Je, uchaguzi wa Marekani unaweza kubadilisha ulinzi ambao Marekani inautoa Ulaya?

g
Muda wa kusoma: Dakika 4

Meli za kivita za Marekani Marekani zinazobeba kundi kubwa za ndege za kivita ni silaha nyingi ni ishara yenye nguvu ya nguvu za kijeshi za Marekani na ishara kwamba iko tayari kutetea washirika na kuzuia maadui.

Kwahivyo uwepo wa nguvu kama hiyo katika Bahari ya Kaskazini katika wiki chache zilizopita ina maana ya kuwahakikishia washirika wa Ulaya, licha ya kutokuwa na uhakika wa kisiasa nyumbani.

Nguvu za kijeshi za Marekani zimesaidia kuilinda Ulaya kwa miaka 75 iliyopita - lakini uchaguzi wa rais wa Marekani unazua swali: je,kwa muda gani?

Makamanda wa kijeshi hufanya kila wawezalo kuepukana na siasa.

Lakini miongoni mwa kundi la waandishi wa habari walioalikwa kwenye meli ya USS Harry S Truman, kinyang'anyiro cha urais wa Marekani kilikuwa ajenda kuu . Swali lilikuwa: Je, Marekani bado itakuwa na uungaji mkono wa Ulaya?

Rear Adm Sean Bailey alisema: "Ninachoweza kukuambia ni kwamba tumejitolea kwa dhati kwa muungano wetu, tumejitolea kwa dhati kwa Nato."

g

Chanzo cha picha, Reuters

Lakini sio yeye ambaye atakuwa anaamua sera ya kigeni ya Marekani, na wala jibu lake haliwezi kupunguza mashaka.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, anajua mabadiliko yapo hewani.

Alipoulizwa kuhusu athari zinazowezekana za uchaguzi wa Marekani barani Ulaya wiki jana, alisema ni swali la iwapo Marekani inafanya "kidogo sana, au kidogo kidogo".

Hakutaja majina, lakini ni Donald Trump ambaye kuna uwezekano wa kufanya kidogo sana.

USS Harry S Truman anajivunia jina la rais ambaye alisaidia kuanzisha Nato miaka 75 iliyopita.

Lakini muhula wa pili wa Trump unaweza tena kutikisa muungano hadi msingi wake.

Mafundisho ya Truman ya kutoa msaada wa kijeshi, kiuchumi na kisiasa kwa mataifa ya kidemokrasia yaliyo chini ya tishio ni tofauti sana na sera ya Trump ya Amerika Kwanza.

Hivi majuzi alisema Urusi inaweza "kufanya chochote kile wanachotaka" kwa washirika ambao hawana matumizi ya kutosha katika ulinzi.

h

Chanzo cha picha, MOD

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kujiondoa kokote kwa Marekani kutoka Ulaya utaacha shimo kubwa.

USS Harry S Truman ni uthibitisho wa kile ambacho marekani huleta kwa ukubwa na idadi - ikiwa na wafanyakazi 5,000 na zaidi ya ndege 60.

Meli ya Kifalme ya Uingereza , HMS Prince of Wales, inayosafiri karibu na hapo, lilitoa ukumbusho wa ulinzi wa kawaida zaidi ya ule unaotolewa na Ulaya.

Meli hiyo ya Uingereza ilikuwa ikisafirisha mbawa chache za helikopta na jeti nane za F-35 - kielelezo cha nguvu za kijeshi za Marekani.

Kwa ujumla Marekani ina wanajeshi zaidi ya 100,000 waliotumwa Ulaya.

Mara ya mwisho alipokuwa rais, Trump alitishia kuondoa baadhi ya vikosi hivyo. Akichaguliwa anaweza kufanya vivyo hivyo tena.

Warepublican wengi wanaamini Ulaya inapaswa kujitegemea yenyewe. Hayo ni maoni ya Elbridge Colby, afisa mkuu wa Pentagon katika utawala uliopita wa Trump.

Anasema Marekani inapaswa "kuondoa" vikosi vyake Ulaya ili kukabiliana zaidi na tisho kutoka China.

Uchaguzi huo pia utakuwa na athari kwa msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine - Marekani ndiyo mfadhili wake mkuu zaidi wa kijeshi.

Lakini afisa mkuu wa Nato, ambaye hakutaka jina lake litajwe, hivi majuzi aliiambia BBC "bila kujali ni nani atashinda sehemu ya mchango wa Marekani kwa Ukraine labda itapungua kwa masharti".

Ulaya, ilisema, haiwezi kutarajia Marekani kuendelea kutoa mchango"mkubwa zaidi".

Ukweli ni kwamba mwelekeo wa kijeshi wa Marekani tayari umekuwa ukihamia mashariki hadi eneo la India-Pacific na kuongezeka dhidi ya Uchina.

Pentagon inaitambua China kama changamoto kubwa zaidi ya usalama. Uchina sasa ina jeshi kubwa la wanamaji kuliko Marekani. Inaunda kundi la ukubwa wa Jeshi la Wanamaji la Uingereza kila baada ya miaka miwili.

Mabaharia na marubani walio kwenye meli hiyo wanatambua kuwa kuna sehemu ya mashariki pia.

Cdr Bernie Lutz amefanya kazi kwa muda mrefu wa taaluma yake ya majini kusafirisha ndege aina ya F-18 kutoka kwa meli ya Marekani katika Pasifiki na Mashariki ya Kati.

Anatambua kwa nini sasa wanasafiri katika maji ya Ulaya. "Kuna mengi yanaendelea," anasema.

Lakini anaongeza kuwa, "Nadhani ukumbi wa vita wa Pasifiki ndio lengo kubwa zaidi la muda mrefu".

Kama wafanyakazi wengine 5,000 wa shehena hiyo, bado hajaambiwa watakuwa wapi tena - lakini imeripotiwa sana kwamba USS Harry S Truman hivi karibuni itakuwa njiani kuelekea Mashariki ya Kati.

Eneo hilo, pia, litabaki kuwa changamoto kwa yeyote atakayekuwa rais.

Kapteni Dave Snowden anasema ana furaha kubeba bendera ya kupunguza kasi au kuzuia au hata kusafiri kwa njia ya hatari - popote anapotumwa.

Lakini kukosekana kwa mjadala mzito wa sera za kigeni katika uchaguzi huo kunaonyesha kusitasita kujihusisha moja kwa moja katika vita zaidi.

Marekani bado itasalia kuwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi ya kijeshi duniani.

Swali ni je rais ajaye ataitumiaje?.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi