Israel imebadilika tangu Trump aondoke mamlakani_ je amebadilika?

- Author, Jeremy Bowen
- Nafasi, International Editor
- Akiripoti kutoka, Jerusalem
- Muda wa kusoma: Dakika 7
Donald Trump amechukua wadhifa wa urais Marekani kwa mara ya pili, lakini ameleta mabadiliko makubwa Mashariki ya Kati kabla hata ya kuingia rasmi ofisini.
Alivunja mbinu za kuchelewesha zilizotumiwa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kwa kushirikiana na washirika wake wa siasa kali, ili kuepuka kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo Rais Joe Biden alileta mezani Mei mwaka jana.
Shinikizo la Marekani kwa Hamas na makundi mengine ya Wapalestina ni jambo la kawaida.
Hata hivyo, wakati wa Biden, shinikizo dhidi ya Israel lilikuwa ni kipengele ambacho hakijatekelezwa.
Trump alipoingia madarakani kwa muhula wake wa pili, alijivunia kumaliza mkataba wa kusitisha mapigano huko Gaza, jambo ambalo linampa sifa nyingi na kumfanya afurahie mafanikio hayo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa upande wake Joe Biden alikuwa yuko tayari kupoteza kura katika uchaguzi wa urais Marekani kwa kuamua kuisaidia Israel kupigana huko Gaza ,licha ya kulalamika jinsi Israel wanavyoua raia na ka kuwanyima mahitaji ya kimsingi kama vile Chakula makazi na matibabu.
Baadhi ya wazalendo wa Israel walifurahia ushindi wa Trump mwezi Novemba wakiamini kuwa Rais ajaye atawapa msaada na nguvu zaidi katika vita hivi na huenda wazo hili likawa sio wanavyotarajia.
Kwasababu Israel ni nchi ambayo imebadilika tangu Trump aondoke mamlakani 2021, Trump huenda akawa sio rais ambaye wamemzoea kama kipindi cha awali.
Uzinduzi Vs Mashambulizi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika ishara ambayo inauzito namna Trump atashirikiana na Israel ni kutokana na kipindi chake cha mwisho cha muhula wa pili alivyoiangalia nchi hiyo.
Ilikuwa ni wakati usiosahaulika wakati Hamas ilivamia Israel mwezi Oktoba tarehe 7 mwka 2023 na namna ulivyochochea mashambulizi yasio kwisha nchini Gaza kama kulipiza kisasi.
Kwa upande mmoja ilionekana washauri wakuu wa Trump wakati huo binti yake Ivanka na mumewe Jared Kushner wakizindua ubalozi mpya wa Marekani eneo la Jerusalem.
Kuhamisha kutoka Tel Aviv na kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel ilikuwa kati ya ahadi alizotoa katika kampeini zake akiwahikikishia wakristo wakievanjelisti ambao walikuwa ni asilimia kubwa ya wafuasi wake.
Katika mwaka 2020, Trump alileta makubaliano ya kihistoria ya Abraham, ambapo Israel iliingia katika ushirikiano na nchi za Kiarabu kama vile Umoja wa Falme za Kiarabu, Morocco, Sudan, na Bahrain. Makubaliano haya yalileta matumaini ya amani, lakini yalikuwa na masuala ya Wapalestina ambayo yalikuwa yamepuuziliwa mbali kwa kiasi kikubwa.
Kama ilivyokuwa kwa Netanyahu, Trump alifanya mabadiliko makubwa, akileta mvutano na masuala ya Wapalestina kwenye meza ya majadiliano. Alijua kuwa suluhu ya amani Mashariki ya Kati ilikuwa ngumu na lenye changamoto nyingi, lakini aliendelea na juhudi zake kwa kuamini kwamba yeye ni mchezaji mwenye nguvu katika siasa za kimataifa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa upande wa pili ilikuwa ni wanajeshi wa Israel wakifyatua risasi huko Gaza na kuua wapalestina ambao walikuwa wakijaribu kuvuka mpaka wa nchi hizo mbili.
Siku hiyo takriban Wapalestina 50 waliuawa na walioponea waliachwa na majeraha ya risasi .

Chanzo cha picha, Getty Images
Tukio la Wapalestina kujaribu kuvuka mpakani na kuingia Israel huenda Hamas walidhani kuwa halaiki ya watu wakiandamani italeta ufanisi nakuingia katika himaya ya Israel.
Tarehe 7 mwezi Oktoba 2023 Hamas walipanga mashambulizi na kuvamia Israel na kuwaua watu 1,200 wengi wao wakiwa ni raia wa Israel na Hamas kuchukua mateka 251 na kuwaleta Gaza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Trump anayeleta sintofahamu
Kuhamisha Ubalozi hadi Jerusalem ilikuwa ni nia ya Trump kuonyesha kuwa ni kwa maslahi ya Marekani ambayo alidhani yangekwamishwa ikiwa Tel aviv.
Alifanyauamuzi tofauti na mataifa mengine ambayo mabalozi yao wameyajenga Tel aviv.
Uzinduzi wa balozi ya Marekani ulijiri wiki moja baada ya Marekani kujiondoa katika dili la nyuklia na Iran ambayo alitaja kuwa ushirikiano huo ulikuwa umeegemea sana upande moja na haukuwa na ufanisi wowote.
Pia aliridhika kwa kuharibu mafanikio makubwa ya sera ya kigeni ya mtangulizi wake Barack Obama.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo Machi 2019 Donald Trump alikubali mamlaka ya Israeli juu ya Milima ya Golan, eneo la Syria ambalo Israeli ilikuwa ikikalia tangu vita vya Mashariki ya Kati vya 1967.
Kutambua kunyakuliwa kwa Israel kwa Golan kulivunja makubaliano ya nchi za Magharibi tangu baada ya Vita vya Pili vya Dunia kwamba mataifa hayapaswi kupata eneo kupitia hatua za kijeshi.
Makubaliano mapya ya Israel na nchi za Kiarabu
Katika mwaka 2020, Trump alileta makubaliano ya kihistoria ya Abraham, ambapo Israel iliingia katika ushirikiano na nchi za Kiarabu kama vile Umoja wa Falme za Kiarabu, Morocco, Sudan, na Bahrain.
Makubaliano haya yalileta matumaini ya amani, lakini yalikuwa na masuala ya Wapalestina ambayo yalikuwa yamepuuziliwa mbali kwa kiasi kikubwa.
Kama ilivyokuwa kwa Netanyahu, Trump alifanya mabadiliko makubwa, akileta mvutano na masuala ya Wapalestina kwenye meza ya majadiliano.
Alijua kuwa suluhu ya amani Mashariki ya Kati ilikuwa ngumu na lenye changamoto nyingi, lakini aliendelea na juhudi zake kwa kuamini kwamba yeye ni mwanasiasa mwenye nguvu katika siasa za kimataifa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hoja ilikuwa makubaliano kati ya Marekani na Saudi ya usalama yangesaidia kutuliza Mashariki ya Kati na kumshinda China.
Hata hivyo, Wasaudi walikataa kuathiri haki za Wapalestina ili kufikia mkataba na Israel na Marekani.
Hamas na Wapalestina wengine waliona kuwa haki zao zilikuwa zikipuuziliwa mbali.
Kiongozi wa Hamas, Khalil al-Hayya, alisema walishambulia Israel kwa sababu haki za Wapalestina hazikuzingatiwa, na walitaka dunia ijue kuwa Wapalestina wanalilia haki.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwana mfalme wa Saudi, Mohammed bin Salman, ameishutumu Israel kwa kutekeleza mauaji ya kimbari Gaza.
Hata hivyo, Wasaudi wamesisitiza kuwa bado wanavutiwa na makubaliano ya Marekani kuhusu kurejesha uhusiano na Israel, kwa sharti la maendeleo ya uhuru wa Palestina.
Mshauri mpya wa usalama wa taifa wa Trump, Mike Waltz, amesema kuwa mkataba wa amani kati ya Israel na Saudi Arabia ni kipaumbele kikubwa.
Alisema kuwa kama Trump angeshinda uchaguzi wa 2020, makubaliano yangefikiwa kwa kushirikiana na Saudi Arabia dhidi ya Iran badala ya kuweka suala la Palestina mbele.
Kuunda upya nchi za uarabuni
Changamoto kuu ya mbinu hii ni kwamba Saudi Arabia imeweka waziwazi ushirikiano wake wakupigania haki za Wapalestina.
Serikali ya Biden ilikubali kuwa mkataba mkubwa wa kubadilisha Mashariki ya Kati haukuwa tu kuhusu kukubalika kwa Israel na Waarabu, bali pia kukubalika kwa haki za Wapalestina na Israel.
Mnamo 14 Januari, wakati akiandaa kuondoka madarakani, Katibu wa Nchi Antony Blinken alielezea hili katika hotuba kwa Baraza la Atlantiki huko Washington.
Alisema Waisraeli lazima wamalize suala la uhusiano wao na Wapalestina, na kwamba hawawezi kudhani kuwa Wapalestina watakubali kuwa watu wasio na haki za kitaifa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Trump anatarajiwa kutoa nafasi kwa Saudi Arabia kuungana na Israel, ingawa atahitaji kukubaliana na masharti ya Wasaudi kuhusu haki za Wapalestina.
Wakati huo, Netanyahu anasema Wapalestina hawawezi kupata taifa huru.
Trump anahitaji kuchagua kati ya ushirikiano wa kibiashara na changamoto za kisiasa, hasa akiwa na lengo la kuleta amani Mashariki ya Kati, ingawa misimamo ya Saudi ni thabiti.
Itakuwa vigumu Trump kumshawishi mwana mfalme Mohammed bin Salman kubadilisha msimamo wake kuhusu Palestina.
Iwapo wataalika rais wa China huko Riyadh itatia tumbo joto Wamarekani.
Lakini je, alikuwa tayari kukubaliana na gharama kubwa za kisiasa za kuleta amani kwa Mashariki ya Kati? Hilo litakuwa jambo la kuzingatia wakati atakapojikuta tena katika Ikulu ya White House.













