Kwanini usitishaji mapigano wa Lebanon ni ahueni na sio suluhu kwa mzozo wa Mashariki ya Kati?

g
Maelezo ya picha,
Muda wa kusoma: Dakika 7

Na Jeremy Bowen

Mchambuzi wa kimataifa

Kwa watu wengi wa Lebanon, usitishaji mapigano haujaja haraka vya kutosha. Mchambuzi mkuu wa Lebanon katika mkutano kuhusu Mashariki ya Kati ninaohudhuria mjini Roma alisema hakuweza kulala kwani saa iliyopangwa ya usitishaji mapigano inakaribia.

"Ilikuwa kama usiku wa kuamkia Krismasi ukiwa mtoto. Sikuweza kungoja jambo hilo litokee."

Unaweza kuona ni kwanini kuna nafuu. Zaidi ya raia 3,500 wa Lebanon wameuawa katika mashambulizi ya Israel. Watu waliokimbia makazi yao walipakia magari yao kabla ya mapambazuko kujaribu kurejea kwenye mabaki ya nyumba zao.

Zaidi ya watu milioni moja kati yao wamelazimika kukimbia kutokana na mashambulizi ya jeshi la Israeli.

Maelfu wamejeruhiwa na nyumba za makumi ya maelfu ya wengine zimeharibiwa.

Lakini nchini Israeli, wengine wanahisi wamepoteza fursa ya kutekeleza uharibifu zaidi kwa Hezbollah.

Unaweza pia kusoma:
g
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alikutana na wakuu wa manispaa za kaskazini mwa Israeli, ambazo zimegeuzwa kuwa mahame na takriban raia 60,000 wamehamishwa kusini zaidi.

Tovuti ya habari ya Ynet ya Israel iliripoti kuwa ulikuwa ni mkutano wa hasira ambao uligeuka kuwa kelele, huku baadhi ya viongozi wa eneo hilo wakiwa wamechanganyikiwa kwamba Israel imechukua shinikizo kutoka kwa maadui zao nchini Lebanon na kushindwa kuweka mpango wa haraka wa kuwarejesha makwao raia waliohamishwa.

Katika safu ya gazeti, meya wa jimbo la Kiryat Shmona, lililopo karibu na mpaka, alisema ana shaka usitishaji wa mapigano utatekelezwa, akiitaka Israel itengeneze eneo la amani kusini mwa Lebanon. Katika kura ya maoni iliyofanywa na kituo cha Israel cha Channel 12 News waliohojiwa walitofautiana kati ya wafuasi na wapinzani wa usitishaji mapigano.

Nusu ya washiriki katika utafiti huo wanaamini Hezbollah haijashindwa huku 30% wakifikiri usitishaji mapigano utasambaratika.

g
Maelezo ya picha, Majengo yaliyoharibiwa kusini mwa Lebanon - zaidi ya watu milioni moja walikimbia nchi

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alikutana na wakuu wa manispaa za kaskazini mwa Israeli, ambazo zimegeuzwa kuwa miji ya roho na takriban raia 60,000 wamehamishwa kusini zaidi.

Tovuti ya habari ya Ynet ya Israel iliripoti kuwa ulikuwa ni mkutano wa hasira ambao uligeuka kuwa kelele, huku baadhi ya viongozi wa eneo hilo wakiwa wamechanganyikiwa kwamba Israel imechukua shinikizo kutoka kwa maadui zao nchini Lebanon na kushindwa kuweka mpango wa haraka wa kuwarejesha makwao raia waliohamishwa.

Katika safu ya gazeti, meya wa jimbo la Kiryat Shmona, lililopo karibu na mpaka, alisema ana shaka usitishaji wa mapigano utatekelezwa, akiitaka Israel itengeneze eneo la mani kusini mwa Lebanon. Katika kura ya maoni iliyofanywa na kituo cha Israel cha Channel 12 News waliohojiwa walitofautiana takriban kati ya wafuasi na wapinzani wa usitishaji mapigano.

