Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini unapaswa kufungua kwa kula tende wakati wa Ramadhan?
Waumini wa dini ya Kiislamu kote duniani baada ya kufunga siku nzima, wengi wao wakati wa jioni wanapofungua wao hula tende.
Katika mwezi wa Ramadhan, ambapo ni siku 30 za kufunga na kuomba, waislamu hujizuia kula na kunywa kuanzia asubuhi hadi machweo jua linapotua, ili kuzingatia nguzo tano za dini ya Kiislamu.
Nabii Muhammad alipendekeza kufungua mfungo na tende, na matunda hayo yametajwa kwenye Quran, kitabu takatifu cha waislamu.
Ila kando na kipengele chake cha kidini, tunda hili lina manufaa yake kiafya na ina pendekezwa kwa wale wanaofunga kuitumia.
Manufaa yake kiafya
Shahnar Bashir, mtalaam wa lishe kutokea Uingereza ambaye amekuwa akifuatilia mfungo wa Ramadhan anasema "Ukifungua, mwili wako utajaribu kuzalisha glukosi kwasababu inahitaji nguvu"
Sukari inayopatikana kwa tende husaidia kuongeza viwango ya sukari mwilini kwa haraka ikilinganishwa na vyakula vingine ambavyo huchukua muda kumengenywa. Bashir anaongezea kuwa "tende ni matunda ya kipekee kwa sababu yana sukari na kabohaidreti"
Hii ina maanisha kuwa tunda hilo hukupa nguvu siku nzima wakati ambapo hujakula kwa muda mrefu. Pia ina vitamini B6,A,K na madini ya Iron ambayo huhakikisha mwili unapata mdini yote hitajika kwa muda mfupi.
Kuhakikisha mwili ina maji ya kutosha
Licha ya kuwa matunda kavu, tende pia husaidia kuhakikisha mwili haishiwi na maji.
Ina madini ya potassium, ambayo huhifadhi maji mwilini.
Bashir anasema, "Watu wengi hufungua kwa kula tende na maji pamoja, na hii ni vizuri kwa kuongeza nguvu na maji mwilini"
Kula kupita kiasi
Watu wengi hupungua kimwili msimu wa Ramadhan, ila kufunga kunaweza kusababisha mtu kunona iwapo atakula chakula kingi wakati wa kufungua,Iftar.
Kiasilia, waislamu hula idadi witiri ya tende, kisha kuomba maombi ya Maghrib, kabla ya kula chakula cha Iftar.
Mwili unapoanza kumengenya 'fiber' iliyoko kwenye tende, hamu ya kula chakula kingi hupungua.
Bashir anasema, "hii huipa mwili wako nafasi ya kujua kuwa umekula na mchakato wa kumengenya chakula hicho umeanza."
mmeng'enyo wa chakula.
Hali kufungana choo na kufura kwa tumbo ni changamoto ambazo mtu hushuhudia anapofunga, kwa sababu kula na kunywa kila siku huchochea mtu kuenda haja kubwa, na hii huenda isishuhudiwe mara kwa mara wakati wa mfungo mrefu.
Tende zina fiber nyingi ambazo husaidia katika mmeng'enyo kwa chakula na kuenda haja kubwa.
Idara ya afya ya Uingereza inapendekeza kula gramu 30 ya fiber kila siku.
Bashir anasema "wakati mwingine wakati wa Ramadhan, mwili hutaka kabohaidreti, ila tukipanga milo yetu mapema, tunaweza hakikisha kuna fiber ya kutosha katika vyakula vyetu."
Njugu na vyakula vya mbegu pia vinaweza kuongezwa kwa chakula kinacholiwa.
Iwapo hupendi tende
Kando na Ramadhan, kufunga kwa kipindi fulani kwa manufaa ya afya, si jambo geni tena.
Bashir anasema, "nikama tu kufunga Ramadhan"
Na iwapo hupendi tende, kuna matunda mengine ambayo unaweza kutumia.
Ila pia unaweza kusaga tende na kuunda sharubati. Bashir anasema, "tende yaweza kuchanganywa na maziwa, njugu au mtindi na kuunda kinywaji kizuri chenye virutubishi vya kutosha."
Imetafsiriwa na Beldeen Waliaula