Kufa kwa heshima: Kuvunja miiko kuhusu wosia wa kifo cha huruma

Wanaharakati wa afya wanatetea wazo la kuishi mapenzi nchini India

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaharakati wa afya wanatetea wazo la kuishi mapenzi nchini India
    • Author, Cherylann Mollan
    • Nafasi, BBC News, Mumbai
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Mwaka 2010, IP Yadev, daktari wa upasuaji kutoka jimbo la kusini mwa India la Kerala, alipaswa kufanya moja ya maamuzi magumu zaidi maishani mwake.

Ilimbidi aamue kati ya kumweka hai baba yake – ambaye alikuwa mgonjwa wa saratani isiyotibika, ama kuachana na matibabu yote na kumuacha afe polepole.

Onyo: Makala haya yana maelezo ya kuhuzunisha

Kama mtoto alijua ni wajibu wake kufanya lolote awezalo ili kurefusha maisha ya baba yake. Lakini hatimaye alifariki akiwa peke yake katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Tukio hilo lilimgusa sana na kumsaidia kutambua umuhimu wa maagizo ya mapema katika matibabu (AMDs), yanajulikana kama wasia ambao mtu huutoa akiwa bado hai.

Wosia huo ni hati ya kisheria inayomruhusu mtu aliye na umri wa zaidi ya miaka 18 kuchagua matibabu ambayo angetaka kupatiwa ikiwa atapatwa na ugonjwa au hali mbaya bila ya tumaini la kupona na hawezi kufanya maamuzi yeye mwenyewe.

Kwa mfano, mtu anaweza kusema hataki kuwekwa kwenye mashine za kusaidia kupumua au anataka apewe dawa za kutosha za kutuliza maumivu.

Mwaka 2018, Mahakama Kuu ya India iliruhusu watu kuadika wasia wakiwa hai na kuchagua kusitishiwa matibabu chini ya miongozo maalumu ili kuharakisha kifo cha mtu.

Mpango wa kutekeleza kifo cha moja kwa moja, ili kumsaidia mtu aliye na ugonjwa usiotibika ni kinyume cha sheria nchini India.

Lakini mpango wa kusitisha matibabu ulipitishwa kisheria, ingawa bado jambo hilo halijatumika sana nchini India. Wataalamu wanasema ni kutokana na jinsi Wahindi wasivyo zungumzia juu ya kifo. Kifo mara nyingi huchukuliwa kuwa suala la mwiko na kutajwa kwake kunadhaniwa huleta bahati mbaya.

Lakini sasa kuna juhudi zinazofanywa kubadili mtazamo huo.

Mwezi Novemba, Dkt Yadev na timu yake walizindua mpango wa kwanza nchini India - katika Chuo cha Serikali cha Matibabu katika wilaya ya Kollam ya Kerala - kuelimisha watu kuhusu wasia wa namna hiyo. Mpango ambao unahusisha kutoa elimu kwa njia ya simu. Watu wa kujitolea pia hufanya kampeni za elimu na kusambaza vipeperushi.

Wafanyakazi wa kujitolea wakiwa katika hospitali inayosimamiwa na serikali huko Kollam, Kerala

Chanzo cha picha, IP Yadev

Maelezo ya picha, Wafanyakazi wa kujitolea wakiwa katika hospitali inayosimamiwa na serikali huko Kollam, Kerala
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwezi Machi, karibu watu 30 kutoka shirika la Pain and Palliative Care katika jiji la Thrissur walitia saini wasia huo. Dk E Divakaran, mwanzilishi wa shirika hilo, anasema lengo ni kufanya wazo la kutoa wasia wa kifo liwe maarufu zaidi miongoni mwa watu.

"Watu wengi hawajawahi kusikia neno hilo kwa hivyo wana maswali mengi, ikiwa agizo kama hilo linaweza kutumiwa vibaya au wanaweza kufanya mabadiliko kwa hiari yao baadaye," anasema Bw Yadev, akiongeza kuwa maswali mengi yametoka kwa watu walio na miaka ya 50 na 60.

"Kwa sasa, ni wasomi, au watu wa tabaka la juu na la kati wanaotumia shirika hilo. Kwa kutumia kampeni za uhamasishaji mashinani, tunatarajia idadi ya watu itaongezeka," anasema.

