Mambo gani ya kuyaepuka katika mitandao ya kijamii wakati wa Ramadhan?

n

Chanzo cha picha, Getty images

    • Author, Ahmad Bawage
    • Nafasi, BBC

Katika miaka kumi iliyopita, dunia imebadilika hasa katika nyanja ya teknolojia, maendeleo hayo yamewafanya watu wengi duniani kuwa na simu za kisasa zinazoweza kupata intaneti.

Katika ulimwengu wa sasa, matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa sehemu ya maisha ya kila siku.

Mitandao hii ya kijamii imekuwa njia ambayo kwayo tunaendesha shughuli nyingi za maisha na matumizi hayo pia huathiri maisha yetu.

Kutokana na athari hizo ipo haja ya kuamua jinsi unavyopaswa kutumia mitandao wakati wa mfungo wa Ramadhani ili kuepuka kumuasi Mungu.

Mambo usiyopaswa kuyafanya

Sheikh Abdullahi Usman Gadon Kaya, ni mwalimu wa Kiislamu katika jimbo la Kano nchini Nigeria, katika mahojiano yake na BBC alieleza namna ambavyo Waislamu wanapaswa kutumia mitandao ya kijamii wakati wa Ramadhani.

Sheikh huyo anasema maana ya swaumu ni kujiepusha na jambo lolote linaloweza kumpeleka mtu katika dhambi na kumkufuru Mungu.

“Hata kama mtu huyo alikuwa akijizuia na mitandao kabla ya kufunga, anapaswa kufanya hivyo zaidi wakati wa mfungo ili asije akaingia kwenye kufunguza,” anasema Gadon Kaya.

Miongoni mwa mambo ambayo Waislamu waepuke wakati wa mfungo ni pamoja na:

  • Kutazama muziki na kucheza
  • Kuangalia picha za uchi
  • Kutoa maoni yasiyo na maana
  • Usambazaji na uchapishaji wa habari za uwongo
  • Kuangalia sinema na picha
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sheikh Abdullahi Gadon Kaya anasema, "inasikitisha ukienda YouTube na kuona mambo yanayofanywa, Muislamu aliyefunga hapaswi kuyaona.

“Mambo yanayofanywa kwenye TikTok, inabidi tuseme Inna lillahi wa inna ilaihir rajiun, mambo mengine hata ukiona yatakufungulia saumu,” anasema mwalimu huyo.

Anasema waliofunga waondoe mikono yao kwenye TikTok, Instagram na YouTube ikiwa sio jambo ambalo litawanufaisha kidini, na ikiwa wanataka funga iwaletee thawabu mbele ya Allah SWT.

Sheikh Abdullahi anaeleza kuwa swaumu ni wakati wa kukizuia kinywa, masikio, macho, pua na mambo ya haramu – sanjari na kujizuia na shughuli za kula na kunywa.

"Sasa Alhamdulilah wanazuoni wanajaribu. Katika mitandao yote hii, kuna khutba na visomo vya Qur-aan, sala, tarawi, tahajjud na tafsiri kwa lugha zote. Waislamu waache kutazama mambo mabaya na watazame mambo mema," anasema Sheikh Kaya.

Waislamu wakitumia TikTok na watazame mahubiri, na kuhakikisha kwamba popote waendako, wanatazama mambo mazuri na sio mabaya.

“Mambo hayo yakifanyika yatasaidia kutunza na kulinda heshima ya mfungo.’’

Mambo unayotakiwa kufanya

vb

Chanzo cha picha, ABDULLAHI GADON KAYA/FB

Maelezo ya picha, Sheikh Abdullahi Gadon Kaya anasema ni bahati mbaya ukienda YouTube na kuona mambo yanayofanywa, Muislamu aliyefunga hapaswi kuyaangalia.

Sheikh Kaya anasema mitandao ya kisasa ya mawasiliano inapoteza muda kwa kuwazuia Waislamu kusoma Qur-aan, kufanya dhikri na kusikiliza mawaidha.

Kwa hivyo, kuna mambo ambayo Waislamu wanapaswa kufanya wakati wa mfungo ili kupata thawabu nyingi zaidi katika mwezi mtukufu.

  • Kusoma Quran
  • Kusikiliza Quran
  • Angalia mambo mazuri
  • Kutoa ujumbe nzuri kwa Waislamu

Mwalimu huyo wa dini ya kiislamu katika jimbo la Kano amesema vyombo vya habari navyo vina mchango wao katika kipindi hiki cha mfungo hasa kwa kuwaita wanazuoni kutoa hotuba au fatwa juu ya mambo yanayofungua saumu.

Vilevile kutoa maelekezo ya swala ya Tarawehe na Tahajjud, na programu za umuhimu wa kuwalisha masikini.

Pia alisema serikali inapaswa kuwarahisishia watu katika shughuli zao za biashara na kuwasaidia watu masikini, na kuwataka wenye fedha kuwasaidia wasiojiweza.