Nusu ya washiriki katika utafiti huo wanaamini Hezbollah haijashindwa huku 30% wakifikiri usitishaji mapigano utasambaratika.

g
Maelezo ya picha, Watu walirejea makwao baada ya kutangazwa kwa usitishaji mapigano

Mwishoni mwa mwezi wa Septemba, katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York, mpango ulionekana kana kwamba ulikuwa karibu. Wanadiplomasia kutoka Marekani na Uingereza walikuwa na hakika kwamba usitishaji mapigano unaofanana sana na ule unaoanza kutekelezwa sasa ulikuwa karibu kutokea.

Pande zote katika vita zilionekana kuashiria nia yao ya kukubali kusitisha mapigano kwa kuzingatia vifungu vya azimio 1701 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo lilipitishwa kumaliza vita vya Lebanon 2006: Hezbollah itajiondoa kwenye mpaka na nafasi yake kuchukuliwa na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Wanajeshi wa Lebanon. Watakapoingia ndani, wanajeshi wa Israeli wataondoka hatua kwa hatua.

Lakini Waziri mkuu Netanyahu alienda kwenye jukwaa la Umoja wa Mataifa kutoa hotuba kali ambayo ilikataa kukubali kusitishwa kwa mashambulizi ya Israel.

Akiwa amerudi kwenye hoteli yake ya New York, mpiga picha rasmi wa Netanyahu alichukua picha wakati alipoamuru kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, pamoja na baadhi ya makamanda wake wakuu. Ofisi ya Netanyahu ilitoa picha hizo, katika kashfa nyingine ya kidiplomasia ya Marekani.

Mauaji hayo yalikuwa pigo kubwa zaidi kwa Hezbollah. Katika wiki kadhaa tangu, jeshi la Israeli lisababishe uharibifu mkubwa kwa shirika la kijeshi la Hezbollah.

Bado inaweza kurusha makombora juu ya mpaka na wapiganaji wake wanaendelea na harakati dhidi ya jeshi la uvamizi la Israeli. Lakini Hezbollah sio tisho sawa kwa Israeli.

Netanyahu: Ni wakati wa ' kutathmini'

Mafanikio ya kijeshi ni mojawapo ya mambo kadhaa ambayo yamemshawishi Benjamin Netanyahu kwamba huu ni wakati mzuri wa kusitisha vita.

Ajenda ya Israel nchini Lebanon ni finyu zaidi kuliko Gaza na maeneo mengine ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Inataka kuisukuma Hezbollah nyuma kutoka kwenye mpaka wake wa kaskazini na kuwaruhusu raia kurejea katika miji ya mpakani.

Ikiwa Hezbollah inaonekana kuandaa mashambulizi, Israel ina barua ya kando kutoka kwa Wamarekani kukubaliana kwamba inaweza kuchukua hatua za kijeshi.

Katika taarifa iliyorekodiwa akitangaza uamuzi wake, Netanyahu aliorodhesha sababu za ni kwanini ulikuwa ni wakati wa kusitisha mapigano. Israeli, ilisema, mapigano hayo yalisababisha ardhi ya Beirut kutetereka. Sasa kulikuwa na fursa ya 'kuvipa vikosi vyetu pumzi na kujiandaa,' aliendelea.

Israel pia ilikuwa imevunja uhusiano kati ya Gaza na Lebanon. Baada ya marehemu Hassan Nasrallah kuamuru mashambulizi kaskazini mwa Israel, siku moja baada ya Hamas kuingia vitani tarehe 7 Oktoba mwaka jana, ilisema yataendelea hadi kutakapokuwa na usitishaji mapigano huko Gaza.

PICHSA:

Sasa, Netanyahu alisema, Hamas huko Gaza itakuwa chini ya shinikizo zaidi. Wapalestina wanahofia kuongezeka tena kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Kulikuwa na sababu moja zaidi; kuzingatia kile Netanyahu alichokiita tisho la Iran. Kuiharibu Hezbollah kunamaanisha kuiharibu Iran.

Ilijengwa na Wairani kuunda tisho kwenye mpaka wa Israeli. Hizbollah ikawa sehemu yenye nguvu zaidi ya mhimili wa upinzani wa Iran, jina ambalo liliupa mtandao wake wa ulinzi wa mstari wa mbele unaoundwa na washirika .

Je, kwanini Iran ilitaka kusitishwa kwa mapigano?

Sawa na viongozi wa Hezbollah waliosalia, wadhamini wao nchini Iran pia walitaka kusitishwa kwa mapigano. Hezbollah inahitaji mapumziko ya vita ili kupona majeraha yake ya kivita . Iran inahitaji kukomesha umwagaji damu katika eneo lake. Mhimili wake wa upinzani sio kizuizi tena. Shambulio la kombora la Iran dhidi ya Israel baada ya mauaji ya Nasrallah halikurekebisha uharibifu.

Wanaume wawili, wote ambao sasa wameuawa, walipanga Hezbollah kuizuia Israeli sio tu kushambulia Lebanon - lakini pia kuishambulia Iran.

Walikuwa ni Qasem Soleimani, mkuu wa Kikosi cha Wakurdi cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran, ambaye aliuawa kwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani kwenye uwanja wa ndege wa Baghdad mwezi Januari 2020. Amri hiyo ilitolewa na Donald Trump katika wiki chache zilizopita katika Ikulu ya White House mwishoni mwa muhula wake wa kwanza.

Mwingine alikuwa Hassan Nasrallah, aliyeuawa kwa mashambulizi makubwa ya anga ya Israel katika viunga vya kusini mwa Beirut.

Trump, Gaza na siku zijazo

Kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon sio suluhu la moja kwa moja la mzozo wa Gaza. Gaza ni tofauti. Vita huko ni zaidi ya usalama wa mpaka, na mateka wa Israeli.

Vita vya Gaza pia vinahusu kulipiza kisasi, kuhusu uhai wa kisiasa wa Benjamin Netanyahu, na serikali yake kukataa kabisa matarajio ya Wapalestina ya uhuru.

Usitishaji vita wa Lebanon ni dhaifu na unaendeshwa kwa makusudi ili kununua muda wa kufanya kazi. Siku 60 ambazo usitishaji huo unatakiwa kuanza kutumika zitakapoisha, Donald Trump atarejea katika Ofisi ya Oval.

Rais mteule Trump amedokeza kuwa anataka kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon, lakini mipango yake sahihi bado haijajitokeza.

Mashariki ya Kati inasubiri njia ambazo zinaweza kuathiri eneo hilo. Baadhi ya watu wenye matumaini wanatumai kuwa inaweza kutaka kuunda muda sawa na ziara ya Rais Nixon nchini China mwaka 1972 kwa kufikia Iran.

Wanaosema wamekata tamaa wanahofia kuwa inaweza kuachana na dhana potofu ambayo Marekani bado inaifanya kuwa wazo la kuunda Palestina huru pamoja na Israel – katika kile kinachojulikana kama suluhu la mataifa mawili. Hilo linaweza kufungua njia ya kunyakua maeneo hayo ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel, ikiwemo sehemu kubwa ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kaskazini mwa Gaza.

Jambo la hakika ni kwamba Mashariki ya Kati haina nafasi ya kutoroka vizazi zaidi vya vita na vifo vya vurugu hadi milipuko ya kimsingi ya kisiasa ya eneo hilo . Kubwa zaidi ni mzozo kati ya Israel na Wapalestina.

Benjamin Netanyahu na serikali yake, pamoja na Waisraeli wengi wanaamini kuwa inawezekana kuwatawala maadui zao kwa kushinikiza ushindi wa kijeshi. Netanyahu anatumia nguvu, bila kuzuiliwa na Marekani, kubadilisha usawa wa madaraka katika Mashariki ya Kati kwa manufaa ya Israel.

Katika mzozo ambao umedumu zaidi ya karne moja Waarabu na Wayahudi wamekuwa na ndoto ya mara amani kupitia ushindi wa kijeshi. Kila kizazi kimejaribu na kimeshindwa.

Matokeo mabaya ya mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel ya tarehe 7 Oktoba 2023 yaliondoa kisingizio chochote kwamba mzozo huo unaweza kudhibitiwa huku Israel ikiendelea kuwanyima Wapalestina haki ya kujitawala.

Kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon ni ahueni. Sio suluhisho.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi