Kwa nini 'kuacha kazi kwa hasira ' kunaongezeka?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuacha kazi kwa hasira kunaonekana kukithiri lakini mara nyingi kuna ushawishi wenye nguvu unaosababisha kuifanya hiyo.
Wengi wetu tumefikiria juu ya kuacha kazi mbaya kwa mtindo sawa wa kushangaza, mbali na kuwa na hasira, 'kuacha kazi kwa hasira' ni ishara ya dosari kubwa mahali pa kazi: kuanzia viwango vya afya na usalama hadi hali ya unyonyaji kazini na wasimamizi wanyanyasaji.
Janga la Covid-19 limeongeza tu msongo wa mawazo ambayo yanaweza kusababisha wafanyikazi kuacha kazi hapo hapo. Lakini kwa vile kuacha hasira kunaelekea kuwa kilele cha mfululizo wa masuala ya kazi, waajiri wanaweza kuepuka wafanyakazi kuacha hovyo kwa kuzingatia ishara za onyo - kabla ya mfanyakazi kuondoka.
Jinsi 'kuacha kazi kwa hasira' kunavyokuwa
Wazo la kuacha kazi kwa hasira limekuwepo tangu muda mrefu, Ingawa hasira ya kuacha inaweza kuonekana na kuhisi kuna msukumo, kutoridhika na kazi huendelea kujijenga hadi tukio litakalosababisha kuacha kazi kutokea.
Na kuwa na sehemu salama ya kwenda kama vile chaguo nyingi za kazi, chanzo kingine cha mapato (kama vile bima ya ukosefu wa ajira) au fursa ijayo (kama vile shule) kunaweza kurahisisha kuvuta kichocheo hicho.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna ukosefu wa takwimu kuhusu kuacha kazi kwa hasira, lakini Peter Hom, mtaalamu katika Chuo Kikuu cha Arizona State nchini Marekani, anaonyesha kwamba nchini Ujerumani, kwa mfano, wafanyakazi wa makampuni makubwa huadhibiwa kwa kuacha kazi bila taarifa.
Marekani ina ajira nyingi zaidi ambazo waajiri wanaweza kuwafuta kazi bila sababu, kwa hivyo itakuwa na maana kuwa mtu kuacha kazi kwa hasira ni jambo la kawaida huko.
Sajeet Pradhan, ambaye anatafiti tabia ya mashirika katika Taasisi ya Usimamizi ya India ya Tiruchirappalli, anasema ikilinganishwa na Marekani na Ulaya, India "inautamaduni wa kustahimili zaidi(kwa bahati mbaya) dhidi ya unyanyasaji kazini", kwa sababu ya " malezi ambayo yamewekewa masharti kama kuheshimu watu walio katika nafasi za mamlaka”.
Nchini India, kulingana na Pradhan, "kuacha kkazi wa hasira kwa ujumla kumeshuhudiwa katika kazi za ujuzi wa juu na vijana wa sasa wa milenia".
Kwa ujumla, anasema Nita Chhinzer, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Guelph nchini Kanada, "watu wenye elimu ya juu wana uwezekano mkubwa wa kuacha kazi, kwa sababu wanafikiri kuwa ujuzi wao unaweza kuhama".
Hata hivyo wale walio na ujuzi wa chini, ajira hatari mara nyingi wanaweza kuacha kwa taarifa ndogo. Peter Hom anarejelea watu wanaofanya kazi katika viwanda vinavyoendeshwa nchini China na Mexico: "Ni kama viti vya muziki - wanaruka kutoka kazi moja hadi kazi nyingine."
Na ingawa wafanyakazi wachanga wakati mwingine huchukuliwa kuwa dhaifu, "ukweli ni kwamba kabla ya kuwa na gharama kubwa, kwa uwekezaji uliozama katika shirika, wanafanya uamuzi kuhusu kile kinachofaa kwao", anaongeza Chhinzer. Inaleta maana kwamba wanaweza kuacha kazi isiyofaa kwa hiari zaidi.
Kitu gani kinachochea hasira za kuacha kazi?
Ingawa kuna sababu nyingi za kuacha kazi isiyoridhisha, kuna mifumo fulani ya mara kwa mara ambayo husababisha kuacha kwa hiari. Moja ya sababu za kawaida ni usimamizi mbaya. Unynyasaji wa wasimamizi unaweza kusababisha kuchoka kihisia. Wakati wasimamizi wanashindwa kushughulikia maswala ya mara kwa mara ya wafanyikazi, matokeo yake yanaweza kuwa wafanyikazi hao wanaoacha kazi kwa hasira.
Usimamizi mbaya mara nyingi huhusishwa na sababu zingine ambazo watu hukasirika na kuacha kazi, kama vile ratiba ngumu, kufanya kazi kupita kiasi na kuondoa maswala ya usalama.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Sarah alikumbana na haya yote katika muda wa miezi mitatu wa hivi karibuni kama mshika fedha katika duka dogo huko Michigan, Marekani.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa amehamia na wazazi wake Alinuia kufanya kazi kwa muda tu alipokuwa akijiandaa kwenda chuo huko Toronto, lakini madai makubwa ya meneja hivi karibuni ya kumtaka afanye kazi kwa muda wote yalimkatisha tamaa.
