Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatatu: Grealish akubali kujiunga Everton kwa mkopo
Winga wa Uingereza Jack Grealish, 29, amekubali kujiunga na Everton kwa mkopo kutoka Manchester City . (TeamTalk)
Chelsea wanafanya mazungumzo na RB Leipzig kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Xavi Simons, 22, jambo linaloweza kumaanisha kuwa mshambuliajii wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, atarejea katika klabu hiyo ya Ujerumani. (Guardian)
Nicolas Jackson anapendelea kuhamia Newcastle United iwapo mshambuliaji huyo wa Senegal, 24, ataondoka Chelsea wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Telegraph -subscription required)
Newcastle wamewasilisha ombi la kumnunua Yoane Wissa wa Brentford lakini Liverpool wanafuatilia hali hiyo huku wakimuona mshambuliaji huyo wa DRC , 28, kama kiungo mbadala wake iwapo watashindwa kumsajili Isak. (Caught Offside)
Newcastle itasubiri kusuluhisha mustakabali wa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, kabla ya kuamua kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Jackson. (Shirika la habari la PA), nje
Mshambulizi wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, angependelea kujiunga na Juventus kuliko Newcastle baada ya kucheza kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo katika klabu hiyo ya Italia kutoka Paris St-Germain . (teamTalk)
Baada ya kumsajili mshambuliaji wa Slovenia Benjamin Sesko, Manchester United wameelekeza nguvu zao kwenye kuwaondoa winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 21, na mshambuliaji wa Brazil Antony, 25. (Standard)
Sunderland wameulizia kuhusu kumsajili beki wa Uingereza Lloyd Kelly, 26, ambaye amejiunga na Juventus kwa uhamisho wa lazima wa kununua baada ya mkopo wa awali kutoka Newcastle . (Gazzetta dello Sport - in Italian)
AC Milan wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Denmark Rasmus Hojlund, 22, lakini wanataka mkopo wenye chaguo la kumnunua huku Manchester United wangependelea yawepo mauzo ya kudumu. (Sky Sports)
Manchester United wanafikiria kumsajili mchezaji huru Dominic Calvert-Lewin baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza, 28, kuondoka Everton mwishoni mwa msimu uliopita. (Caught Offside)
Nottingham Forest wametoa ofa kwa kiungo wa kati wa Monaco mwenye umri wa miaka 21 Soungoutou Magassa. (L'Equipe - in French)
Kostas Tsimikas anakaribia kuondoka Liverpool baada ya kuachwa nje ya kikosi chao cha Ngao ya Jamii, (Community Shield squad,), huku Nottingham Forest ikimtaka beki huyo wa kushoto wa Ugiriki mwenye umri wa miaka 29. (Echo)
Enzo Fernandez hataondoka Chelsea msimu huu wa joto licha ya ripoti nchini Uhispania zikimuhusisha kiungo huyo wa kati wa Argentina, 24, na kuhamia Paris St-Germain . (Fabrizio Romano)
Besiktas na Fenerbahce huenda wakamnunua Jonathan Rowe wa Marseille , huku Rennes na Atalanta pia wakihusishwa na winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22. (L'Equipe - in French)
Mshambulizi wa Jamaica Michail Antonio, 35, anasema anazungumza na vilabu vya Uingereza na nje ya nchi baada ya kuondoka West Ham mwishoni mwa msimu uliopita. (Sport)
Klabu ya Saudi Pro League Al-Nassr imefikia makubaliano na winga wa Ufaransa Kingsley Coman, 29, kuhusu kuhama kutoka Bayern Munich . (Bild - kin Germany)
Kiungo wa kati wa Mali Abdoulaye Doucoure, 32, amejiunga na klabu mpya ya Saudia iliyopandishwa daraja ya Neom kama mchezaji huru baada ya kuondoka Everton . (L'Equipe - in French)
End of Unaweza pia kusoma:
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi