Robert Mugabe akamatwa Afrika Kusini kwa tuhuma za kujaribu kuua
Chanzo cha picha, Anadolu Agency via Getty Images
Polisi
nchini Afrika Kusini wamemkamata mtoto wa mwisho wa Rais wa zamani wa Zimbabwe,
Robert Mugabe, ambaye anakabiliwa na shtaka la kujaribu kuua baada ya
kuripotiwa tukio la ufyatuaji risasi katika nyumba moja kwenye kitongoji cha
kifahari cha Johannesburg.
Bellarmine
Mugabe, mwenye umri wa miaka 28, alikamatwa baada ya mwanaume mwenye umri wa
miaka 23, anayeaminika kuwa mtunza bustani, kupigwa risasi na kujeruhiwa.
Maafisa waliokuwa
wakisaka nyumba iliyoko Hyde Park, ambapo Mugabe alikuwa akiishi, wamepata
risasi lakini hakuna bunduki, polisi wamesema.
Bellarmine
Mugabe ni mtoto wa mwisho wa Robert na mkewe wa pili Grace Mugabe. Robert
Mugabe, ambaye alifariki mwaka wa 2019, aliiongoza Zimbabwe kwa miaka 37 kabla
ya kufurushwa madarakani akiwa na umri wa miaka 93 mwaka wa 2017.
Mwanamume
mwingine amekamatwa pamoja na Bellarmine Mugabe huku wachunguzi wakiendelea na
kazi yao, msemaji wa polisi Kanali Dimakatso Nevhuhulwi alisema.
Wawili hao
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani "hivi karibuni", kulingana na
taarifa ya polisi.
Polisi bado
hawajamtaja rasmi Bellarmine Mugabe kama mmoja wa waliokamatwa, lakini
waandishi wa habari waliokuwepo eneo la tukio walimwona akiwa amefungwa pingu
na ametajwa sana na vyombo vya habari vya ndani.
Mwathiriwa
yuko hospitalini akiwa katika hali mbaya baada ya kupigwa risasi mara moja,
msemaji huyo aliongeza.
Katika
taarifa iliyotolewa nje ya nyumba hiyo, Nevhuhulwi alisema washukiwa hao wawili
"hawajatuambia bunduki hiyo iko wapi, na hawasemi chochote kuhusu bunduki
hiyo".
Dunia ina siku 10 kuona ikiwa Iran inafikia makubaliano au 'kitu kibaya kitokee' - Trump
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais Donald
Trump amesema dunia itajua "ndani ya siku 10 zijazo" kama Marekani
itafikia makubaliano na Iran au kuchukua hatua za kijeshi.
Katika
mkutano wa uzinduzi wa Bodi yake ya Amani huko Washington DC, Trump alisema
kuhusu mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu juu ya mpango wake wa nyuklia:
"Lazima tufikie makubaliano yenye tija vinginevyo mambo mabaya yatatokea."
Katika siku
za hivi karibuni, Marekani imeongeza vikosi vya kijeshi Mashariki ya Kati, huku
hatua ikisemekana kupigwa katika mazungumzo kati ya wapatanishi wa Marekani na
Iran nchini Uswisi.
Wabunge wa
chama cha Democrat, na baadhi ya Warepublican, wamepinga hatua yoyote ya
kijeshi kuchukuliwa nchini Iran bila idhini ya bunge.
Katika
maelezo yake, Trump alibainisha kuwa Wajumbe Maalum Steve Witkoff na Jared
Kushner, ambaye pia ni mkwe wa Trump, walikuwa na "mikutano yenye tija sana"
na Iran.
"Imedhihirika,
kwa miaka mingi kuwa si rahisi kufanya makubaliano yenye maana na Iran,"
alisema. "Vinginevyo, mambo mabaya yatatokea."
Siku moja kabla,
Waziri wa habari wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alionya kwamba Iran itafanya
la "busara sana" kufikia makubaliano na Marekani, akiongeza kwamba
Trump bado alikuwa na matumaini ya suluhisho la kidiplomasia kuhusu mpango wa
nyuklia wa Tehran.
Makombora na
ndege za ivita za Marekani zilishambulia vituo vitatu vya nyuklia vya Iran mnamo
mwezi Juni mwaka jana, na Ikulu ya White House iliripotiwa kujadili chaguzi
mpya za mashambulizi wiki hii.
Vikosi vya
Marekani vimekuwa vikiongeza uwepo wao katika eneo hilo katika wiki za hivi
karibuni, ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa meli ya kivita ya USS Abraham
Lincoln.
Picha za
setilaiti pia zimeonyesha Iran ikiimarisha vifaa vya kijeshi, na Kiongozi Mkuu
wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamanei, amechapisha ujumbe kwenye mitandao ya
kijamii akitishia vikosi vya Marekani.
"Rais
wa Marekani husema kila mara kwamba Marekani imetuma meli ya kivita kuelekea
Iran. Bila shaka, meli ya kivita ni kifaa hatari cha kijeshi," moja ya ujumbe
wa Khamenei ulisema.
Wabunge
kadhaa wa Bunge la Marekani wameonyesha kupinga hatua yoyote ya kijeshi dhidi
ya Iran.