Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 29.01.2024

TH

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta yuko kwenye orodha ya watu watatu walioteuliwa kuchukua nafasi ya Xavi huko Barcelona, ​​pamoja na kocha anayeondoka wa Liverpool Jurgen Klopp na kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann. (Gerard Romero kupitia Sun)

Arteta anafikiria kuachia ngazi kama kocha wa The Gunners mwishoni mwa msimu huu licha ya kuwa amebakiza miezi 18 kwenye mkataba wake, ingawa bado Barcelona hawajawasiliana naye. (Sport - kwa Kihispania)

Kocha wa zamani wa Ujerumani na Bayern Munich Hansi Flick pia anazingatiwa na Barcelona . (Bild)

Paris St-Germain wana uhakika wa kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle mwenye umri wa miaka 26 wa Brazil Bruno Guimaraes msimu huu wa joto (Mirror)

Brentford wamekubali mkataba wa pauni milioni 25 na Club Brugge kwa winga wa Norway Antonio Nusa, 18, ambaye pia alikuwa akivutiwa na Tottenham (Standard)

Luton wako kwenye mazungumzo na Sint-Truiden kuhusu mpango wa kumsaini beki wa pembeni wa Japan Daiki Hashioka, 24. (Telegraph)

TH

Chanzo cha picha, REX FEATURES

Liverpool wanafikiria kumuajiri mkurugenzi wa ufundi wa Bournemouth Richard Hughes kurithi mikoba ya Jorg Schmadtke, ambaye anajiuzulu kama mkurugenzi wa michezo mwishoni mwa dirisha la usajili la Januari(Mail)

AC Milan wamewasiliana na Arsenal kuhusu dili la kumnunua beki wao wa Poland Jakub Kiwior, 23. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Mshambulizi wa Lille na Canada Jonathan David, 24, ameibuka kama mchezaji anayelengwa na Chelsea . (Telefoot kupitia CaughtOffside)

Bayer Leverkusen wanatazamia kutaka kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 Jean-Philippe Mateta, ambaye thamani yake ni pauni milioni 20. (Sun)

Fulham wanatarajiwa kutuma ofa ya pili kwa mshambuliaji wa Chelsea wa Albania Armando Broja mwenye umri wa miaka 22 baada ya ofa ya awali ya mkopo, ikiwa na chaguo la kumnunua mwishoni mwa msimu kwa £25m, kukataliwa. (Teamtalk). (Teamtalk)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Aston Villa wametoa ofa ya tatu yenye thamani ya karibu £15m kumnunua winga wa Middlesbrough Muingereza Morgan Rogers, 21 (Birmingham Mail)

Everton wanavutiwa na beki wa kati wa Lyon na Ireland Jake O'Brien mwenye umri wa miaka 22.(Irish Independent)

Cardiff, Blackburn na Leeds wana nia ya kumsajili kwa mkopo beki wa Liverpool Muingereza Nat Phillips, 26. (Mail)

Kocha wa Ugiriki Gus Poyet ameibuka kama mgombeaji wa kazi ya Jamhuri ya Ireland baada ya Lee Carsley kuashiria kuwa hataki kuacha jukumu lake kama meneja wa timu ya vijana wa chini ya miaka 21 ya England (Times - subscription required)

West Ham bado wana matumaini ya kukamilisha dili la winga wa FC Nordsjaelland mwenye umri wa miaka 19 kutoka Ghana Ibrahim Osman kabla ya tarehe ya mwisho licha ya kwamba dau la pauni milioni 15 lilikataliwa.(Sun)

Sunderland wako kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu mkataba wa mkopo wa winga wa Uingereza Charles Sagoe Jr. 19 (Football Transfers)

Chelsea lazima iuze mchezaji ikiwa wanataka kufanya usajili wowote kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili mwezi huu, huku kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 23, akiendelea kuivutia Tottenham . (Football Insider)

Sunderland wamekataa ofa ya euro 16m (£13.6m) kutoka kwa klabu ya Italia, inayooripotwa kuwa Lazio , kwa Jack Clarke na hawataki kumuuza winga huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 23 muda huu wa usajili . (Fabrizio Romano)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah