Vita vya Ethiopia: Nasa yaonesha eneo la vita kutoka angani

Chanzo cha picha, NASA SATELITE
Picha mpya zilizochukuliwa kutoka angani usiku zinaonesha jinsi mzozo wa eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia umewaacha watu wakikabiliwa na moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani.
Picha hizo za satelaiti za Nasa zimesambazwa na BBC huku wanajeshi wa Ethiopia na wanamgambo, pamoja na wanajeshi kutoka nchi jirani ya Eritrea, wakionekana kupata nguvu dhidi ya vikosi vya Tigrayan.
Siku ya Jumanne, Ethiopia ilisema jeshi lake limechukua udhibiti wa Shire, moja ya miji mikubwa ya Tigray, na miji ya Alamata na Korem, ambayo iko kusini mwa mji mkuu wa mkoa, Mekelle. Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Marekani, miongoni mwa mengine, wanaonya kwamba kuzuka upya kwa vita vikali kunaweza kuzidisha hali ambayo tayari ni janga kwa raia.
Takwimu mpya kutoka kwa Ofisi ya Afya ya Tigray, iliyotolewa na BBC, inaonesha jinsi kizuizi katika eneo hilo - ambacho kimesimamisha kwa kiasi kikubwa misaada ya kibinadamu na huduma nyingine kama vile umeme na benki - kumeathiri watoto wadogo.
Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya walio chini ya umri wa miaka mitano ambao wamekufa kutokana na utapiamlo imeongezeka kwa asilimia 1,533 katika kipindi cha miaka miwili kuanzia Julai 2020 - miezi minne kabla ya vita kuanza.
Dkt. Kokeb Hagos, ambaye anakusanya data za Ofisi ya Afya ya Tigray, aliiambia BBC kwamba watoto 2,450 walikufa hospitalini kati ya Julai 2021 na Julai 2022 - imekuwa vigumu kwa wafanyakazi wa afya kuzunguka eneo hilo kwa sababu ya uhaba wa mafuta huku laini za simu na intaneti pia zikiwa zimekatika.

Chanzo cha picha, AFP
Nambari zinapaswa kuandikwa kwenye vipande vya karatasi na kutumwa na usafiri wowote unaopatikana kwa ofisi, ikiwa ni pamoja na taarifa kwamba 70% ya watoto waliopatikana na utapiamlo mkali hawajatibiwa kwa sababu ya ukosefu wa chakula na dawa.
Mmoja wa watoto wanaojulikana kufariki mwaka huu ni Surafeal Mearig.
BBC iliripoti kisa chake kwa mara ya kwanza mnamo Januari 2022.
Wakati huo alikuwa na umri wa miezi mitatu na uzito wa kilo 2.3 tu (5lb), 1kg pungufu kuliko alivyokuwa wakati wa kuzaliwa.
Wazazi wake walikuwa wamekosa pesa za kununua chakula baada ya kukosa kazi.
Madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Mekelle ya Ayder, alikokuwa akitibiwa, walituambia alifariki mwezi mmoja baadaye.
Bwawa la umeme lililopigwa kwa bomu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Katika picha za Nasa za Black Marble (kuanzia Novemba 2020 hadi Agosti 2022) mwelekeo wa mzozo unaweza karibu kuchorwa - kwani zinaonesha viwango vya mwanga vikipungua katika miji ya Shire, Aksum na Mekelle.
Ni mchanganyiko wa kila mwezi wa mwanga unaotolewa kutoka kwa miji husika na dalili ya upatikanaji wao wa umeme.
Serikali ya shirikisho ya Ethiopia inadhibiti gridi ya taifa ya umeme lakini imeshutumiwa kwa kukata Tigray, ambapo umeme ulikuwa thabiti katika miji ya eneo hilo kabla ya vita, vyanzo kadhaa vimeiambia BBC.
Kulingana na uchunguzi uliochapishwa mwezi Septemba na Tume ya Kimataifa ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ethiopia, serikali "ilisitisha umeme, intaneti na mawasiliano ya simu, na huduma za benki huko Tigray mnamo 4 Novemba 2020" - siku ambayo mzozo ulianza.
Picha hizo zinaonesha mwangaza mkali katika miji ya Shire na Aksum kuanzia Novemba 2020.
Taa katika miji hiyo miwili huimarika zaidi kati ya Machi na Juni 2021 zikiwa mikononi mwa serikali. Mekelle ilisalia na mwanga hadi Julai 2021, baada tu ya jiji hilo kutekwa tena na vikosi vya Tigray.
Ilikuwa imeanguka ndani ya mwezi wa kwanza wa mzozo na kubaki angavu wakati wa miezi saba iliyokuwa chini ya udhibiti wa serikali.
"Wakati majeshi ya Tigrayan yalipochukua tena udhibiti wa sehemu kubwa za Tigray, ikiwa ni pamoja na Mekelle, mwishoni mwa Juni 2021, serikali ya shirikisho ilijibu kwa kuzima tena umeme, mtandao na mawasiliano ya simu, na huduma za benki kwa eneo hilo," ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema.
Wakati wa mzozo chanzo kikuu cha nishati kwa watu milioni saba wa Tigray kimekuwa Bwawa la Umeme wa Tekeze, ambalo lililipuliwa Desemba 2021.
Picha hizo zinaonesha jinsi taa zilivyofifia sana huko Mekelle baadaye Desemba 2021 baada ya bwawa hilo kulipuliwa na bomu.
Hata mitambo miwili inayofanya kazi inazalisha umeme bila ufanisi kwani ina hitilafu kadhaa ambazo zingeweza kurekebishwa ikiwa vipuri vingepatikana," alisema Profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Calgary.

