Je Putin anatafuta washirika wa Kiarabu ili kukwepa vikwazo vya magharibi?

Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Putin

Magazeti ya Uingereza yaliandika kuhusu ziara ya Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Tehran na athari zake za kimataifa hususan katika mzozo wa Syria, pamoja na operesheni za hivi karibuni za kijeshi za Israel dhidi ya Iran.

Mwanzo gazeti la Telegraph, ambalo liligusia katika ripoti ya ziara ya Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Tehran, ambayo ni safari yake ya pili ya nje tangu kuanza kwa uvamizi wa Ukraine Februari iliyopita.

"Rais wa Urusi, aliyetengwa kimataifa kwa ajili ya vita vyake vya bure dhidi ya Ukraine, anahitaji washirika ambao wanafurahia mzozo zaidi," gazeti hilo lilisema katika ripoti hiyo, iliyotiwa saini na Kon Coughlin, mhariri mkuu wa masuala ya ulinzi.

"Shambulio lisilo la msingi la Putin dhidi ya jirani ya kusini mwa Urusi limeitenga katika eneo la kimataifa, wakati uchumi wa Urusi umeumizwa na athari za vikwazo vikali vya Magharibi," Coughlin aliongeza.

Aliamini kwamba "kiwango cha kweli cha matatizo ya kifedha ya Moscow kilifichuliwa mwezi uliopita, wakati Urusi iliposhindwa kulipa deni lake la nje kwa mara ya kwanza tangu Mapinduzi ya Bolshevik."

"Kutengwa kwa Moscow kimataifa kulionekana katika uungwaji mkono mdogo uliovutia katika kura ya Umoja wa Mataifa mwezi Machi kulaani uvamizi wa Ukraine. Ni tawala nyingine nne tu za kimabavu zimejiunga na Urusi: Korea Kaskazini, Eritrea, Syria na Belarus," Coughlin aliongeza.

Alieleza, "Ndio maana Putin ana uhitaji mkubwa wa washirika wapya. Hapana shaka kuwa hili ndilo lengo kuu la ziara yake mjini Tehran."

Lakini lengo hasa la mkutano wa kilele wa Tehran ni kuchunguza iwapo inawezekana kwa vikosi hivyo vinavyoshindana kuweka tofauti zao kando na kuungana katika sababu ya pamoja ya kupinga shinikizo zataifa ya Magharibi.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Alitoa maoni kwamba, "mbali na kuendeleza kampeni ya kijeshi ya Urusi kunyakua maeneo makubwa ya ardhi ya Ukraine, lengo lingine kuu la Putin ni kupata uungwaji mkono kwa juhudi zake za kukwepa ushawishi wa vikwazo vya Magharibi."

"Kiongozi wa Urusi mara nyingi ameshutumu vikwazo kama tangazo la vita vya kiuchumi la Magharibi na anatafuta njia za kuepuka vikwazo hiyo , gazeti la Telegraph iliongezea.

Alikumbuka kwamba "Iran - ambayo ina uzoefu wa miaka mingi katika kukwepa vikwazo vya Magharibi - tayari imejitolea kusaidia Urusi kuuza mafuta yake kwenye masoko ya kimataifa kwa kutumia mfumo wa siri wa benki na kifedha ambao Tehran tayari imeweka ili kukwepa vikwazo vya Magharibi."

Hivi karibuni, kumekuwa na dalili za ushirikiano wa karibu wa kijeshi kati ya Tehran na Moscow, huku maafisa wa Marekani wakiripoti kwamba Iran imejitolea kuipatia Urusi mamia ya ndege zisizo na rubani kusaidia juhudi za vita nchini Ukraine.

Na aliamini kwamba "kwa kujibu, Iran itatafuta msaada wa Urusi kwa shughuli zake nchini Syria, ambapo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran linaimarisha uwepo wake wa kijeshi ili kutishia usalama wa Israeli."

"Kujaribu kuleta Uturuki upande wake itakuwa changamoto muhimu zaidi kwa kiongozi wa Urusi, sio kwa sababu Erdogan alichukua jukumu muhimu katika kusaidia vikosi vya Ukraine kupinga majaribio ya Urusi kuivamia nchi yao," alisema.

"Ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB2 iliyotengenezwa na Uturuki ilikuwa na athari mbaya kwenye uwanja wa vita, kwani mabomu yake ya leza yenye uzani mwepesi yaliathiri vibaya majeshi ya Urusi," aliongeza.

Je Syria itakuwa mzozo uliosahaulika?

Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika muktadha unaohusiana na hayo, Martin Chulov, mwandishi wa gazeti la The Guardian Mashariki ya Kati, aliandika makala ya uchambuzi kuhusu mustakabali wa mzozo wa Syria kwa kuzingatia mabadiliko ya sasa ya kimataifa.

Huku juhudi za kidiplomasia kuhusu Ukraine zikiendelea, Mzozo wa Syria upo katika hatari za kusahaulika .

"Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Urusi Vladimir Putin, na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, wamechukua majukumu ya kuongoza katika masaibu ya Syria kwa zaidi ya muongo mmoja, na walikuwa wameazimia kuvuna manufaa ya machafuko yaliyosalia," alisema.

"Wakati Urusi inasonga mbele, ikianzisha eneo lisiloweza kuruka kwa ndege na kuwazuia waasi kaskazini, Iran ilikuwa ikijishughulisha na kuimarisha uwepo wake katika nchi ambayo imekuwa mshirika wa kimkakati kwa muda mrefu, na wakati huo imekuwa fursa nzuri kwa nchi yake dhidi ya Israel,” aliongeza.

"Kwa muda wa muongo mmoja uliopita, Iran imetumia washirika wake kupambana na makundi ya upinzani na wanajihadi, huku ikipata ushawishi katika wizara muhimu na kufikia nchi nzima," alisema.

"Tehran na Moscow zilikuwa na malengo sawa mwanzoni mwa mapigano - kuzuia Damascus isianguke. Hata hivyo, wana miundo tofauti sana kuhusu ni aina gani ya nchi inapaswa kutoka kwenye vifusi," Chulov aliongeza.

Kuhusiana na msimamo wa Uturuki, aliongeza, "Vitisho vikali vya Erdogan vya kutaka kuivamia Syria kwa mara ya pili, ili kuwaepusha na kundi la PKK na washirika wake kwenye mpaka, vilikabiliwa na karipio kali kutoka kwa Khamenei kabla ya kuanza kwa mkutano wa kilele wa Jumanne."

"Tehran ilishikilia msimamo wake kwamba Assad ndiye mpatanishi pekee halali wa Syria na kudai kwamba mazungumzo juu ya kaskazini mashariki inayoongozwa na Wakurdi yanapaswa kujumuisha Damascus," alisema.

Wiki iliyopita, Urusi ilipiga kura ya turufu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupunguza muda wa usambazaji wa misaada kutoka Uturuki hadi maeneo ya upinzani kutoka mwaka mmoja hadi miezi sita.

"Kura hiyo ilitokana na shinikizo kubwa la kukomesha kabisa uwasilishaji wa misaada - hatua ambayo mashirika ya misaada yanahofia kuwa haiwezi kuepukika huku Syria ikiimarika kama sehemu ya migogoro ya kudumu, wakati juhudi ngumu za kidiplomasia za kimataifa zinaendelea kushirikiana na Ukraine," alisema.

"Kama ilivyokuwa kwa miaka mitano iliyopita angalau, kuna mazungumzo ya mustakabali wa Syria bila uwepo wa Assad, ambaye mara kwa mara anamkumbusha Putin kwamba anabaki tu katika ikulu yake ya rais kwa sababu ya uungwaji mkono wake," aliongeza.