Kwa mujibu wa amri ya Mahakama ya Juu, mtu lazima aandike wasia, atie saini mbele ya mashahidi wawili, na uthibitishwe na mwandishi wa hati za sheria au afisa wa gazeti la serikali. Nakala ya wasia lazima iwasilishwe kwa msimamizi aliyeteuliwa na serikali ya jimbo.

Dr Nikhil Datar (right) handing over his living will to the custodian

Chanzo cha picha, Nikhil Datar

Maelezo ya picha, Dr Nikhil Datar (right) handing over his living will to the custodian

Sheria katika majimbo

Ingawa miongozo ipo kwenye karatasi, serikali nyingi za majimbo bado hazijaweka mipango ya utekelezaji. Dk Nikhil Datar, daktari wa magonjwa ya wanawake kutoka jiji la Mumbai, aligundua hilo miaka miwili iliyopita wakati alipojaza wasia wake na hakukuwa na msimamizi mbaye angeweza kuziwasilisha hati hizo kwake.

Kwa hivyo alikwenda kortini na serikali ya Maharashtra ndipo ikateua maafisa wapatao 400 katika jimbo hilo kutumika kama walinzi wa wasia.

Mwezi Juni, jimbo la Goa lilitekeleza maagizo ya Mahakama ya Juu kuhusu wasia na jaji wa mahakama kuu akawa mtu wa kwanza katika jimbo hilo kujisajili.

Siku ya Jumamosi, jimbo la Karnataka liliamuru maafisa wa afya wa wilaya kuteua watu wa kuhudumu katika bodi ya matibabu itakayo tumika kudhibitisha wasia wa aina hiyo. [Bodi mbili za matibabu zinapaswa kuthibitisha kwamba mgonjwa anakidhi vigezo kwa ajili ya kutekelezwa kwa wa wasia kabla ya madaktari kuchukua hatua.]

Bw Datar pia anapigia kampeni kuwepo kwa mifumo ya kidijitali ya wasia huo, ili huduma hiyo ipatikane kote nchini. Pia ameweka wasia wake mwenyewe bure kwenye tovuti yake kama mfano. Anaamini wasia huo husaidia kuzuia matatizo kwa familia na madaktari pale mgonjwa anapokuwa katika hali mbaya na hawezi kupona.

"Mara nyingi kwa sababu wana familia hawawezi kumhudumia mgonjwa nyumbani, wanamweka hospitalini. Madaktari, kwa kuzingatia maadili ya matibabu, hawawezi kuzuia matibabu. Mgonjwa huishia kuteseka bila ya uwezo wa kueleza matakwa yake," anasema Datar.

Wasia huo hauhwasiani na kusitishiwa tu matibabu, anasema Dk Yadev, anaeleza kisa kimoja ambapo mtu mmoja wasia wake ulibainisha kuwa anapaswa kuwekwa kwenye usaidizi wa maisha ikiwa hali yake inaruhusu.

"Alieleza kwamba mtoto wake wa pekee anaishi nje ya nchi na hakutaka kufa hadi mwanawe apate kukutana naye," anasema Yadev. "Una uhuru wa kuchagua jinsi unavyotaka kufa. Ni mojawapo ya haki tulizopewa, kwa nini usiitumie?" Anasema.

Watetezi wa huduma hii wanasema kuwa mazungumzo kuhusu huduma hiyo yanakua polepole, na kutoa msukumo kwa wasia huo.

Dk Sushma Bhatnagar wa Taasisi ya All India, ya Sayansi ya Tiba ya Delhi anasema hospitali hiyo inazindua idara ya kuelimisha wagonjwa kuhusu wasi wa namna hiyo.

"Kimsingi, madaktari wanapaswa kujadili wasia na wagonjwa, lakini kuna pengo la mawasiliano," anasema, akiongeza kuwa kutoa mafunzo kwa madaktari juu ya mazungumzo ya aina hiyo kunaweza kusaidia kuhakikisha mtu anakufa kwa heshima.

"Katika maisha yetu yote, chaguzi zetu huchochewa na matakwa ya wapendwa wetu au na kile ambacho jamii inafikiria kuwa ni sawa," anasema Yadev.

"Angalau katika kifo, wacha tufanye chaguzi ambazo ni kwa masilahi yetu wenyewe."

Imetafsiriwa na Rashi Abdalla