Chanzo cha picha, AFP
Hofu ya siku zijazo
Serikali ya Ethiopia inaendelea kukataa kuwa imezuia upatikanaji wa umeme, benki na mawasiliano huko Tigray, ingawa baada ya kuteka Shire wiki hii, iliahidi ufikiaji wa mashirika ya kibinadamu katika maeneo ambayo sasa inadhibiti kupitia uwanja wa ndege wa jiji hilo.
Vyanzo vya habari kwenye mstari wa mbele viliiambia BBC kuwa muungano wa majeshi sasa unasonga mbele kuelekea mashariki kutoka Shire na kuelekea Aksum, Adwa na Adigrat.

Ni wakati wa kutisha kwa wakazi wanaokadiriwa kuwa 500,000 wa jiji hilo.
"Vita vimezidi. Siku zote tunajiuliza, ndege isiyo na rubani itakuja lini? Je, nitawapata watoto wangu wakiwa hai?" muuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Ayder aliniambia.
Mmoja wa wafanyakazi wachache wa kutoa misaada waliosalia katika kanda hiyo alisema kuwa wafanyakazi wenzake pia walikuwa wana njaa. "Chakula kilichobaki kimepungua na watu wote wana njaa," alisema. "Mamia na maelfu ya watu waliokata tamaa wanabisha hodi kwenye milango yetu wakitafuta usaidizi. Kuna watu wengi zaidi wanaokufa kwa njaa majumbani mwao, wakitarajia chakula kwa siku nyingi."
Wanahofia nini kitatokea - hasa uwezekano wa kulipiza kisasi kutoka kwa wanajeshi wa Ethiopia na Eritrea. Kwa Prof Getachew, vita hivyo vitakuwa na athari ya kudumu kwa miundombinu ya eneo hilo hata kama kizuizi kitaondolewa.
Tayari kuna ripoti za uporaji huko Shire na madai kwamba bidhaa zinasafirishwa kurudi Eritrea, kama ilivyoripotiwa kutokea sana katika miji ambayo wanajeshi wa Eritrea walichukua mapema katika mzozo huo. "Kama ni kweli, wataendelea na kile kilichosalia cha miundombinu ya umeme."
















