Moja kwa moja, Kujitoa kwa wanajeshi wa NATO nchini Afghanistan kunastahili heshima-Prince Harry

Duke wa Sussex ametoa wito kwamba kujitoa kwa wanajeshi wa NATO kujadiliwe kwa ukweli na kwa heshima”, baada ya rais wa Marekani kudai kuwa washirika “walikaa nyuma” kutoka mstari wa mbele nchini Afghanistan.

Moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

  1. Mkuu wa jeshi la Sudan Kusini amewapa wanajeshi siku saba kuumaliza uasi

    Jeshi

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Mkuu wa majeshi ya Sudan Kusini amewapa wanajeshi siku saba “kuukandamiza uasi” mashariki mwa nchi, ambao unatishia usalama wa mji mkuu, Juba.

    Hivi karibuni, Jeshi la Ukombozi wa Watu wa Sudan kwa Upinzani (SPLA-IO) limevamia na kuteka maeneo kadhaa katika jimbo la Jonglei, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa eneo hilo aliyeliambia BBC, ingawa taarifa hizo hazikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.

    Mapigano ya hivi karibuni yameutishia mji mkuu wa Jonglei, Bor, ulioko umbali wa takribani saa mbili kwa gari kutoka Juba.

    Kiongozi wa SPLA-IO, Makamu wa Kwanza wa Rais aliyesimamishwa kazi, Riek Machar, kwa sasa yuko mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya mauaji, uhaini na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ambayo ameyakanusha.

    Kuna hofu kwamba mapigano haya yanaweza kuchochea tena vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

    Vikosi vya ziada vya jeshi la Sudan Kusini sasa vimetumwa mjini Bor, ambao ulikuwa mji wa kwanza kutekwa na majeshi ya upinzani katika mgogoro wa miaka 2013–2018. Mji huo unaonekana kuwa kituo muhimu cha kimkakati kuelekea mji mkuu.

    “Tuliwaleta hapa kwa ajili ya ujumbe maalum,” alisema mkuu wa majeshi ya ulinzi, Jenerali Paul Nang Majok, akiwaambia wanajeshi wake.

    “Ninawapa siku saba tu kukamilisha hilo, kuwamaliza waasi katika maeneo hayo na kuyarejesha chini ya udhibiti wetu.”

    Jeshi la Sudan Kusini linaungwa mkono na wanajeshi kutoka Uganda. Idadi yao halisi haijulikani. Ripoti moja imetaja idadi ya wanajeshi 4,000, lakini taarifa hiyo haijathibitishwa.

    Unaweza kusoma;

  2. Kujitoa kwa wanajeshi wa NATO nchini Afghanistan kunastahili heshima-Prince Harry

    Price Harry

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Duke wa Sussex ametoa wito kwamba kujitoa kwa wanajeshi wa NATO “zijadiliwe kwa ukweli na kwa heshima”, baada ya rais wa Marekani kudai kuwa washirika “walikaa kidogo nyuma” kutoka mstari wa mbele nchini Afghanistan.

    “Nilihudumu huko. Nilipata marafiki wa maisha huko. Na nilipoteza marafiki huko,” alisema Prince Harry, ambaye alitumwa nchini humo mara mbili, siku ya Ijumaa alipokuwa akitoa heshima kwa wanajeshi wa NATO waliouawa katika mgogoro huo, wakiwemo wanajeshi 457 wa Uingereza.

    Mwanamfalme huyo alikuwa akijibu maoni tata yaliyotolewa na Donald Trump katika mahojiano siku ya Alhamisi.

    Maneno ya Trump yamesababisha kulaaniwa na washirika wa kimataifa, huku Waziri Mkuu Sir Keir Starmer akiyataja kuwa “ya kudhalilisha na, kusema kweli, ya kusikitisha sana.”

    Uingereza na mataifa mengine yaliungana na Marekani nchini Afghanistan baada ya kifungu cha usalama wa pamoja cha NATO kuanzishwa kufuatia mashambulizi ya 9/11.

    Prince Harry alisema: “Mwaka 2001, NATO ilitekeleza Kifungu cha 5 kwa mara ya kwanza na ya pekee katika historia. Hii ilimaanisha kwamba kila taifa mshirika lililazimika kusimama pamoja na Marekani nchini Afghanistan kwa ajili ya kulinda usalama wetu wa pamoja. Washirika waliitikia wito huo.”

    Aliongeza: “Maelfu ya maisha yalibadilika milele. Akina mama na baba waliwazika wana na binti zao. Watoto waliachwa bila mzazi. Familia zinaendelea kubeba gharama ya mateso hayo.

    “Sadaka hizo zinastahili kusemwa kwa ukweli na kwa heshima, huku sote tukiendelea kubaki wamoja na waaminifu katika kutetea diplomasia na amani.”

    Unaweza kusoma;

  3. Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu