Tetesi za soka Ulaya Jumapili 19.05.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 24, na huenda wakamtumia fowadi wa Colombia Jhon Duran, 20, kama sehemu ya mkataba huo. (Telegraph – Subscription required)
Mshambulizi wa Brentford na England Ivan Toney, 28, anasakwa na Tottenham kama mmoja wa washambuliaji wawili wanaotarajiwa kusajiliwa msimu huu. (Football Insider)
Bosi wa Ipswich Kieran McKenna ndiye mgombea anayeongoza kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino katika klabu ya Chelsea, ambaye hatma yake kama meneja haijaamuliwa. (Guardian)
Kocha wa Brighton anayeondoka Roberto de Zerbi ndiye anayelengwa na Bayern Munich kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel kama meneja. (Bild)

Chanzo cha picha, PA Media
Bayern na Muitaliano De Zerbi tayari wameamua kuwa hawatafanya kazi pamoja, kwa mujibu wa mkurugenzi wa klabu hiyo Max Eberl. (Fabrizio Romano)
Newcastle, Everton na Crystal Palace wana nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Uingereza Kasey McAteer, 22, ambaye anatazamiwa kuingia mwaka wa mwisho wa kandarasi yake na Leicester City. (Football Insider)
Everton wanajiandaa kukabiliana na ofa za ufunguzi kwa mlinzi wa kati Jarrad Branthwaite, 21, huku Manchester United, Manchester City na Tottenham zote zikiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo wa England. (Mail)
Manchester United wanataka kumuuza mshambuliaji Muingereza Mason Greenwood, 22, ambaye amekuwa akihusishwa na Napoli, Juventus na Atletico Madrid baada ya kucheza kwa mkopo Getafe. (Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Napoli ya Italia imefanya mawasiliano na Manchester United juu ya kutaka kumnunua Greenwood. (Subscription Required)
Borussia Dortmund pia wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya Greenwood. (Mirror)
Kocha anayetarajiwa Liverpool Arne Slot ametanguliza saini ya beki wa Ureno Antonio Silva, 20, kutoka Benfica. (Give me Sport)
RB Leipzig wameweka kipengele chao cha kuachiliwa kwa mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, 20, ambaye anahusishwa na Arsenal, kwa £55.6m. (Sky Sports Germany)
Kocha wa Barcelona Xavi anasema bado anaungwa mkono na klabu hiyo licha ya ripoti kueleza kuwa huenda akafutwa kazi. (Saa – Subscription Required)












