Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Bado kuna uwezekano wa Fernandes kuhamia Saudi

Chanzo cha picha, Getty Images
Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes, 30, bado anaweza kuhamia Saudi Arabia, Tottenham wanamtaka Morgan Rogers wa Villa, huku Arsenal wakikataa nia ya Uturuki kumnunua winga Leandro Trossard.
Kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes, 30, alikataa ofa tatu kutoka kwa klabu za Saudi zinazomilikiwa na PIF msimu huu, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno akichagua kusalia Old Trafford. Hata hivyo, nahodha huyo wa United bado ana uwezekano wa kwenda Saudi Arabia kwa sababu kuna nia ya kumsajili katika msimu wa joto wa 2026. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City itamenyana na Liverpool pamoja na wababe wakubwa wa Ulaya Bayern Munich , Barcelona na Real Madrid kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace Marc Guehi, 25, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Star)
Bayern Munich wamefikiria kumnunua winga wa Liverpool Cody Gakpo majira ya joto. Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa mmoja wa washambuliaji kadhaa waliofuatiliwa na mabingwa hao wa Ujerumani, ambao walimsajili mchezaji mwenzake wa zamani Luis Diaz. (Sky Sport Germany)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea imepokea dau la pauni milioni 59.5 kutoka kwa klabu ya Saudia ya Al-Qadsiah inayoshiriki Ligi ya Mabingwa kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 msimu uliopita alikuwa Strasbourg kwa mkopo nchini Ufaransa. (Mirror)
Morgan Rogers ameibuka kama mchezaji anayelengwa na Tottenham kwa mwezi Januari. Bosi wa Spurs Thomas Frank ni shabiki wa kiungo wa kati wa Aston Villa, 23, ambaye kwa sasa yuko kwenye majukumu ya kimataifa na Uingereza. (Teamtalk)

Chanzo cha picha, EPA
Juventus wanalenga kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Cebellos Januari. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, 29, alikuwa akilengwa na klabu hiyo ya Italia msimu wa joto lakini hakuna dili lililofikiwa. (TuttoMercatoWeb)
Bournemouth wako kwenye mazungumzo ya kiwango cha juu na Olympiakos kuhusu makubaliano ya kumruhusu mshambuliaji wa Uingereza Zain Silcott-Duberry, 20, kujiunga na klabu hiyo ya Ugiriki. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal hawana mpango wa kumruhusu winga wa Ubelgiji Leandro Trossard kuondoka katika klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekuwa akihusishwa na kuhamia Besiktas lakini alisaini mkataba mpya Emirates mwezi uliopita. (Fabrizio Romano)
Beki wa Liverpool Giovanni Leoni, 18, alikataa kuhamia Newcastle alipokuwa Parma ingawa Magpies walikuwa tayari kulipa klabu hiyo ya Italia zaidi ya Reds kumsajili. (Gazzetta di Parma via Football Italia)
Kiungo wa zamani wa Liverpool , Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 34, amekubali kujiunga tena na wafanyikazi wa kiufundi wa klabu ya Barcelona chini ya kocha Hansi Flick. (Marca - in Spanish)











