Iran: Jinsi simu yako inavyoweza kukuweka jela

Mamlaka ya Iran inafanya kila linalowezekana kukomesha usambazaji wa video na picha zinazoipinga serikali mtandaoni.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mamlaka ya Iran inafanya kila linalowezekana kukomesha usambazaji wa video na picha zinazoipinga serikali mtandaoni.

"Weka neno la siri la kufungua simu yako!" ofisa wa usalama wa Iran alimwambia mwandamanaji kwa sauti ya juu.

Kila neno alilotamka kwa ukali lilifuatiwa na ngumi ya usoni.

Kijana huyo aliye na umri wa mwanzoni mwa miaka 20 alikamatwa wakati wa maandamano katika mji mkuu Tehran Oktoba mwaka jana.

"Vikosi vya usalama vilikuwa vinamkamata mwanamke," anasema. "Baada ya kumsaidia kutoroka, afisa mmoja alinikabili na kuniangusha chini.

"Kisha maafisa wawili walinibana kwa miguu yao mgongoni na usoni, na wa tatu akanipiga kwa dakika kadhaa." Wakanyamaza na kuomba simu yake ambayo aliitoa.

Mara baada ya kupata neno la siri la kufungua simu yake pia, aliweka ndani ya gari. Kwa ajili ya usalama, hatuta mtaja yeye na wengine tutakaowaangazia katika makala haya.

"Waliendelea kunipiga huku ofisa mwengine akiendelea kufungua simu yangu na kuipekua," aliambia BBC.

"Baada ya dakika chache alisema, 'Ni safi'. Hatimaye waliniachilia." Alisema maafisa walipekua sehemu ya kuhifadhi picha kwenye simu yangu kubaini ikiwa nilirekodi video inayoangazia maandamano.

Laiti angelikuwa na video ya aina hiyo kwenye simu yake, angeshitakiwa kwa kosa la kueneza "propaganda dhidi ya nchi", sawa na waandamanaji wengine.

Utawala wa Iran unapania kubana zaidi.

Bunge kwa sasa linapitia muswada ambao utaharamisha upigaji wa filamu na kushiriki picha za "uhalifu".

Adhabu ya hadi miaka mitano jela itatolewa, na inatarajiwa kujumuisha upigaji picha wa maandamano "haramu".

Ikiwa mtu mashuhuri atatoa "taarifa ya uwongo" ambayo inaweza kuwa chochote kinachosababisha machafuko, wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 15 jela.

Hukumu ya kifo kwenye Instagram

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametaja 'mtandao' kama uwanja wa vita, na amehimiza mara kwa mara mamlaka "kupigana dhidi ya vita vya mseto vya maadui".

Anasema aina yoyote ya upinzani ni kazi ya Marekani na washirika wake.

Mwandamanaji mwingine mchanga aliniambia kwamba yeye na wengine walitishiwa "kubakwa, kuuawa na kukamatwa kwa wanafamilia" ili kuwalazimisha kufungua simu zao kwa ajili ya upekuzi.

Alizuiliwa katika bohari pamoja na watu wengine 300 mnamo Septemba. Kisha walilazimishwa kusaini "maungamo" ya uwongo ya kujihukumu.

Kiongozi mkuu wa Iran anasema maandamano hayo ni kazi ya Marekani na washirika wake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiongozi mkuu wa Iran anasema maandamano hayo ni kazi ya Marekani na washirika wake.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mahakama ya Iran pia imechapisha madai ya picha za skrini za machapisho ya Instagram na mazungumzo ya mtandaoni ili 'kuthibitisha' hatia ya kijana aliyehukumiwa kifo.

Mohammad Boroughani mwenye umri wa miaka 19 alipatikana na hatia ya "uadui dhidi ya Mungu" na kushutumiwa kwa kumdunga kisu afisa wa usalama pamoja na "kuwahimiza" watu kushiriki katika maandamano hayo.

Baada ya watu kuhamasishwa kwenye mitandao ya kijamii na nje ya jela yake mwezi Januari, kesi yake imerejeshwa katika Mahakama ya Juu kwa ajili ya kutathminiwa upya.

Afsaneh Rigot, mtafiti wa teknolojia, sheria na haki za binadamu katika Chuo Kikuu cha Harvard, anasema vifaa vya simu za mkononi vinaelekea kuwa "eneo la uhalifu".

Amekuwa akisoma matumizi ya ushahidi wa kidijitali kuhusu mateso wanayopitia watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja maarufu LGBTQ, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kwa muongo mmoja.

"Tunaona mbinu hii ikitumika hasa katika mazingira ya ukandamizaji ambapo mifumo ya serikali na polisi inatazamia kushtaki uhalifu wa mawazo, kujieleza na hata utambulisho."

Anasema mara kwa mara " kupitia njia haramu" ushahidi wa kidijitali ka,a vile picha, video au programu tumishi huchukuliwa kama ushahidi halisi.

Kisha hutumiwa kuunga mkono kesi ya serikali mahakamani wakati wa "kesi ya uwongo" wakati historia ya kile mtu anachofanya mtandaoni inaweza kuwa ushahidi bora zaidi.

"Katika nchi kama Iran, ambazo zimefanya mapenzi ya jinsiana uhalifu wa mawazo na upinzani kuwa uhalifu, dhana ya kutokuwa na hatia haipo, "anasema.

"Unafikiriwa kuwa na hatia, na ushahidi unahitaji tu kupatikana au kughushi."

"Tunaona mbinu hii ikitumika hasa katika mazingira ya ukandamizaji ambapo mifumo ya serikali na polisi inatazamia kushtaki uhalifu wa mawazo, kujieleza na hata utambulisho."

Upekuzi maalum

Vifaa vya kielektroniki hukamatwa mara kwa mara bila vibali au utaratibu unaotazamiwa.

Nyumba ya familia ya mwandishi wa habari mjini Tehran ilivamiwa mwezi Oktoba na maafisa dazeni kutoka Wizara ya Ujasusi.

Alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa wiki. Lakini hakuwa mtu pekee aliyeathiriwa na uvamizi huo.

Maafisa waliovalia nguo za nyumbani walichukua simu ya kila mtu na kisha kupekua vifaa vya watu walio chini ya umri wa miaka 40 kutafuta "ushahidi" wa kidijitali.

Kijana mmoja aliyekuwepo aliambia BBC kwamba maafisa hao walipekua mazungumzo ya WhatsApp, Telegram na Instagram.

Pia waliangalia machapisho ya mitandao ya kijamii lakini walilenga zaidi sehemu ya kuhifadhi picha.

“Mmoja wa maofisa hao alianza kunihoji kuhusu kile alichokitaja kuwa nguo ‘zisizo za kawaida’ za mwanamke katika mojawapo ya picha za familia yangu,” asema.

"Nilipoanza kubishana na afisa huyo nikisema kwamba picha hizo ni picha za kibinafsi za familia, kiongozi wa timu ya maafisa aliingilia kati na kusema 'Tafuteni tu picha na video za maandamano! Puuza picha za kibinafsi'."

Anaamini kuwa maofisa hao walikuwa wakiwalenga kwa sababu ya umri wao na historia yao ambayo ina uwezekano mkubwa wa kuhamasisha watu mitaani.

"Wanataka tu kuhakikisha kuwa ulimwengu hauoni picha za maandamano."

Tangu mamlaka ya Iran kuanza kuwanyonga waandamanaji, mikusanyiko ya mitaani imekuwa ya hapa na pale na kitovu cha vuguvugu la maandamano kimehamia kwenye mazishi.

All social media apps are now banned in Iran

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Programu zote za mitandao ya kijamii sasa zimepigwa marufuku nchini Iran

Utawala pia umeweka mtego mkali dhidi vyombo vya habari.

Vituo vyote vya utangazaji vinadhibitiwa na serikali na magazeti yanayofadhiliwa na serikali hurudia simulizi rasmi.

Jimbo pia hutumia marufuku, vitisho na kukamatwa ili kufunga machapisho ambayo yanakosoa sera za serikali.

Huku vyombo vya habari vya kawaida vikiwa vimezibwa, Wairani wengi wanategemea chaneli za TV za setilaiti zinazotangazwa nchini na intaneti ili kupata habari.

Kulingana na takwimu zilizotolewa na serikali ya Iran, 70% ya watu 84m wenye nguvu wanatumia mtandao ingawa Iran ina moja ya nafasi za mtandaoni zilizodhibitiwa zaidi duniani.

Majukwaa yote maarufu ya mitandao ya kijamii na zana za kutuma ujumbe zimepigwa marufuku nchini Iran.

Ili kukwepa vikwazo hivi, watu nchini Iran hutumia mitandao pepe ya seva mbadala na huduma za seva mbadala, ambazo zinalengwa vikali na serikali pia.

Kwa Afsaneh Rigot, ambaye pia ni mtafiti mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Ibara ya 19, hakuna jipya kati ya haya lakini dau ni kubwa sana.

"Katika mikono ya mataifa yenye mamlaka, ushahidi wa kidijitali ni silaha hatari sana."