Norland: Taasisi inayoelimisha yaya wa gharama kubwa zaidi

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanaweza kuwa wamevalia sare maridadi lakini usifanye makosa ndani ya madarasa ya yaya (wafanyakazi za ndani) na walezi wa watoto katika shule hii hujifunza ujuzi wa kisasa kama vile usalama wa mtandao na kuendesha gari kwa kiwango cha juu.

Ni wanafunzi wa Norland, taasisi ambayo imekuwa ikitoa elimu kwa yaya wa bei ghali zaidi sokoni kwa miaka 130, ambao watawalea watoto wa familia tajiri zaidi nchini Uingereza pamoja na familia ya kifalme.

Katika shahada yao ya kwanza ya miaka mitatu katika malezi na elimu ya utotoni, "Norlanders" husoma baadhi ya ujuzi wa kitamaduni wa biashara hiyo kama vile kupika na kushona lakini pia na masomo mengine kama vile karate (martial arts) .

"Ndio maana mara nyingi kuna utani kuhusu sisi kuwa mchanganyiko wa James Bond na Mary Poppins," Janet Rose, mkuu wa shule hiyo, aliambia BBC, na kuongeza:

"Tumeweka vipengele vya kiutendaji ambavyo vilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1892 lakini tumehakikisha baada ya muda kwamba mtaala unabaki kuwa muhimu kwa miaka ya sasa, kwa hivyo sasa tuna mtaala wa kisasa sana wa karne ya 21."

Kwa nini karate?

"Usalama binafsi ni jambo ambalo linatuathiri sisi sote kwa sasa, kwa mfano, tulikuwa na baadhi ya wahitimu ambao walikumbwa na shambulio la Westminster," anasema mkurugenzi huyo, akizungumzia kile kilichotokea Machi 2017 baada ya mtu mmoja kuendesha gari na kuogonga makumi ya watu karibu na Bunge na kumchoma kisu polisi.

"Mhitimu wetu alikwama ndani ya jumba moja la makumbusho, ninavyoelewa, kwa takriban saa nne au sita na alilazimika kumlinda mtoto mdogo lakini aliweza kutulia na kumtuliza mtoto."

Hivi sasa, taasisi hiyo ipo huko Bath, jiji la ndani la Uingereza linalojulikana kwa magofu ya mabafu kutoka kwa Warumi lakini asili yake ni London, ambapo Septemba 25, 1892, Emily Ward aliweka misingi ya kile ambacho kingekuwa Taasisi ya Norland huko Norland Place.

"Kwa kufanya hivyo, aliunda taasisi ya kwanza ya elimu kutoa mafunzo ya aina yoyote ya malezi ya watoto na taaluma ya wataalamu waliofundishwa kulelea watoto," chuo kinasema kwenye tovuti yake.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Taasisi inaadhimisha miaka 130 ya kuendelea na masomo.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Watahiniwa wa kwanza walitoka katika taasisi zinazofundisha walimu wa shule, kama vile Chuo cha Stockwell na Chuo cha Preceptors na walikuwa na uzoefu wa kutunza Watoto ama kwa njia isiyo rasmi kutunza wanafamilia wadogo zaidi au watoto wa marafiki au rasmi zaidi kama watawala.

 Kama sehemu ya vigezo vya kujiunga, watahiniwa walitakiwa kufaulu mtihani wa maarifa ya jumla.

 Kupitia rekodi za zamani, imeweza kuonekana kuwa wengi walitoka kwa familia zenye rasilimali nzuri, kwani katika kitengo cha "kazi ya baba" (hakukuwa na sehemu ya kazi ya akina mama kwa sababu ilieleweka kuwa hawakuwa nazo ) kuna mifano mingi ya taaluma kuliko biashara.

 Wanafunzi wengi walioandikishwa katika miaka hiyo ya kwanza walikuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30. Umri wa chini ulikuwa 18, ingawa kulikuwa na baadhi wa umri tofauti kama vile Edith Sperling, ambaye alikuwa na umri wa miaka 15 aliyejiandikisha 1893.

 Mwaka 1911, Emily Ward aliandika kwamba taasisi aliyoanzisha ilimwakilisha bora: "uboreshaji wa malezi ya watoto kama msingi wa kweli wa maisha ya familia, kwani kazi hii sio ya huduma au ya nyumbani, lakini ni ya kielimu ... kwasababu tabia, mawazo na maadili ambayo huundwa katika utoto ndio hutengeneza maisha." Umuhimu wa kazi ya yaya ni jambo ambalo watangulizi wao bado wanaitetea, zaidi ya karne moja baadaye.

 "Cha kufurahisha, kuzingatia malezi ya watoto kama taaluma ni vita ambayo tunaendelea kupigania leo, kwa sababu malezi ya watoto bado yanaonekana na jamii kuwa ya hali ya chini na malipo duni kwa ujumla.

Sivyo ilivyo kwa wahitimu wetu, tunashukuru, lakini bado tunapambana na hilo."

Mishahara ya kuvutia macho

Mshahara mdogo si tatizo kwa wanafunzi wa Norland.

 Rose anasema, pamoja na kuajiriwa kwa 100%, wahitimu wanapata mishahara zaidi ya wastani.

 "Wastani wa kipato cha wanafunzi wetu mwaka wanaohitimu ni takriban £40,000 kwa mwaka (kama $47,500), lakini baada ya miaka mitano huenda wana wastani wa zaidi ya £50,000 (kama $60,000), £65,000 (zaidi ya $77,000), au zaidi. Sasa hivi tunayo ajira katika eneo ya karibu dola za Marekani 120,000," anaeleza mkurugenzi huyo.

Mandy Edmond, mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo, anasema mara nyingi wanatania kwamba yaya wa Norland ndio pekee wanaoweza kununua nyumba huko London.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Aina hii ya mshahara huvutia waombaji wengi, karibu 240 kwa nafasi 100 zinazopatikana kwa mwaka.

 BBC News ilimuuliza Edmond kama hakukuwa na hatari ya kuvutia wanafunzi wanaopenda pesa zaidi kuliko kazi.

 "Siku zote kuna wengine wanaokuja na nia hiyo, lakini hilo liko wazi katika mahojiano. Tumekuwa tukifanya hivi kwa miaka 130 ili tuweze kutofautisha na wale ambao wana mapenzi ya kweli."

Mabadiliko ya taratibu

Kama Kate, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 20, anavyoeleza faida ya kiuchumi huanza mara tu wanapotoka darasani.

"Mwaka wetu wa nne ni mwaka wa majaribio, lakini kimsingi ni mwaka wa kulipwa, wakati bado tuko kwenye mazoezi na hiyo inashangaza ikilinganishwa na watu wengi ninaowajua ambao wanahitimu na hali yao bado haieleweki."

Mwanafunzi mwingine, Ike, 23, anakiri kwamba watu hushangaa wanaposikia anachoweza kupata kutokana na kulea watoto: "Sijui rafiki yangu yeyote ambaye anapata pesa nyingi hivyo."

Ike ni mmoja wa wanafunzi wachache wa kiume katika chuo hicho. Ingawa mambo mengi yamebadilika tangu 1892, uwepo wa wanaume bado ni ubaguzi.

Kulingana na Naibu Mkurugenzi Edmond, kwa sasa kuna asilimia 5 tu ya wanaume walioandikishwa.

HHH

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katsuki Yuzawa alikuwa mwanamume wa kwanza kuhitimu kutoka Chuo cha Norland, Oktoba 1999.

Kwa Ike, tamaa ya kuwajali wengine inatokana na historia yake ya binafsi. Yeye na dada zake watatu walichukuliwa na mwanamke ambaye alibadili maisha yao halisi kwa uamuzi huu.

"Nadhani watu wengi wanafikiri kuwa kulea watoto ni jambo la msichana, lakini mimi ni mvulana wa kawaida na ninaipenda."

Wateja wa Norland wanasema nini kuhusu walezi wa watoto? Janet Rose anasema kwamba, ingawa polepole, kila kitu kinabadilika.

"Kwa mfano, tumeanzisha sare zetu za kwanza zisizoegemea kijinsia moja. Tuna jamii tofauti sana na tunaamini tunahitaji kuzalisha wanafunzi wanaoakisi utofauti huo."