Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Mustakabali wa Rodri unaihusu Man City

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester City wana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kumpoteza nahodha wa Uhispania Rodri, 29, kwani bado hajaamua kama aongeze mkataba wake zaidi ya 2027, huku Real Madrid wakitafuta kusaini kiungo wa kati msimu huu. (AS - In Spanish)

Everton wamefanya mazungumzo zaidi juu ya kumsajili winga wa Uingereza Jack Grealish, 29, kwa uhamisho wa mkopo kutoka Manchester City , ambao unaweza kuwagharimu The Toffees £12m. (Time -Subscription required)

Chelsea wameongeza mazungumzo na Manchester United kuhusu kumnunua winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 21 Alejandro Garnacho. (Athletic)

Newcastle United wamekubali mkataba wa kumsaini beki wa AC Milan raia wa Ujerumani Malick Thiaw, 24, kwa mkataba wa thamani ya euro 40m (£34.6m). (Mail)

Mshambulizi wa zamani wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 28, amemuacha muwakilishi wake na atafanya mazungumzo yake mwenyewe huku akitumai kujiunga na Manchester United baada ya kuondoka Everton mwishoni mwa msimu uliopita. (Sun).

Brentford wamefanya mazungumzo ya awali na Bournemouth kuhusu kumsajili winga wa Burkina Faso Dango Ouattara, 23. (Sky Sports).

Liverpool ndio wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili mlinzi wa Uingereza Marc Guehi iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ataondoka Crystal Palace msimu huu wa joto. (Telegraph - subscription required)

Newcastle United wamemwambia mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak kwamba hatauzwa msimu huu wa joto na hataruhusiwa kujiunga na Liverpool, ambao wamekataliwa ofa ya pauni milioni 110 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph - subscription required)

Chelsea bado wapo kwenye mazungumzo kuhusu mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 22. (Sky Sports)

Dunderland iliyopanda daraja mpya iko mbioni kukubali mkataba wa pauni milioni 10 kwa mlinzi wa Getafe wa Paraguay Omar Alderrete, 28. (Sun)

Mshambulizi wa Nantes Mfaransa Matthis Abline mwenye umri wa miaka 22 anavutiwa na Paris FC , Eintracht Frankfurt na Wolves . (Fabrizio Romano)

Al Nassr wanaandaa dau la takriban euro 30m (£26m) kumnunua winga wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 29 Kingsley Coman. (Florian Plettenberg)

AC Milan wako tayari kumenyana na wapinzani wa jiji la Inter , pamoja na Liverpool , kumnunua beki wa kati wa Parma , Giovanni Leoni, 18 . (Corriere dello Sport - In Italian)