Je, uchaguzi wa Marekani unaweza kubadilisha dunia kwa jinsi gani?

h

Chanzo cha picha, Reuters

    • Author, Na Liz Doucet
    • Nafasi, Mwandishi mkuu wa habari za Kimataifa - BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 8

Wakati Rais wa Marekani Joe Biden alipoitembea Kyiv mnamo Februari 2023 katika ziara ya kushtukiza kuonyesha mshikamano na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, za ving’ora zilikuwa zinasikika . "Nilihisi kitu chenye nguvu zaidi ambayo sijawahi kuwa nayo," baadaye nilikumbuka. "Marekani ni nguzo ya ulimwengu."

Sasa dunia inasubiri kuona nani ataongoza "nguzo" hii baada ya Wamarekani kufanya uchaguzi wao katika uchaguzi wa rais wiki ijayo. Je, itakuwa Kamala Harris, kwa imani yake kwamba "Marekani haiwezi kumudu kurudi nyuma katika nyakati hizi za misukosuko," kuendelea kuongoza kwa Biden? Au itakuwa Donald Trump, na matumaini yake kwamba "Umarekani, sio utandawazi" utakaoongoza?

Tunaishi katika ulimwengu ambao thamani ya ushawishi wa Marekani ulimwenguni unatiliwa shaka.

Mataifa yenye nguvu ya kikanda yanakwenda kwa njia yao wenyewe, tawala za kiimla zinaunda ushirikiano wao wenyewe, na vita vya kutisha huko Gaza, Ukraine, na kwingineko vinaibua maswali yasiyo na wasiwasi juu ya thamani ya jukumu la Washington.

Lakini Marekani ni muhimu kwa sababu ya nguvu zake za kiuchumi na kijeshi, na jukumu lake kuu katika ushirikiano mwingi. Nilizungumza na waangalizi wenye ufahamu mzuri na wanaotazamwa kwa karibu kwa mawazo na tafakari zao kuhusu athari za ulimwengu za uchaguzi huu muhimu.

Unaweza pia kusoma:

Nguvu ya kijeshi

Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa NATO, Rose Gottemoeller, alisema: "Siwezi kupunguza maonyo haya ya Donald Trump ni jinamizi kwa Ulaya, haswa kutokana na tishio lake la kujiondoa kutoka kwa NATO linalosikika kama mwangwi masikioni mwa kila mtu."

Matumizi ya ulinzi ya Washington ni sawa na theluthi mbili ya bajeti ya kijeshi ya nchi 31 wanachama wa NATO. Nje ya NATO, Marekani hutumia zaidi jeshi lake kuliko mataifa 10 makubwa zaidi kwa pamoja, ikiwa ni pamoja na China na Urusi.

Trump anajivunia kuwa ana jukumu kubwa katika kuzilazimisha nchi nyingine za NATO kufikia malengo yao ya matumizi ya kijeshi ya asilimia 2 ya pato la taifa - ni nchi 23 tu wanachama ambazo zimefikia lengo hilo kufikia mwaka 2024. Lakini kauli zake za uongo bado zinatia wasiwasi.

Ikiwa Kamala Harris atashinda, Bi Gottemoeller anaamini, "NATO bila shaka itakuwa katika mikono mizuri huko Washington." Wakati huo huo, pia anaonya kwamba Kamala "atakuwa tayari kuendelea kufanya kazi na NATO na EU ili kupata ushindi nchini Ukraine, lakini hataacha kuishinikiza Ulaya kuhusu matumizi ya kijeshi."

g

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Harris aliahidi kuwa mshirika mkubwa wa Ukraine.

Lakini timu ya Kamala ya White House italazimika kushindana na Seneti au Baraza la wawakilishi ambalo hivi karibuni linaweza kuwa mikononi mwa Republican na halitakuwa na mwelekeo wa kuunga mkono vita vya kigeni kuliko wenzao wa Democratic.

Kuna hisia inayoongezeka kwamba yeyote atakayekuwa rais, shinikizo litaongezeka mjini Kiev kutafuta njia za kuondokana na vita hivi wakati wabunge wa Marekani wakizidi kuhangaika kupitisha vifurushi vikubwa vya misaada.

‘‘Mtafutaji amani’’

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Rais mpya wa Marekani atalazimika kufanya kazi katika ulimwengu unaokabiliwa na mapambano makubwa zaidi tangu zama za Vita Baridi, kati ya mataifa makubwa.

"Marekani bado ni mhusika muhimu zaidi wa kimataifa katika masuala ya amani na usalama," anasema Comfort Ero, rais na mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utatuzi wa migogoro ya kimataifa , International Crisis Group. "Lakini uwezo wake wa kusaidia kutatua migogoro umepungua," anaonya.

Vita vinaendelea kuwa vigumu zaidi kumalizika. "Mgogoro wa muda mrefu unazidi kuwa mgumu, huku ushindani mkubwa wa nguvu ukiongezeka na nguvu za kati zikiongezeka," Bi Ero anaelezea mazingira. Vita kama vile vya Ukraine huhusisha nguvu nyingi, na migogoro kama Sudan inawapa wahusika wa kikanda maslahi ya kushindana dhidi ya kila mmoja, wengine zaidi wamewekeza katika vita kuliko amani.

Marekani inapoteza msingi wake wa maadili, Bi Comfort anasema. "Wahusika wa vita wa kimataifa wanatambua kwamba inahusika kwa kiwango kimoja kwa vitendo vya Urusi nchini Ukraine na kwa vitendo vya Israeli huko Gaza," anasema. "Vita nchini Sudan vimekuwa na ukatili wa kutisha lakini vinachukuliwa kama suala la daraja la pili."

Ushindi wa Harris , anasema, "atamaanisha mwendelezo na utawala wa sasa," wakati ikiwa Trump atashinda, anaweza "kuipa Israeli uhuru mkubwa zaidi huko Gaza na kwingineko, na amedokeza kwamba anaweza kujaribu kupunguza makubaliano na Moscow juu ya Ukraine kwa gharama ya Kiev."

Kuhusu Mashariki ya Kati, mgombea huyo wa chama cha Democratic alirudia mara kwa mara kuunga mkono vikali hatua ya Biden ya "haki ya Israel kujilinda," lakini pia alisisitiza kuwa "mauaji ya Wapalestina wasio na hatia lazima yakome."

Trump pia alitangaza kwamba ni wakati wa "kurejea kwenye amani na kuacha kuua watu," lakini aliripotiwa kumwambia kiongozi wa Israeli Benjamin Netanyahu: "Fanya kile unachotakiwa kufanya."

g

Chanzo cha picha, Reuters

Mgombea wa Republican anajivunia kuwa yeye ni "mtafutaji amani." Aliahidi katika mahojiano na Al Arabiya Jumapili jioni: "Nitafikia amani katika Mashariki ya Kati hivi karibuni."

Ameahidi kupanua mkataba wa mwaka 2020 unaofahamika kama Abraham Accords, ambao ulirejesha uhusiano kati ya Israel na mataifa kadhaa ya Kiarabu lakini unaonekana kuwa umewatenga Wapalestina na kuchangia katika mgogoro wa sasa ambao haujawahi kutokea.

Kuhusu Ukraine, Trump hajawahi kuficha sifa zake kwa "watu wenye nguvu" kama kiongozi wa Urusi Vladimir Putin. Mgombea huyo wa Republican ameweka wazi kwamba anataka kumaliza vita nchini Ukraine, na kwa msaada mkubwa wa kijeshi na kifedha wa Marekani. "Ninaondoka," alisisitiza katika mkutano wa hivi karibuni. "Tunapaswa kuondoka katika vita hivi."

Kwa upande wake, Bi Harris alisema: "Nimekuwa na fahari kusimama na Ukraine. Nitaendelea kushirikiana na Ukraine. Na nitajitahidi kuhakikisha kuwa Ukraine inashinda vita hivi."

Lakini Comfort Ero, rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kikundi International Crisis Group ana wasiwasi kwamba bila kujali nani anachaguliwa, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi duniani.

Mahusiano ya kibiashara na Beijing

Kwa mtazamo wa msomi wa China Profesa Rana Mitter, pendekezo la Trump la ushuru wa asilimia 60 kwa bidhaa zote za China zinazoingizwa nchini humo ni "mshtuko mkubwa kwa uchumi wa dunia katika miongo kadhaa."

Kuonesha gharama kubwa kwa China na washirika wengine wengi wa kibiashara imekuwa moja ya vitisho vya Trump vinavyoendelea kama sehemu ya mbinu yake ya "Marekani Kwanza".

Lakini Trump pia anachukulia kile anachokiona kama uhusiano wake wa kibinafsi na Rais Xi Jinping. Aliiambia bodi ya wahariri ya Wall Street Journal kwamba hatalazimika kutumia nguvu za kijeshi ikiwa Beijing itaamua kuizuia Taiwan kwasababu kiongozi huyo wa China "ananiheshimu na anajua nina wazimu."

Lakini viongozi wote wa Republican na Democrats ni wachuuzi, na wote wanaiona Beijing kuwa na nia ya kujaribu kuipiku Marekani kama taifa lenye nguvu zaidi duniani.

Lakini mwanahistoria wa Uingereza anayesomea uhusiano wa Marekani na Asian katika shule ya Kennedy ya Harvard, Profesa Mitter, anaona tofauti kadhaa. Pamoja na Bi Harris, anasema, "uhusiano huo unaweza kubadilika kwa kiwango sawa na ilivyo sasa." Ikiwa Trump atashinda, itakuwa "hali mbaya zaidi."

