Jinsi sakata ya Epstein inavyokuza propaganda za Urusi

Putin akiwafananisha viongo wa juu wa mataifa ya Magharibi kama "kundi la mpira wa wanyama wa kutisha" mnamo Februari 2024

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Putin akiwafananisha viongo wa juu wa mataifa ya Magharibi kama "kundi la mpira wa wanyama wa kutisha" mnamo Februari 2024
    • Author, BBC Monitoring
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Kwa waandishi wa habari la Urusi, sakata ya Jeffery Epstein inaonekana kama fursa ya mwaka ya kutoa dukuduku la moyoni kwa tumia maneno kama "si tuliwaambia". Faili za Epstein ni uthibitisho wa masimulizi ya muda mrefu ya Kremlin kuhusu kuzorota kwa maadili ya Magharibi na unyanyasaji wa kijinsia wa dhidi ya watoto.

Televisheni ya taifa ya Urusi kila siku imekuwa ikiangazia kwa kina taarifa zinazohusiana na faili za Estein tangu zilipotolewa hadharani, taarifa kuu ya Rossiya 1, Channel One na NTV zikiitengea suala hilo hadi dakika tisa.

"Wale waliokuwa wakijidai kuwa mfano bora wa maadili ya kijamii wamekuwa na uhusiano wa karibu na mnyasaji wa kingono wa kimataifa," mwandishi wa Rossiya 1 wa Marekani alitangaza tarehe 4 Februari.

"Wale ambao walizungumza kwa sauti kubwa kuhusu umuhimu wa kudumisha msingi wa sheria wenyewe hawazingati sheria, "aliongeza.

Siku hiyo hiyo, Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi Maria Zakharova aliiambia Radio Sputnik kwamba ni vigumu kufuatilia matukio ''bila kupatwa na kichefuchefu," kuashiria kauli ya Rais Vladimir Putin ya mwaka 2024 dhidi ya watu mashuhuri wa mataifa ya magharibi kwamba ni "kundi la kutisha" la watu ''walijinufaisha bila kujali athari za vitendo vyao kwa karne kadhaa".

Habari zaidi zimeongeza nadharia za njama za QAnon na Pizzagate-kama vile mila za kishetani na ulaji nyama huku zikimlinda kwa uangalifu Rais wa Marekani Donald Trump. NTV ilisisitiza kuwa FBI "haizingatii data hiyo kuwa ya kuaminika" inapokuja kwake.

Vyombo vya habari vya serikali pia vimejaribu kuingiza Ukraine katika simulizi, na madai yasiyo na msingi kwamba Volodymyr Zelensky " huenda anauhusika katika biashara ya ulanguzi wa watu."

Je, taarifa potofu zinaenezwa vipi mtandaoni?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Harakati hizi haziendelelezwi kupitia vyombo vya habari pekee bali zinafanyika pia mitandaoni.

Mtandao wa roboti unaohusishwa na Kremlin "Matryoshka" umezindua kampeni iliyoratibiwa ya kutumia faili za Epstein, kulingana na watafiti katika mradi wa Bot Blocker ambao hufuatilia shughuli za Urusi kwenye mitandao ya kijamii.

Tangu tarehe 30 Januari, taarifa ghushizilizo na nembo za mashirika makubwa ya habari ikiwa ni pamoja na Reuters, Al Jazeera na Libération ta Ufaransa zimefurika mitandao ya X, Telegram, na majukwaa mengine ya kijamii.

Miongoni mwa madai yaliyotolewa ni: kwamba watoto wa Ukraine ni "rasilimali kuu" katika operesheni ya Epstein baada ya maandamano ya 2014, na Zelensky alidaiwa kuwasiliana na wageni wa kisiwa cha Epstein; kwamba Emmanuel Macron alitembelea kisiwa hicho mara 18 katika miezi 18; na kwamba New Caledonia imekuwa "kisiwa kipya cha Epstein" chini ya ulinzi wa serikali ya Ufaransa.

Gazeti la insider limethibitisha kuwa hakuna ripoti yoyote kati ya hizi iliyoonekana kwenye akaunti halisi za mitandao ya kijamii za mashirika ya habari yaliyotajwa.

Vyombo vya habari vya serikali ya Urusi pia vinaashiria kufichua faili zinamhusisha Zelensky na biashara haramu ya binadamu.

Chanzo? Barua iliyosheheni lugha chafu iliyojaa makosa ya - ikijumuisha makosa mengi ya tahajia ya jina la Zelensky - iliyotumwa kwa mamlaka ya Marekani na mtu asiyejulikana.

Gazeti la Insider liliripoti kwamba barua hiyo pia ilidai hatua kutoka kwa "Rais Trump na Bw Putin" na kudai kwamba Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alikuwa "Cyril Epstein".

Wakati, barua hiyo ilipofuatiliwa ilitoweka ghafla kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, kwani inaonekana iliondolewa pamoja na maelfu ya hati zingine.

Je, Epstein alikuwa na uhusiano na ujasusi wa Urusi?

Faili hizo zinaripotiwa maelezo zaidi ya 1,000 ya Rais Vladimir Putin na takriban 6,000 za Urusi.

Gazeti la Daily Mail, likinukuu "vyanzo vya kijasusi ambavyo havikufichuliwa, viliripoti kwamba mtandao wa Epstein huenda ulifanya kazi kama operesheni ya "mtego wa asali" wa kukusanya habari za kijasusi za Urusi - madai ambayo yameibua mzozo wa kisiasa.

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk alitangaza kuwa serikali yake itachunguza uhusiano kati ya Epstein na idara za ujasusi za Urusi.

"Hii inaweza tu kumaanisha kuwa wanamiliki nyenzo za kali ambayo zinaweza kuwathiri baadhi ya viongozi wengi ambao bado wanahudumu katika nyadhifa za juu serikalini," alisema.

Vyombo huru vya habari vimebaini nini?

Vyombo huru vya Urusi vimekuwa vikichunguza "nyayo ya Urusi" inayoonekana kwenye faili - ingawa kutajwakwa taifa hilo kwenye nyaraka hizo hakumaanishi kosa lolote.

Idhaa za Urusi ya RFE/RL iliangazi kutajwa mara nyingi kwa "wasichana wa Urusi" na juhudi zinazoashiria kupanga ziara nchini Urusi, pamoja na barua pepe ya 2010 ambayo Epstein aliuliza ikiwa anahitaji visa, akiongeza: "Nina rafiki wa Putin, je, nimfikie?"

Kituo cha Meduza ambacho kinaendesha shughuli zake nje ya nchi kiliripoti kwamba Epstein aligusia uwezekano wa kukutana na rais wa Urusi na kudai kuwa alikataa mwaliko wa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi wa St Petersburg mnamo 2013 kwa sababu "masharti hayakuzingatia maslahi yake.''

Chombo hicho hata hivyo kilisisitiza, kwamba chanzo walichozingatia hakitoi ushahidi kwamba wawili hao waliwahi kukutana. Kremlin pia inakanusha hakuna mkutano wowote uliofanyika.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi