Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Marc Guehi hatajiunga na Liverpool

Palace ilimsajili Marc Guehi, kutoka Chelsea mnamo 2021

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Palace ilimsajili Marc Guehi, kutoka Chelsea mnamo 2021
Muda wa kusoma: Dakika 3

Klabu ya Liverpool haitamsajili beki wa Crystal Palace Marc Guehi mwezi Januari. The Reds walishindwa kupata pauni milioni 35 za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 wiki iliyopita. Mkataba wake utakapokamilika msimu ujao wa kiangazi. (Times - usajili unahitajika)

Majadiliano kati ya mlinzi wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate kuhusu kandarasi mpya bado yanaendelea na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye anaongoza orodha ya wachezaji wanaolengwa na Real Madrid. (Fabrizio Romano via Givemesport)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 26, amemuomba Mohamed Salah wa Liverpool kuungana naye Real Madrid. Winga huyo wa Misri, 33, alitia saini mkataba mpya wa miaka miwili Anfield mwezi Aprili lakini huenda akaingiwa na tamaa ya kuhamia Bernabeu. (Teamtalk)

Kipa wa Manchester United Andre Onana amekubali kujiunga na klabu ya Uturuki Trabzonspor kwa mkopo lakini klabu hiyo haikupewa chagua la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 29 katika mkataba huo. (Fabrizio Romano)

Onana ameongeza mshahara wake maradufu kwa kukubali kujiunga na Trabzonspor kutoka Manchester United kwa msimu uliosalia. (Mail)

Klabu za Aston Villa, Leeds United na Newcastle United zinavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 28 na huenda zikawania kumsjili Januari. (Caught Offside)

Onana akubali kujiunga na klabu ya Uturuki Trabzonspor kwa mkopo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Onana akubali kujiunga na klabu ya Uturuki Trabzonspor kwa mkopo

Klabu za Birmingham City, Wrexham na West Brom zina nia ya kumsajili kiungo wa wa Uingereza Dele Alli kwa uhamisho wa bure. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hivi majuzi alikatisha mkataba wake na klabu ya Italia ya Como. (Mail)

Kipa wa Lazio Christos Mandas, 23, anatarajiwa kuamua mustakabali wake mwezi Januari baada ya kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza, huku Wolves wakitarajiwa kufufua nia yao, baada ya kuwasilisha ombi la pauni milioni 17.3 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ugiriki msimu wa kiangazi. (Corriere dello Sport)

Beki wa Inter Milan Denzel Dumfries amesema angefurahia fursa ya kucheza Ligi ya Premia baada ya majira ya kiangazi ambapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 29, alihusishwa na Manchester United. (Metro)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi