Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Man Utd wanafikiria uhamisho wa Rashford na Watkins

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United ina mpango wa kubadilishana wachezaji utakaomhusisha Marcus Rashford na mshambuliaji wa Aston Villa Ollie Watkins, Alexander Isak kusalia Newcastle United na Manchester City inapanga kumnunua mlinda lango Diogo Costa.

Manchester United wanafikiria mpango wa kubadilishana wachezaji ambao utamhusisha mshambuliaji Marcus Rashford, 27, wa kubadilisha uhamisho wa mkopo wa Aston Villa kuwa wa kudumu huku mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Uingereza Ollie Watkins, 29, akijiunga na Man Utd wakati wa uhamishaji wa majira ya kiangazi. (Star)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kipa wa Cameroon Andre Onana, 29, ataruhusiwa kuondoka Manchester United ikiwa klabu hiyo itapokea ofa ya zaidi ya £20m. (Mirror)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone anamfuatilia kwa karibu beki mwenzake wa kati wa Argentina na Tottenham Cristian Romero na huenda akajaribu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kabla ya Kombe la Dunia la Vilabu msimu huu wa joto. (Sunday Express)

.

Chanzo cha picha, Rex Features

Winga wa Uhispania Nico Williams, 22, amehusishwa na uhamisho wa Arsenal na Barcelona lakini amependekeza kuwa anataka kusalia na Athletic Bilbao na kuichezea katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao ikiwa watafuzu. (AS - in Spanish)

Klabu kadhaa zinavitiwa na Viktor Gyokeres wa Sporting lakini mshambuliaji huyo wa Uswidi mwenye umri wa miaka 26 anasema "hakuna anayeweza kutabiri kitakachotokea - tunafurahia wakati uliopo". (Metro)

.

Chanzo cha picha, Reuters

Real Madrid inapanga kuachana na kocha Carlo Ancelotti na tayari klabu hiyo imewasiliana na kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso, ingawa hatua ya kumtimua Mhispania huyo anaweza kuwagharimu takriban pauni milioni 15 kama malipo yake. (Sky Sports Germany)

Iwapo Ancelotti ataondoka Real Madrid angependelea kuchukua nafasi ya kocha wa timu ya taifa ya Brazil. (Athletic - subscription required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, ambaye anahusishwa na Arsenal na Liverpool, anatarajiwa kusalia Newcastle United huku Magpies wakipanga kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 katika uhamisho wa majira ya msimu wa joto. (Football Insider)

Chelsea, Newcastle na Juventus wanavutiwa na beki wa kati wa Korea Kusini Kim Min-jae, huku Bayern Munich wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports Germany)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City wanapanga kumnunua mlinda mlango wa Porto Diogo Costa na wanaamini kwamba ofa ya pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno inaweza kutosha, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuwa na kipengele cha kumnunua cha pauni milioni 63 katika mkataba wake. (Mirror)

Bayern Munich wanamfuatilia kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Andrey Santos, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Strasbourg ya Ufaransa. (Mail)

Imetafsiriwa na Asha Juma na kuhaririwa na Ambia Hirsi