Bwana Mitter anaangazia viwango viwili vya Trump kuhusu iwapo atatetea kisiwa kilicho mbali na Marekani - Taiwan.

Viongozi wa China wanaamini kuwa Harris na Trump watakuwa na msimamo mkali. "Kikundi kidogo cha watu wanaoanza biashara kinampendelea Harris, kwa kuzingatia msemo wa zamani 'Ni bora adui unayemjua kuliko rafiki usiyemjua,'" anasema Profesa Mitter.

Watu wachache wanamuona Trump kama mtu asiyetabirika ambaye anaweza kufanya biashara kubwa na China, hata hivyo hakuna uwezekano wa hilo kuonekana.

Mgogoro wa hali ya hewa

"Uchaguzi wa Marekani una madhara makubwa sio tu kwa raia wake bali kwa dunia nzima kwa sababu ya dharura ya mgogoro wa hali ya hewa na mazingira," anasema Mary Robinson, rais wa zamani wa Ireland na kamishna mkuu wa zamani wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, ambaye sasa ni mwenyekiti wa The Elders, kundi la viongozi wa dunia lililoanzishwa na Nelson Mandela.

h

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Onyo la joto kali katika Death Valley, California, USA

Lakini wakati kimbunga Milton na Helene vikiendelea, Trump alidharau mipango na sera za mazingira kushughulikia dharura ya hali ya hewa kama "moja ya kashfa kubwa zaidi kuwahi kutokea." Wengi wanatarajia Trump kujiondoa katika mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi wa mwaka 2015, kama alivyofanya katika muhula wake wa kwanza.

Hata hivyo, Robinson anaamini kuwa Trump hawezi kuzuia kasi ambayo hali ya hewa ya sasaya Marekani: "Hawezi kuzuia mabadiliko ya nishati nchini Marekani na kuondoa mabilioni ya dola katika ruzuku ya kijani."

Harris, ambaye bado hajatoa msimamo wake juu ya hali ya hewa, alihimiza kila mtu kuongeza juhudi za "kuongoza katika kulinda mazingira ."

Uongozi katika masuala ya kibinadamu

"Matokeo ya uchaguzi wa Marekani ni muhimu sana, kutokana na ushawishi usio wa kawaida ambao Marekani inautumia, sio tu kupitia nguvu zake za kijeshi na kiuchumi, bali kupitia uwezo wake wa kuongoza kwa mamlaka ya kimaadili katika jukwaa la dunia," anasema Martin Griffiths, mpatanishi mkongwe wa migogoro ambaye hadi hivi karibuni alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya dharura.

Griffith anaona mwanga mkubwa wa matumaini ikiwa Harris atashinda. Kwa upande mwingine, anasema, "kurejea kwa urais wa Trump, wa upande mmoja kunazidisha tu ukosefu wa utulivu duniani na kukata tamaa."

g

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Bango mjini Tehran linamuonyesha rais wa Iran na mkuu wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi akikabiliana na Biden na Netanyahu.

Marekani pia ni mfadhili mkubwa zaidi linapokuja suala la mfumo wa Umoja wa Mataifa, ikitoa rekodi ya dola bilioni 18.1 mnamo 2022.

Lakini katika muhula wa kwanza wa Trump, alisitisha ufadhili kwa mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa na kujiondoa katika Shirika la Afya Duniani. Wafadhili wengine walikimbilia kujaza mapengo - kitu ambacho Trump alitaka kuona kikitokea.

Lakini Bwana Griffiths anaangazia kuongezeka kwa kukata tamaa katika jamii ya kibinadamu hata zaidi, na kukosoa "uamuzi" wa utawala wa Biden juu ya hali mbaya katika Mashariki ya Kati. Viongozi wa mashirika ya misaada wamelaani mara kwa mara mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7 dhidi ya Waisraeli. Lakini mara kwa mara wameitaka Marekani kuchukua hatua zaidi kukomesha mateso makubwa ya raia katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.

Licha ya Biden na maafisa wake wa ngazi ya juu kutoa wito wa mara kwa mara wa kutaka msaada zaidi kwa Gaza, wakosoaji wanasema misaada na shinikizo hilo havijatosha.

"Uongozi wa kweli unatokana na kushughulikia migogoro ya kibinadamu kwa uwazi usioyumba wa kimaadili, na kutekeleza ulinzi wa maisha ya binadamu kuwa msingi wa diplomasia ya Marekani ," Griffiths alisema.

Lakini bado anaamini kuwa Marekani ni taifa lenye nguvu kubwa. "Katika wakati wa migogoro ya kimataifa na kwa kutokuwa na uhakika, dunia inatamani Marekani iinuke kwenye changamoto ya uongozi wa uwajibikaji, wa kanuni," alisema. "Tunahitaji zaidi. Tunastahili zaidi. Na tuna ujasiri wa kutumaini zaidi."

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanhyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi