Vita vya Ethiopia: Hali ndani ya mji mkuu wa Tigray Mekelle

Huku vita katika jimbo la Ethiopia la Tigray vikiendelea kuwa vikali kwa mara nyingine tena, raia wanazidi kuhusika katika mapigano
Makamanda wa waasi wa Tigray wameanza kampeni ya kuwajiri, ambapo awali walishutumiwa kwa kuwalazimisha watu kujiunga na vita.
Shutuma sawa zimetolewa dhidi ya Eritrea, ambayo imeingia katika vita hivyo upande wa serikali ya Ethiopia.
BBC imepokea ripoti ya kipekee kutoka kwa mwandishi wa habari kutoka katika mji mkuu wa Tigray Mekelle, kuhusu jinsi wakazi hali ya maisha ya vita.
Ndege zisizokuwa na rubani zinapaa kwenye anga la Mekelle, lenye jumla ya watu wapatao 300,000, karibu kila siku. Ninaweza kusikia moja kwa sasa wakati nikiandika Makala hii. Inanifanya nihisi sina usalama. Katika wiki chache zilizopita mashambulio ya anga yamepiga viwanja vya michezo na maeneo ya makazi - haiku wazi maeneo yaliyolenga.
Wiki hii jeshi la Tigray limetoa wito kwa kila mtu mwenye uwezo kujiunga na mapigano – na baada ya ghasia za miezi 23 kuwachosha wanakubali wito.
"Inachukuliwa kama mwiko kutojiunga na jeshi ," anasemamkazi, ambaye jina lake BBC inalificha kwa ajili ya sababu za usalama.
Watigray wengi bado wamesalia kuwa wapinzani, wakisema hawatakubali tena utawala wa shirikisho, huku Wazri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed akiwashutumu viongozi wa jimbo kwa kuasi kwa lengo la kuchukua tena mamlaka waliyoyapoteza wakati alipoingia mamlakani mwaka 2018.
Kila mtu hapa anataka kulinda haki zake. Ghasia za hivi karibuni zilianza mwishoni mwa mwezi Agosti baada ya kuvunjika kwa mkataba wa mizi mitano wa kibinadamu.
Watu mbali mbali, wakiwemo wanawake na vijana, wanaitikia wito wa kujiunga na jeshi la Tigray People's Liberation Front (TPLF).
Wanawake wamepokea mafunzo ya kijesh, na wanasema wako tayari kupigana iwapo wataitwa kufanya hivyo.
Wanajumuisha mwanamke mwenye umri wa miaka 23 ambaye aliniambia kuwa "anajivunia kuwa Mtigray na anafurahia kuwa alipata mafunzo ya kulinda haki zangu na kuilinda ardhi yangu ".
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tigray imekuwa chini ya mkwamo tangu Juni 2021, na hali ya maisha imekuwa mbaya kwa muda mrefu.
Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu mifumo ya sim una intaneti vifungwe, na kututengenisha na ulimwengu mwingine.
Watu wamekuwa wakirejea kutumia kalam una karatasi kuandika jumbe kwa familia zao na marafiki – au wanakwenda kwenye mpaka wa jimbo la Amhara la Ethiopia kupiga sim una kupokea pesa kutoka kwa jama zao wanaoishi ng’ambo.
Makundi hukusanyika kusikiliza redio moja kando ya barabara kufahamu ni nini kinachoendelea. Kila mtu anazungumzia kuhusu mchakato wa amanina kufuatilia kwa karibu habari kuhusu hilo lakini watu wengi hapa wanaamini kuwa serikali ya Ethiopia haiku tayari kwa amani, kwasbabu hawajaacha kupiga mabomu.
Watu hapa hawawezi kufanya biashara na kupata pesa, au kupata pesa zao kutoka kwenye benki kwasababu zimefungwa. Kwahiyo biashara hakuna.
Hii imesababisha dharura ya kujitokeza kwa masoko ya wazi, ambayo yalikuwa ni kinyume cha sheria kabla ya vita, na mzunguko wa pesa katika masoko ya siri, huku madalali wakitoza faida ya walau 30%, chini kutoka 50% kilichokuwa kikitozwa miezi michache iliyopita.
Majirani zanyu wenye wanaishi kwa kutegemea pesa zinazotumwa na jamaa za familia zao zilizopo marekani na Canada.
Mmoja wa majirani anasema hawezi kuwalisha watoto wake watano kama hawatamtumia pesa. Ana madada wawili nchini Mareknani, na amepokea pesa kutoka kwa ndugu zake mara nne tangu vita vianze.
Mzozo umezuia upatikanaji wa huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na mafuta kufika Tigray. Watu wengi hutembea kwa miguu, au kubebwa kwa punda.

Bei zinaendelea kupngezeka. Teff, nafaka ambayo hutumiwa kwa kawaida kutengeneza mkate wa kitamaduni unaofahamika kama injera, hupanda kila wiki. Bei ya sasa ya kilo 100 ni (220 lb) karibu $265, ikilinganishwa na $85 mwaka mmoja uliopita.
Watu wanakufa kutokana na ukosefu wad awa ambazo haziwezi kuletwa kwasababu ya vita. Gharama ya matibabu ya magonjwa ya kudumu imeongezeka.
Kadri kila shambulio linavyowauwa watu zaidi, vijana zaidi wanasukumwa kujiunga na jeshi.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 29 aliniambia kwamba watu watatu wa familia yake – maka zake wawili na dada yake mmoja – wamejiunga na jeshi la Tigray.
Kwa kipindi cha miezi miwili amekuwa akitumia muda wake, na kutumia kidogo alichonacho, kuandaa chakula kwa ajili ya wapiganaji walioko vitani.
Wakazi wengine wanagawala chakula chao na familia za wale ambao wamekwenda kupigana.
Wakati taarifa ilipojitokeza wiki iliyopita kwamba Umoja wa Afrika umeweza kuanzisha mazungumzo na yanaweza kuanza nchini Afrika Kusini, watu walifurahi.
Lakini mazungumzo hayakuweza kufanika kwasababu ambazo hazikujulikana. Wengi hapa wanataka sana amani na makanisa na misikiti vinajaa watu kila usiku, watu wakiomba vita hivi viishe.
















