Jinsi sheria mpya inavyowabana wapenzi wa jinsia moja Urusi

"Mimi ndiye malkia pekee niliyebaki nahangaika nchini Urusi," Danya ananiambia kwa majivuno yote wakati akijiremba vipodozi vya kuashiria shetani mweupe mbele ya kioo. Tumekaa jikoni kwake huku bendera yenye rangi za upinde wa mvua ikiwa imepamba ukuta.
Danya anaigiza katika filamu ya maudhui ya kutisha - kwenye Halloween. Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifanya onesho mara kwa mara kwenye klabu ya usiku ya queer huko St Petersburg inayoitwa Gender Blender.
Lakini mradi huo sasa umeacha kufanya maonesho yake baada ya sheria mpya dhidi ya wapenzi wa jinsia moja -LGBT kupitishwa na Bunge la Urusi mnamo mwezi Disemba. Hivyo kazi ya Danya imeisha.
"Kulingana na sheria, ni marufuku kufanya kile tunachofanya," Danya anasema. "Tuna wasiwasi zaidi sasa. Hatari ni kubwa zaidi."
Sheria hiyo mpya inapiga marufuku "propaganda ya mahusiano ya kingono yasiyo ya kitamaduni" miongoni mwa rika zote. Mtu yeyote atakayepatikana akifanya "kosa" hilo anaweza kutozwa faini ya hadi $5,840 ambayo ni faini ya juu zaidi kwa mashirika au waandishi wa habari.
Tangu sheria hiyo ipitishwe, Danya ameamua kuondoka Urusi na kuhamia Ufaransa. Anasema kuwa kuishi katika nchi ambayo ni kinyume cha sheria "kuwa wewe tu" kunamfanya ahisi hofu.

"Mikono yangu imefungwa. Sina chaguo tena. Ama niondoke nchini, au nibaki hapa na kungojea hali kuwa mbaya zaidi. Kinachotokea sasa - kinatisha sana."
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mswada huo ulianza kupitia mfumo wa sheria wa Urusi katika msimu uliopita wa joto, muda mfupi baada ya Moscow kuanzisha kile kinachoitwa operesheni maalum ya kijeshi.
Muda sio suala la bahati mbaya: Vladimir Putin anasema kwamba Urusi haipigani tu na Ukraine kwenye uwanja wa vita, lakini pia inapambana na maadili ya "Magharibi". Wakati akisoma hotuba yake huko Kremlin kuashiria kushikilia mikoa minne ya Ukraine, rais alikashifu haki za Magharibi na LGBT, na kuziita "Ushetani haswa".
Mwanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja Piotr Voznesensky anasema uhusiano wa vita nchini Ukraine ni upo kwa upande wake. Katika makazi yake St Petersburg, ananionesha maonyesho ya wapenzi wa jinsia moja aliyofanya kwa muda mfupi – ‘Russia first’. Alifungua maonyesho hayo kwa umma Septemba mwaka jana lakini alilazimika kuyafunga tena mara tu sheria mpya ilipopitishwa.
Anasema sheria hiyo ni jaribio la Urusi la kutaka kugeuza mawazo ya umma kuwa mbali na vikwazo kwenye uwanja wa vita. "Vita vinasababisha uchumi kuharibika na mamlaka zinahitaji kuwaonesha watu kile ambacho wamekihatarisha katika maisha yao," anasema Piotr. "Na wazo bora zaidi walilo nalo ni kuwatafuta wao wapenzi wa jinsia moja kuwa mbadala- LGBT."

Hii sio sheria ya kwanza kuweka vizuizi kwa jamii ya watu wa Urusi. Miaka kumi iliyopita, mswada ulipitishwa kupiga marufuku kile kinachoitwa "propaganda za wapenzi wa jinsia moja" kuhusiana na watoto. Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa ilifuatiwa na ongezeko la mashambulizi ya chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Urusi.
Olga Baranova, kutoka Kituo cha Jumuiya cha Moscow cha Mipango ya LGBT+, aliniambia kuwa sheria mpya itawanyanyapaa zaidi wapenzi wa jinsia moja.
"Tutadidimizwa zaidi, kutakuwa na ndoa za uongo, familia za uongo. Wale waliobahatika wataondoka nchini. Wale ambao hawawezi kuondoka nchini watadidimia zaidi na kutafuta washirika kwa namna fulani - kwa kutumia njia zilizofungwa."
Wasiwasi uliopo sasa kwa miongoni mwa jumuiya ya LGBT ni jinsi gani, lini na dhidi ya nani sheria hiyo itatumika. Sheria za Urusi hazieleweki kabisa, na kuzipa mamlaka chombo butu ambazo zinaweza kutumika kiholela.
Lakini hofu inayotokana na sheria hiyo tayari inasababisha udhibiti: sinema za mtandaoni zimefuta filamu zenye maudhui ya wapenzi wa jinsia moja na hata vipindi vya TV kuhariri matukio ya wapenzi wa jinsia moja .

Vitabu, pia, vinakaguliwa na Maduka yote nchini yameondoa mada zilizo na mandhari na wahusika wa LGBT kutouzwa. Katika duka moja la vitabu la St Petersburg, ninapata jina lililotolewa hivi karibuni, Shattered - hadithi ya mapenzi kati ya wanaume wawili. Kwa kuwa kitabu kimefungwa kwa plastiki, lazima ninunue ili kutazama ndani. Maandishi yamechapishwa upya, na sehemu zote zimebadilishwa kwa kuekewa mistari nyeusi.
Mmoja wa waandishi mwenza wa sheria, ambaye ni mzalendo mwenye chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja anayeitwa Vitaly Milonov, anakubali kuzungumza nami kupitia kiunga cha video. Inadaiwa yuko katika mji wa Horlivka mashariki mwa Ukraine unaokaliwa na Urusi ambako ameenda kujitolea kupigana. Anakanusha shutuma kuhusu sheria hiyo ya kibaguzi, akisema maisha binafsi ya watu yataheshimiwa.
Wakati ambapo maelfu ya watu wanakufa nchini Ukraine, Urusi imetengwa kimataifa na watu wanaikimbia nchi hii, ninamuuliza ikiwa inafaa kuzingatia sheria ya LGBT. "Urusi haijatengwa, tuna mzozo na ulimwengu wa Magharibi!" Bwana Milonov anasema. "Kwa nini utuelekeze kuwa tuna itikadi potofu? Nadhani ni haki yetu kuu kuwa na sheria ambayo tunapenda kuwa nayo."
Nikiwa nimerudi kwenye makazi ya Danya, ananionyesha baadhi ya mavazi ambayo amebuni kwa ajili ya kitendo chake cha kukokota. Watazamaji katika vilabu vya St Petersburg wanapenda uigizaji wake mbadala, anasema. Hataki kuondoka nchi hii.
"Ni Urusi gani unaweza kufikiria kutaka kuishi?" Nilimuuliza. "Urusi huru," ananiambia, akifikiria juu ya swali hilo kwa uangalifu. "Moja ni kuwa haihujumu haki za msingi za binadamu ambazo kila mtu anapaswa kuwa nazo. Kwa sababu nadhani mwelekeo wangu ni haki yangu tangu kuzaliwa, na hakuna mwenye haki ya kuifuta, kuipiga marufuku, au kunishtaki kwa hilo."