Pia ilikuwa wazi kuwa usalama wa wafanyikazi haukuwa kipaumbele. Sarah alihisi kutokuwa salama kwa njia nyingi: wateja walevi wakati mwingine walikuwa wagomvi, watu wengi walikataa kuvaa barakoa na alikuwa mfanyakazi pekee katika duka.
Jaribio la mwisho ilikuwa wakati mteja alipoanza kumnyemelea. Sarah alimwomba meneja wake kumhamishakutoka kwenye nafasi yake dukani, ambapo mteja yeyote aliweza kuona ni lini atafanya kazi, na kumpeleka kwenye sehemu ya faragha.
Sio tu kwamba meneja alikataa, lakini pia alimfokea Sarah kwa kumtaja mhusika. "Bosi wangu mara moja hakusita. Alikuwa kama, ‘Unahitaji kuwa mtu mzima. Kwa nini wewe si mtu mzima kuhusu hili?’ Alirudia hivyo mara nyingi sana,” asema Sarah.
Aliachana na kazi hiyo, mwezi mmoja kabla ya kazi hiyo kuisha. "Nilijisikia vibaya sana kwa sababu nilitakiwa kuweka wiki mbili [notisi] ... Lakini basi kadiri nilivyofikiria juu yake, nilikuwa kama, hii haifai kwangu. wakati au usalama wangu.”
Kiimarishaji cha Covid
Baadhi ya mashinikizo haya ya wafanyikazi yamechochewa wakati wa janga la Covid-19. Chhinzer anasema kuwa mnamo 2020, viwango vya kuacha kwa ujumla vilishuka ambapo watu walishikilia kazi.
Lakini kuacha kazi kumeongezeka mnamo 2021, "wasimamizi na mashirika na idara za Utumishi wana wasiwasi sana juu ya kuhifadhi uwezo". Walakini, kama uzoefu wa Sarah unavyoonyesha, wasiwasi huo sio kila wakati hutafsiri kuwa ulinzi bora wa wafanyikazi, haswa katika majukumu yanayolipwa kidogo.
Hakika, usalama umekuwa kichocheo cha kawaida kwa wafanyikazi wanaowakabili wateja kuacha kazi kwa hasira.
Muuguzi ambaye wenzake walieneza habari potofu kuhusu chanjo; mfanyakazi wa mgahawa ambaye wasimamizi wake huficha ukweli kwamba Covid imekuwa ikienea kati ya wafanyikazi; au mfanyikazi ambaye ana wasiwasi juu ya kusambaza virusi kwa jamaa aliye hatarini wote wameacha kazi ghafla wakati wa janga hilo.
Covid-19 imeleta mwelekeo mwingine kwa wasiwasi huu wa mahali pa kazi. Kwa wale ambao wmeacha kazi kwa hasira, hasa wale walio na 'mawazo ya kifo', sehemu ya 'hasira' "inaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kuchochewa na ukweli kwamba waajiri wanashindwa kutoa hatua za kutosha za usalama kulinda afya ya wafanyikazi wao", anabainisha Rui ( Hammer) Zhong, mwanafunzi wa PhD katika Chuo Kikuu cha British Columbia nchini Kanada.
Njia mbadala ya kuacha kazi kwa hasira
Kwa mtu anayejaribiwa na hasira, inaweza kuwa muhimu kupata mtazamo juu ya kile kilicho chini ya hasira, zaidi ya kuridhika mara moja kuwa na bosi mbaya.
Pia ni muhimu kuzingatia kwa nini watu wengi hawaachi kazi ghafla na kwa hasira. Simulizi za wafanyakazi wanao na kazi nyingi kupita kiasi ili kuwaridhisha wakubwa wao na wakati mwingine zinatia moyo. Lakini bila shaka inasikitisha kuacha bila mpango mbadala.

Chanzo cha picha, Getty Images
Alexander alikuwa na bahati ya kutotegemea kazi yake ya kupiga muziki DJ, kwani kazi yake kuu ilikuwa kama mwanasayansi. "Hakika ingekuwa vigumu zaidi kuondoka ikiwa sikuwa na kazi nyingine tayari," anabainisha.
Na sio kila mtu anayeweza kumudu kuacha kazi ya inayokandamiza au kuondoka na hundi ya mwisho ya malipo bila kutarajia, kwa hivyo sio muhimu kila wakati kwa wale ambao wamesimama kwa miguu miwili kuwahimiza wengine kuacha kazi mbaya mara moja.
Ikiwa mfanyakazi ataacha kazi kwa hasira, hii inapaswa kuwa tahadhari kwa mwajiri. Miezi sita baada ya Alexander kuondoka kwenye klabu iliyokuwa na joto kupita kiasi akiwa ameshika vifaa vyake vya DJ, walipatana na mmiliki na kurudi.
Lakini mwaka uliofuata aliondoka tena, kufuatia ahadi zilizovunjwa na hazikutimia na hali zisizo salama za kufanya kazi. "Hiyo ilikuwa mara yangu ya mwisho kufanya DJ nje ya nyumba yangu. Nilichoshwa tu na jambo hilo lote.”















