Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Barcelona wataka kumsajili Marc Guehi

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nahodha wa Crystal Palace Marc Guehi
Muda wa kusoma: Dakika 2

Barcelona wako tayari kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Crystal Palace na Uingereza Marc Guehi kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao huku Liverpool na Real Madrid wakiwa tayari wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Sport - In Spanish)

Beki wa Liverpool Joe Gomez, 28, alivutiwa na Crystal Palace na Brighton siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alibaki Anfield huku mabingwa hao wa Premier League wakishindwa katika jitihada zao za kumnunua Guehi. (Football Insider,)

Hatima ya beki wa kati wa Uingereza James Tarkowski, 31, beki wa pembeni wa Ukraine Vitalii Mykolenko, 26, na kiungo wa kati wa Uingereza James Garner, 24, itaangaliwa Everton, huku watatu hao wakiwa wameingia miezi 12 ya mwisho ya kandarasi zao. (Times - Subscription Required)

Manchester United wanaweza kurejea kumnunua kiungo wa kati wa Brighton Carlos Baleba mwaka ujao baada ya kushindwa katika jaribio lao la kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21 katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (GiveMeSport)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Emilio Martinez

Fulham watatoa kandarasi iliyoboreshwa zaidi kwa Rodrigo Muniz baada ya kumshikilia fowadi huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 24 licha ya kutakiwa na klabu ya Serie A Atalanta msimu wa joto. (GiveMeSport,)

Emiliano Martinez anatarajiwa kujumuishwa tena katika kikosi cha Aston Villa baada ya mlinda lango huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33 kushindwa kuhamia Manchester United siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Subscription Required)

Martinez yuko tayari kukataa ofa kutoka kwa Saudi Pro League na Turkish Super Lig, ambapo dirisha la uhamisho bado liko wazi, ili kusalia Villa kwa msimu mwingine. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jan Paul van Hecke

Azma ya Tottenham kumsajili Jan Paul van Hecke, 25, imeongezwa baada ya beki huyo wa kati wa Uholanzi kuamua kugoma kusaini mkataba mpya na Brighton. (GiveMeSport,)

Rangers wanaweza kurejea na ofa mpya kwa ajili ya Jesurun Rak-Sakyi wa Crystal Palace baada ya timu hiyo ya Scotland kukosa ombi la kuchelewa kumnunua winga huyo mwenye umri wa miaka 22. (Football Insider)

Wolves wameingiza kipengele katika mkataba wa mkopo ambacho kilimruhusu fowadi Sasa Kalajdzic, 28, kujiunga na LASK ambayo ina maana kwamba wanaweza kumrejesha Januari. Pia hakuna chaguo kwa klabu ya Austria kumnunua kama sehemu ya makubaliano. (Express & Star)

Imetafsiriwa na Seif Abdalla