Je, Urusi itasimamisha mashambulizi nchini Ukraine ili kuliokoa jimbo la Kursk?

Wanajeshi wa Ukraine wanaendelea kusonga mbele katika eneo la Kursk, ingawa kasi ya awali imepungua sana

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Mashambulizi ya Ukraine katika eneo la Kursk yamekuwa yakiendelea kwa siku 15, lakini hadi sasa moja ya kazi zake kuu, kulazimisha Urusi kupeleka tena wanajeshi kutoka sehemu nyingine za mstari wa mbele,haionekani kukamilika.

Hii itaruhusu vitengo vya Wanajeshi wa Ukraine, ambavyo vinazuia mashambulizi ya mara kwa mara ya Urusi huko Donbass, kupumua na, ikiwezekana, kuboresha mbinu zao.

Wataalamu wengi wana shaka kwamba uhamisho wa askari wa Kirusi utatokea hivi karibuni na kwa idadi kubwa.

Ukweli, baada ya kuanza kwa operesheni ya Kursk, Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine vimerekodi kupungua kwa mapigano katika maeneo mengine mengi ya mstari wa mbele. Kupungua huku kwa ukubwa wa vita sio muhimu sana, karibu 15-17%, lakini inaweza kuwa uthibitisho wa mwanzo wa uhamishaji wa vikosi na rasilimali kwenda Kursk.

Vyombo vya habari vya kigeni, vikitoa data zao wenyewe, vinaandika kwamba Urusi imeanza kuhamisha hifadhi yake kutoka mstari wa mbele hadi Kursk.

Hasa, jarida la Marekani la Wall Street, likitaja vyanzo kati ya maafisa wa Marekani, linabainisha "kujikusanya tena" kwa vikosi vya Urusi. Lakini WSJ haitoi taarifa ni wanajeshi wangapi ambao Moscow inawaondoa kwenye uwanja wa vita.

Kulingana na mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa Ukraine Konstantin Mashovets, baada ya Wanajeshi wa Ukraine kuanza mashambulizi yao, amri ya Urusi iliunda safu ya kwanza ya wanajeshi kuiondoa, ikiwa na idadi ya vita 10-11. Hii ni takribani watu elfu 3-5.

Mtaalamu wa kijeshi, kanali mstaafu Petr Chernik aliiambia BBC kwamba Urusi lazima ikusanye kundi la wanajeshi wasiopungua 30-40 elfu kuwa na mafanikio katika eneo la Kursk. Kwa kweli, hii ni 10% ya kundi zima la jeshi la Urusi huko Ukraine.

Idadi ya wanajeshi wa Urusi katika eneo la Kursk, mtaalam huyo anasema, inapaswa kuwa mara 3-4 zaidi ya idadi ya wanajeshi wa Ukraine. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Warusi labda watalazimika kushambulia safu za ulinzi zilizowekwa na Waukraine.

Wanajeshi wa Urusi katika mkoa wa Kharkov

Kulingana na Chernik, Kremlin itaweza kuvutia akiba zaidi kutoka kwa kundi la wanajeshi wa Kaskazini, ambalo kwa sasa linapigana katika mkoa wa Kharkov. Nguvu yake inaweza kuwa hadi wanajeshi elfu 75.

Ni sehemu hii ya mstari wa mbele ambayo iko karibu kijiografia na eneo la Kursk.

Mnamo Mei 10, wanajeshi wa Urusi walivuka mpaka na kuingia mkoa wa Kharkiv kuelekea jiji la Vovchansk na kijiji cha Liptsy.

Maendeleo hayo yalifanyika kwa siku mbili au tatu za kwanza.

Tangu wakati huo, mstari wa mbele katika mkoa wa Kharkiv haujabadilika. Wanajeshi wa Urusi bado wanapigana katika sehemu moja tu ya Vovchansk, kaskazini mwa Mto Vovchya, na pia wanajaribu kuikaribia Liptsy kutoka kijiji cha Glubokoe.

Jeshi la Urusi limekuwa likipigania Volchansk bila mafanikio kwa mwezi mmoja sasa

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Vikosi vya Kiukreni hapa sio tu kujilinda, lakini pia kukabiliana na kulazimisha adui kwenda kujihami.