"Kinachoingoja Syria sasa bado ni swali la kutatanisha kama ilivyokuwa siku zote," alisema. "Kabla ya mkutano huo, Erdogan aliwasilisha utayari wake wa kuzuia Finland na Sweden kujiunga na NATO ikiwa hatapata alichotaka nchini Syria. Iran pia haina nia ya kudhoofisha uwepo wake katika nchi ambayo ina ufunguo wa kushindwa." sera yake ya mambo ya nje.

Alihitimisha, "Wengi wanaweza kuisahau Syria, lakini inasalia kuwa kichochezi chenye nguvu cha matukio ya kimataifa."

Kutoaminika kwa Iran

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Na hitimisho la Financial Times, ambalo lilichapisha ripoti ya mwandishi wake huko Tehran, Najma Bozorgmehr, yenye kichwa "Mashambulizi ya Israeli yanachochea kutoaminiana na hofu nchini Iran."

"Kuuawa kwa kamanda wa kijeshi huko Tehran kumeongeza hofu ya uwezekano wa vita vya kivuli," alisema.

Katika onyesho la mshikamano wa watu wengi, mwezi huu waziri wa ujasusi wa Iran na mkuu wa kijasusi wa Walinzi wa Mapinduzi walipiga picha, na kuahidi kufanya kazi pamoja ili kuimarisha usalama - ikimaanisha kupambana na operesheni za Israel katika Dola ya Kiislamu.

"Uamuzi wa kupunguza ushindani kati yao unazungumzia wasiwasi katika ngazi za juu za uanzishwaji wa Iran na katika mitaa ya Iran kuhusu kuongezeka kwa mashambulizi yaliyohusishwa na Israeli, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kamanda wake mwezi Mei mlangoni mwake katikati mwa Tehran. ," aliongeza.

Alisema kuwa "kiwango cha kujipenyeza kwa Israel nchini Iran kimekuwa wazi, kama wachambuzi wanasema."

"Kujipenyeza ni suala zito sana, ambalo serikali inahitaji kulifutia suluhu," mchambuzi mmoja wa kihafidhina alinukuliwa akisema.

Bozorgmehr alibainisha kuwa "pia kulikuwa na ripoti za mashambulizi ya mtandao ya Iran nchini Israel."

Ilisema "inashukiwa kuwa shambulio la mtandaoni la Iran lilikuwa nyuma ya arifa za uongo za king'ora huko Jerusalem Magharibi na Eilat mwezi uliopita, kulingana na vyombo vya habari vya Israel."

Aliongeza kuwa "Wairani walivamia tovuti nyingi maarufu za Israeli za kuhifadhi, na waliweza kupata habari za kibinafsi za Waisraeli zaidi ya 300,000, kulingana na ripoti za Israeli."

"Maafisa wa Irani wanaonya kwamba hawatajaribu kuzidisha tena mvutano na Israel," alisema.

Imemnukuu mdau wa ndani wa utawala wa Iran akisema, "Sera ya Iran inabakia kufanya kazi na vikosi vyake vya wakala na hatutaanzisha mashambulizi yoyote dhidi ya Israel ikiwa Israel haitashambulia Lebanon [Hezbollah ndio wakala mkuu wa Iran]."

"Sio busara kwetu kupigana na Israel. Wazayuni pia wanaonyesha meno kushambulia, lakini meno yao hayana makali ya kutosha kufikia kuipiga Iran," aliongeza.

Mwezi uliopita, Mohammad Ali Jafari, kamanda wa zamani wa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, alitaja "operesheni za kisaikolojia" za adui ambazo zinajenga dhana kwamba Israel ilihusika katika mashambulizi ambayo "hawakufanya." "Hii ina maana kwamba Marekani inaweza kuwa nyuma ya mashambulizi haya," mwandishi anatoa maoni.

Imewanukuu wachambuzi wakisema, "Pamoja na kutengeneza makombora, ndege zisizo na rubani na boti za mwendo kasi, Iran inahitaji kujiandaa kwa ajili ya masuala haya ya kisaikolojia na kiintelijensia.