Nani kushinda Ligi ya Mabingwa msimu huu-Utabiri wa BBC

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal, Inter Milan, Barcelona na Paris St-Germain wamejikatia tiketi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Hizo ndizo timu nne za mwisho zilizosalia.
Ni wakati wa kuangalia nani anaweza kubeba kombe hilo huko Munich, Ujerumani mwezi ujao. Waandishi wa habari wa BBC Sport na wachambuzi wanatupa maoni yao - huku Paris St-Germain ikipewa nafasi kubwa ya kushinda.
Paris St-Germain
Mtaalamu wa soka wa Uhispania Guillem Balague, anasema, wana kila kitu. Umiliki, muundo, ushambuliaji, ubora, kila mchezaji ana fikra lakini wanacheza kama timu, wote wanafikiri kwa njia moja.
Njia pekee ya kuwashinda ni ikiwa watalazimika kulinda sana kwenye eneo lao. Barcelona wanaweza kuwalazimisha kujilinda. Ikiwa fainali itakuwa kati ya timu hizo mbili.
Mwandishi wa soka Phil McNulty, anasema, licha ya ushahidi wa Arsenal katika mechi mbili dhidi ya mabingwa Real Madrid, itakuwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa yenye kusisimua kati ya PSG na Arsenal - lakini ninakwenda na timu bora ambayo nimeona kwenye mashindano ya msimu huu.
PSG walicheza dhidi ya Aston Villa katika mechi ya mkondo wa pili, na wana timu imara - na mashambulizi ya kiwango cha kimataifa kutoka kwa Ousmane Dembele, Khvicha Kvaratskhelia na kijana mahiri Desire Doue au Bradley Barcola.
Beki wa zamani wa Arsenal na mchambuzi Matt Upson, anasema ni rahisi kubadili maoni mara tu unapoingia kwenye mkondo mwingine wa mechi lakini nitabaki na hisia zangu za PSG kushinda shindano hilo.
Nadhani wanacheza vizuri muda wote. Walikuwa na wakati mgumu sana huko Aston Villa na walinusurika. Uimara wao sijauona katika timu nyingine yoyote ya PSG.
Mwanahabari wa soka Sami Mokbel, anasema, Luis Enrique ameunda timu isiyo na majina makubwa sana, lakini ina nguvu. Lionel Messi, Neymar na Kylian Mbappe wameondoka - lakini timu hii mpya ya PSG inawakilisha ushindi, umoja na muundo.
Waliifanya Liverpool ionekane kama timu ndoga katika mechi mbili katika hatua ya 16 bora - hilo si jambo dogo. Tarajia Parisians kunyanyua kombe la Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza.
Arsenal
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mwandishi wa habari wa soka Alex Howell, anasema Arsenal kikosi cha Mikel Arteta kimekabiliwa na misukosuko mingi msimu huu, lakini kimepata mafanikio katika Ligi ya Mabingwa.
Katika safu ya ulinzi, wanafanya vizuri, na Bukayo Saka ni mshambuliaji hatari, The Gunners wana ubora wa kuifunga timu yoyote iliyosalia kwenye mashindano.
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal na mchambuzi Theo Walcott, anasema, nataka Arsenal washinde na bila shaka wana uwezo wa kufika mbali, baada ya kwenda Bernabeu na kuifunga Real Madrid.
Lakini kuna kitu kuhusu Inter Milan ambacho kinanitia wasiwasi. Jinsi wanavyojilinda, inanifanya nifikirie kwamba nafasi ya kushinda pia. Hata kabla ya kufika fainali, hapa nusu fainali tu - ni ngumu kusema ni nani atashinda kwa uhakika.
Beki wa zamani wa Manchester City na mchambuzi Nedum Onuoha, anasema mshinda atakuwa Arsenal au PSG, yeyote atakayepita katika nusu fainali hapo. Ni ngumu sana kuchagua kati ya hizo mbili lakini nitachagua Arsenal.
Kuishinda Real Madrid, hata kama hii sio toleo bora la Real Madrid ni jambo moja, lakini kwenda Bernabeu na mazungumzo yote kuwa watafungwa, inaonyesha wako vizuri.
Kwa ujumla, kwa jinsi walivyojiandaa na kushambulia, na bado tishio katika ushambuliaji, naweza kusema kuwa wao ndio timu kamili iliyosalia kwenye mashindano.
Barcelona
Mwandishi wa michezo Simon Stone, niliamini tangu mwanzoni mwa shindano hili kuwa watachukua ushindi - kwa sababu nilitaka timu tofauti ishinde - na sitabadili utabiri wangu sasa.
Wanaweza kujilinda vizuri, wabunifu katika safu ya kiungo na wana washambuliaji wazuri. Hawajashinda taji hilo tangu wakati wa Lionel Messi. Watashinda msimu huu.
Inter Milan
Mwandishi mwandamizi wa soka wa BBC, Ian Dennis, anasema, najua Arsenal imevutia sana dhidi ya Real Madrid, lakini timu ambayo inaonekana imeingia kwenye rada za kutinga nusu fainali kwangu ni Inter Milan.
Mabingwa hao wa Italia wana rekodi bora zaidi ya ulinzi kwenye shindano hilo, hakuna aliye linda lango vizuri zaidi kuliko kipa wao Yann Sommer.
Wako vizuri na ni tishio. Ni mara ya pili katika misimu mitatu Inter kufika nusu fainali na nadhani wanaweza kuleta upinzani mkali kwa Barcelona.