Kwa kuzingatia kwamba vitengo vya kundi moja la askari wa Urusi, ambayo ni "Sever", vinafanya kazi katika mikoa ya Kursk na Kharkov, ni sawa kwamba akiba yake ilikuwa ya kwanza kupelekwa tena Kursk.

Taarifa kuhusu harakati zao zinathibitishwa na kikundi cha uendeshaji-tactical "Kharkov" cha Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine.

"Adui anahamisha vitengo tofauti, vikosi tofauti na rasilimali kutoka kwa mwelekeo wetu hadi eneo lao la Kursk. Lakini bado hatuwezi kusema kwamba hii imekuwa na athari kubwa kwa hali yetu," Vitaliy Sarantsev, msemaji wa jumuiya ya umoja wa eneo, aliiambia Idhaa ya BBC ya Kiukreni.

Anakiri kwamba Moscow haihamishi vitengo vikubwa, kama vile brigedi, kwenda mkoa wa Kursk, isipokuwa ni kwa sehemu tu.

Kwamba hatua hii bado sio muhimu sana inaoneshwa na kuongezeka kwa shughuli za Warusi karibu na Kharkov katika siku za hivi karibuni. Sarantsev aliripoti kwamba mnamo Agosti 13, Warusi walijaribu kutekeleza shambulio kubwa kuelekea kijiji cha Liptsy, lakini Waukraine walizuia shambulio hilo.

Kulingana na Konstantin Mashovets, Urusi ilihamisha vikosi vinne vya bunduki zenye injini kutoka upande wa Kharkov na kikosi kingine kutoka Kupyansk hadi Kursk.

Wanajeshi katika mikoa ya Zaporizhzhya na Kherson

Kamandi ya Ukraine inaripoti kwamba Urusi pia inaondoa baadhi ya wanajeshi kutoka mikoa ya Zaporizhia na Kherson. Kupungua kwa kasi ya mapigano kumerekodiwa hapa wiki iliyopita.

"Tuna habari za kijasusi kuhusu kupelekwa tena kwa vitengo vingine vya vikosi vya uvamizi kutoka kwa mwelekeo wa Dnieper na Zaporizhia," alisema.

Katika mkoa wa Zaporizhia, jeshi la Urusi lilijaribu kusonga mbele karibu na kijiji cha Rabotino, ambacho Vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine viliikomboa mwaka jana.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata hivyo, kulingana na yeye, ni mapema mno kuzungumza kuhusu ushawishi wa hali ilivyo katika eneo la Kursk.

Hatahivyo, kama katika maeneo mengine ya mstari wa mbele, Urusi inajiondoa kwenye uwanja wa vita huko Ukraine sio muundo mzima wa vitengo vyake, lakini sehemu zao za binafsi, pamoja na vikosi vya nyuma na kampuni za vikosi maalumu.

Pokrovsk, Toretsk: Kinachojiri Donetsk

Kufikia katikati ya Agosti, hali ya jeshi la Ukraine ni ngumu karibu na miji ya Donetsk ya Pokrovsk na Toretsk.

Wanajeshi wa Urusi tayari wamekaribia kwanza hadi ndani ya kilomita 15 na, ikiwa kasi itaendelea, wataweza kupita kwenye barabara muhimu za kimkakati kutoka kuelekea mashariki na kusini katika wiki zijazo.

Kuhusu Toretsk, Warusi tayari wanapigana katika viunga vyake, karibu wameteka kijiji jirani cha New York na wako tayari kuanza kushambulia jiji hilo katika siku zijazo.

Wanajeshi wa Ukraine wanaopigana katika maeneo haya wanazungumza juu ya uchovu, hasara kubwa, upangaji wa vitengo na uhaba wa wafanyakazi waliofunzwa kwa ajili ya ulinzi.

Wataalamu, hata hivyo, wanaamini kuwa Urusi, ikipata mafanikio huko Donbass, haitahatarisha kuondoa hata sehemu ya askari wake kutoka sehemu hii ya mbele na kuwahamisha Kursk.

"Hakutakuwa na uondoaji , mkubwa wa wanajeshi kutoka kwa safu ya mapigano, kwani kutekwa kwa Donetsk kunasalia kuwa kipaumbele kwa Warusi," anasema Petr Chernik.

Pamoja, Urusi haina uwezo wa kufanya hivi haraka, angalau kwa sababu ya shida za vifaa.

Imatafsiriwa na Lizzy Masinga