Tetesi za soka Ulaya Jumanne 15.10.2024

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pep Guardiola
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola, 53, amevutiwa na hatua za shirikisho la Soka nchini England kumtaka kuwa meneja wake huku kocha huyo wa Manchester City akitarajiwa kuamua kuhusu mustakabali wake wiki zijazo. (Times).

Guardiola pia anafikiria kusaini mkataba wa mwaka mmoja kusalia City. (Telegraph),

Kocha wa muda wa England Lee Carsley ameambiwa hatapata kazi ya kudumu ya England. (Sun)

Newcastle United wanapanga kukubali ofa ya kiungo wa Paraguay Miguel Almiron, 30, mwezi Januari katika jaribio la kutafuta fedha za kuwekeza tena kwenye kikosi chao. (Football Insider)

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Almiron

Liverpool wanavutiwa na mlinzi Loic Bade kama mbadala wa nahodha wao wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33. Hata hivyo, Sevilla haitasikiliza ofa za chini ya euro 20m kwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mundo Deportivo – In Spanish),

Manchester United imekuwa ikimfuatilia kwa karibu winga wa Crystal Palace Eberechi Eze, 26, huku idara ya skauti ya klabu hiyo ikimfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza katika msimu mzima uliopita. (Football Transfers).

United inaweza kumsajili tena beki wa kushoto wa Uhispania chini ya miaka 21 Alvaro Carreras, 21, ambaye aliondoka Old Trafford na kwenda Benfica msimu wa joto. (Mirror)

Barcelona wameonyesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal na Ghana Thomas Partey, 31, huku wakitafuta soko huria la usajili wa wachezaji wapya. (Goal),

Mshambuliaji wa Uingereza Chloe Kelly, 26, anaweza kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu huu baada ya kuona uhusiano wake na meneja Gareth Taylor ukidorora. (Mail)

Hatua zinachukuliwa na kampuni ya usimamizi wa michezo ya A22 kuzindua Super League mnamo Septemba 2025. (AS – In Spanish),

Kiungo wa kati wa zamani wa Ufaransa Paul Pogba, 31, anastahili kurejea Machi 2025 baada ya kutumikia marufuku iliyopunguzwa ya dawa za kusisimua misuli lakini kuna uwezekano wa kuchezea Juventus tena. (Fabrizio Romano)

Pogba amekataa mpango wa klabu ya Broke Boys FC ya Urusi. (French Soccer via Mail)

Pia unaweza kusoma

imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla