Urusi yadai kuudhibiti mji wa Bakhmut, Ukraine inasema ni "mtego wa panya". Nani yuko sahihi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Huko Moscow, waliamua kusitisha operesheni ya kuudhibiti mji wa Bakhmut - - ambayo imekuwa ikiendelea kwa karibu miezi kumi. Kabla ya vita, karibu watu 70,000 waliishi huko. Sasa jiji hilo limeharibiwa vibaya na watu kuondoka, lakini mapigano yanaendelea. Hali kwenye uwanja wa vita inatathminiwa tofauti huko Moscow na Kyiv.
Mwishoni mwa wiki, mkuu wa kundi la "Wagner" PMC, Yevgeny Prigozhin, alitangaza udhibiti kamili wa Bakhmut.
"Tumeuteka jiji kabisa. Nyumba hadi nyumba, ili mtu yeyote asitulaumu kwa kutochukua hata kipande," alisema.
Prigozhin pia alitangaza kwamba anakusudia kuwaondoa mamluki kutoka kwenye huo ifikapo Mei 25 ili "kupumzika na kujiimazoezi tena", na kuhamisha nafasi zao kwa vitengo vya jeshi la kawaida la Urusi.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia ilitangaza kudhibitiwa kwa Bakhmut. Rais Vladimir Putin mara moja aliwapongeza wapiganaji wa Wagner 'Wagnerite' na wanajeshi wa wa jeshi la Urusi kwa mafanikio yao.

Chanzo cha picha, AFP
Kyiv, kwa upande wake, inapinga taarifa kuhusu kutekwa kwa mji wa Bakhmut na Warusi. Siku ya Jumanne, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, Hanna Malyar, alisema kuwa Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine bado vinadhibiti sehemu ya kusini-magharibi ya mji huo, na mapigano yanaendelea katika vitongoji kadhaa.
"Kwenye ukingo wa Kaskazini na Kusini mwa Bakhmut, tunasonga mbele kidogo," alisema Hanna Malyar.
Kamanda wa vikosi vya ardhini vya Ukraine, Kanali-Jenerali Syrskyi kwa ujumla anadai kwamba wapiganaji wa kundi la Wagner wamezagaa ndani ya jiji "kama panya kwenye mtego wa panya."
"Prygozhin anataka kutoroka kutoka Bakhmut kabla ya mtego wa panya kuanza kufungwa, na askari wa kawaida wa Shirikisho la Urusi watakuwa huko, ili baadaye waweze kusema kwamba jeshi la kawaida la Urusi halikuweza kushikilia Bakhmut," - anaamini mtaalam wa kijeshi, mkurugenzi wa kituo cha utafiti New Geopolitics Research Network Mykhailo Samus.
Kwa nini mji wa Bakhmut ni muhimu?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakati wa majira ya joto yaliyopita, baada ya shughuli za mafanikio za Kirusi kudhibiti miji ya Popasnaya, Severodonetsk na Lysychansk, Bakhmut ulikuwa mji mwingine muhimu kuudhibiti kwa mtazamo wa kimkakati.
Hesabu zao ni kuwa ni muhimu kuelekea kushambulia na kukabiliana na mashambulizi kuelekea huko Sloviansk na Kramatorsk. Vikosi vya Urusi, vilivyoimarishwa na mamluki kutoka kundi la "Wagner" PMC, walipaswa kushambulia kutoka mashariki, na kundi la Izyum - kushambulia kutoka kaskazini magharibi.
Ingefanikiwa, jeshi la Urusi linaweza kusambaratisha vikosi vya Ukraine na kukamata karibu miji yote mikubwa ya Donbas. Lakini haikufaulu.
Kuanzia Agosti 1, 2022, Warusi walishambulia kikamilifu Bakhmut na mazingira yake. nguvu ziliwekezwa kwa Kundi la Wagner PMC, ambapo kiongozi wake Prigozhin aliruhusiwa kuajiri wafungwa wa Urusi kwa wingi ili wakapigane Ukraine.
Watu wengi, haswa Prigozhin mwenyewe, waliripoti juu ya hasara kubwa kwa sababu ya mashambulio kutoka kwenye ngome za Ukraine.
Nini hasa ilikuwa lengo la operesheni ya kudhibiti Bakhmut haijulikani hata sasa. Licha ya kuwepo kwa dhana kadhaa zinazotajwa na wataalam wa kijeshi mpaka sasa hakuna lengo linaoonekana kufikiwa.
Ikiwa warusi wataudhibiti Bakhmut kweli, je, wataweza kuendelea kuushikilia?
Kuna utata. Upande mmoja wa Urusi unasema kuhusu kuudhibiti karibu mji wote wa Bakhmut na kuweka chini yao mipaka ya eneo la Kaskazini na Kusini mwa mji. Kwa upande mwingine, UWanajeshi wa Ukraine wanadhibiti upande wa magharibi mwa Bakhmut na kuendelea kupambana kwenye maeneo ya pembezoni.
"Inaonekana kwamba mamluki wa Wagner wanataka kuondoka Bakhmut haraka iwezekanavyo, kimsingi kwa sababu waliuawa huko," mwandishi wa habari na mwanasayansi wa siasa Taras Berezovets, mwakilishi wa brigedi ya Jeshi linalopigana huko Bakhmut, alisema katika mazungumzo na BBC. Wamebaki mamluki wasiozidi elfu nne na anataka atoke hapo haraka iwezekanavyo. Hapo jana alisema kuwa wapiganaji wake wameuteka kabisa mji huo, lakini wanajeshi wa Ukraine na vikosi maalum bado vinadhibiti eneo la magharibi mwa Bakhmut. Kwa hivyo, madai yote ya Warusi ya ushindi huko Bakhmut ni upuuzi ".

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la Urusi linaendesha vita vya kujihami karibu na vijiji vya Klishchiivka na Kurdyumivka kusini na Dubovo-Vasylivka na Berkhivka - kaskazini.
Vyombo vya habari vya propaganda vya Urusi vinaelekea kuonyesha kwamba kuna hatari ndogo kwa Jeshi la Urusi kusonga mbele huko Bakhmut.
Pengine, kwa sasa jeshi la Ukraine halina nguvu ya kuendeleza mashambulizi ya haraka na kujenga tishio la kweli kukabiliana na uvamizi Bakhmut. Lakini kwa Urusi pia - kudhibiti maeneo yaliyosalia ya jiji, kuyarudisha majeshi ya Ukraine na kupata angalau mapumziko si jambo rahisi.

Chanzo cha picha, Rex Features
Hasara za kijeshi huko Bakhmut
Rais wa Marekani Joe Biden alisema katika mkutano wa G7 nchini Japan kwamba Urusi imepoteza takriban watu 100,000 katika vita vya Bakhmut.
Hili ni gumu kulithibitisha kwani wahusika hawasemi kwa upande wao. Ni wazi na kawaida, jeshi linaloshambulia kutaka kuteka eneo fulani- ndio hupoteza zaidi - hadi kupata mafanikio kwa kuvunja ulinzi wa adui.
Kwa upande wa Bakhmut, hakuna kitu cha aina hiyo kilichotokea wakati sasa ni karibu miezi 10 ya mapigano.












