Mawaziri wa ulinzi wa Marekani na Urusi waijadili Ukraine katika mazungumzo ya nadra

Chanzo cha picha, Getty Images
Mawaziri wa Marekani na Urusi wamezungumza kwa njia ya siku, katika mawasiliano ya ngazi ya juu baina ya nchi mbili tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi katika Ukraine.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin na mwenzake wa Urusi Sergei Shoigu walizungumza Ijumaa, nchi mbili zimethibitisha.
Kila upande ulisema kuwa hali katika Ukraine ilijadiliwa.
Ni mara ya kwanza wawili hao kuzungumza tangu walipowasiliana kwa njia ya simu tarehe 13 Mei.
Bada ya mazungumzo ya Ijumaa, katibu wa habari wa Pentagon Brigadia Jenerali Pat Ryder aliiambia BBC kuwa Uingereza BBC ina "hamu ya kuendelea kuwa wazi kwa ajili ya mazungumzo ".
"Waungwana hawa wawili hawajaongea tangu mwezi Mei, kwahiyo Waziri Austin aliichukulia leo kama fursa ya kuungana na waziri Shoigu," alisema.
Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kwamba "maswali ya sasa ya usalama wa taifa yalijadiliwa, ikiwa ni pamoja na hali katika Ukraine ".
Baada ya mazungumzo ya awali mwezi Mei, Bw Austin alimtaka mwenzake kutoa wito wa kusitisha mapigano mara moja - ombi ambalo halikutajwa katika mazungumzo ya sasa.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hii inakuja baada ya rais wa Urusi Vladimir Putin kudokeza kwamba huenda akawa tayari kutumia silaha za nyuklia katika Ukraine, na tahadhari dhidi ya hili kutoka kwa rais wa Marekani Joe Biden.
Maafisa katika katika nchi za Marekani na Uingereza wote wanasema wanaamini fursa ya Bw Putin ya kufanya haya ni ndogo.
Alipoulizwa iwapo mazungumzo ya simu baina ya viongozi hao yalikuwa yamepangwa kama jibu la suala hili, Brigadia Jenerali Pat Ryder alisema kwamba wakati vidokezo vya Putin vimekuwa vya ‘ukosefu wa uwajibikaji na vya kutia hofu’ Marekani imeona "hakuna dalili wakati huu’’ kwamba Urusi imeamua kutumia silaha za nyuklia.
Mahusiano baridi baina ya Urusi na Marekani yamekuwa mabaya hata zaidi tangu Urusi ilipoivamia Ukraine.
Viongozi wa nchi zote mbili walikuwa na mkutano katikati ya mwaka 2021, ambao ulisifiwa kama hatua nzuri kuelekea uhusiano bora. Lakini mazungumzo haya yalikwama kutokana na kuongezeka kwa vita juu nchini Ukraine.
Bw Putin na Bw Biden walifanya mazungumzo kadhaa ya simu miezi kadhaa kabla ya vita, ambapo rais wa Marekani alimuonya mwenzake kuacha vita.
Hapajafanyika mazungumzo baina ya viongozi hao wawili tangu uanze uvamizi nchini Ukraine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanaume wote wawili wako tayari kuhudhuria mkutano wa G20 nchini Indonesia mwezi ujao, lakini wameashiria kwamba wataepuka mkutano.
Marekani ilijibu vita kwa vikwazo kwa Urusi, na kuongeza msaada mkubwa wa kijeshi kwa Ukraine.
Mapema wiki hii Bw Biden alimshutumu Bw Putin kwa kujaribu kuwatisha Waukraine ili wasalimu amri, baada ya kutangaza sheria ya kijeshi katika majimbo manne ya Ukraine yaliyonyakuliwa hivi karibuni.
Rais wa Urusi kwa sasa yuko katika "nafasi ngumu sana", alisema, na "nyenzo pekee iliyopo kwake ni kuwatesa raia binafsi katika Ukraine".
Awali Urusi iliipinga Marekani na Magharibi kwa kujaribu kushawishi vita kwa kutoa silaha na msaada mwingine kwa Ukraine.
Katika mojawapo ya hotuba za chuki zaidi dhidi ya Marekani, Bw Putin alizishutumu nchi za Magharibi kwa kuwa "wakoloni" mwezi uliopita, wakati alipoadhimisha kunyakuliwa kwa majimbo manne ya Ukraine.
















