Ramadhan: Ni chakula kipi unachofaa kula na kipi cha kuepuka mwezi wa mfungo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mamilioni ya Waislamu duniani kote wanakaribia kuanza mfungo wa Ramadhani moja ya miezi mitakatifu zaidi katika kalenda ya Kiislamu.
Inaashiria wakati Koran, kitabu kitakatifu cha Uislamu, kilifunuliwa kwa Mtume Muhammad.
Kipindi cha kufunga huzingatiwa katika mwezi mzima na ni moja ya nguzo tano za Uislamu, jukumu la lazima ambayo Waislamu wote wanapaswa kujaribu kutekeleza.
Wakati wa Ramadhani, Waislamu hula chakula cha asubuhi kabla ya alfajiri, kinachojulikana kama suhoor au sehri.
Hawali au kunywa chochote - ikiwa ni pamoja na maji - mpaka wafungue mfungo wao baada ya jua kuzama na chakula cha jioni, kinachoitwa iftar au fitoor.
Ni watu tu ambao wana afya njema ndio wanaotarajiwa kufunga na wale ambao ni wagonjwa, watoto ambao hawajabalehe, wajawazito, wanaonyonyesha au wanawake walio katika hedhi na wasafiri wanachukuliwa kuwa wamesamehewa.
Baadhi ya watu wanaweza kuhisi kufunga ni rahisi lakini kwa wengine inaweza kuwa changamoto na njaa inaweza kupata wawapo kazini na shughuli nyingine za kila siku.
Kwa hiyo, ni aina gani ya chakula unahitaji kula ili kikusaidie kupata kupitia mwezi wa Ramadhani?
Nini cha kula wakati wa suhoor?

Chanzo cha picha, Getty Images
Suhoor ni maandalizi funga ya siku na kula chakula sahihi ni muhimu ili kupunguza tamaa baadaye mchana.
"Wakati wa Ramadhani, ili kukidhi kiwango cha nishati na virutubisho ambavyo mwili wako unahitaji wakati wa mchana, unapaswa kula vyakula vyenye protini, wanga, vitamini, na madini, na unapaswa kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha," anasema mtaalamu wa lishe Ismet Tamer.
Anashauri kula kifungua kinywa lkwa chakula chenye , afya na cha kushibisha.
"Kabla ya jua kuzama, unaweza kula bidhaa za maziwa na mboga safi kama jibini, mayai, nyanya, na matango. Zaidi ya hayo, unaweza kufurahia supu, mboga zilizopikwa katika mafuta ya mzeituni
Ni nini cha kula wakati wa iftar?
Wakati wa kufungua mfungo wa siku kwa ujumla inashauriwa unywe maji mengi na vyakula vyenye sukari ya asili kwa aajili ya nishati ya mwili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Maji na tende, ni njia nzuri ya kufungua mfungo wako wa siku kabla ya kula chakula," anasema mtaalamu wa lishe Bridget Benelam. "Vinakupa nguvu na kukuepusha na upungufu wa maji mwilini."
"Supu ni bora pia kufungua mfungo, kwani itakuwa na vitu kama maharagwe, kunde, dengu na mboga - vitu vingi ambavyo vitakupa virutubisho na nyuzi bila kupakia kupita kiasi," anasema.
"Baada ya siku ndefu ya kutokula usingependa kuanza na kitu kizito kwa sababu hiyo labda itakufanya uhisi uchovu, uvivu na usiye na afya."
Baada ya kufungua , chakula cha iftar hutofautiana kati ya tamaduni na mila tofauti, lakini kwa ujumla hujumuisha vyakula kadhaa.
Inashauriwa kuhakikisha vyakula unavyokula kwenye iftar vinatoa uwiano wa vyakula vyenye wanga, ikiwa ni pamoja na mboga za nyuzinyuzi na matunda, maziwa na vyakula vyenye protini kama nyama, samaki, mayai na maharagwe. Inashauriwa pia kuzuia hamu ya kula chakula na vyakula vingi vyenye sukari dkama desserts nyingi tamu ambazo zinaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito wa mwili.
Baadhi ya wataalamu wa lishe pia wanashauri kugawanya chakula cha iftar mbili, badala ya kula mlo mmoja mkubwa, kwani hii itasaidia kudhibiti kupanga haraka kwa viwango vya juu vya sukari ya damu, pamoja na kupunguza hatari ya mwili kushindwa kukisaga.
Je, kufunga ni jambo zuri kwa afya yako?
Kufunga, kwa ujumla, imeonyeshwa kuwa na faida za afya, na kufunga kwa vipindi imeonekana kuwa njia maarufu ya kupoteza uzito.
Badala ya kuzingatia nini cha kula, kufunga kwa vipindi kunaelezea wakati wa kula. Kunahusisha kufunga kwa idadi fulani ya masaa kila siku.
Wazo ni kwamba mara tu mwili wako umetumia maduka yake ya sukari, huanza kuchoma mafuta, na uzito hupungua - mchakato unaojulikana kama metabolic switching
Uchunguzi umeonyesha kuwa faida za afya ambazo zinaweza kupatikana kupitia kufunga kwa vipindi ni pamoja na kushuka kwa shinikizo la damu la chini na cholesterol, kuvimba mwilini kwa jumla, na kupunguza hatari ya aina ya kisukari cha 2.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kufunga kwa Ramadhani kunashirikisha karibu sifa zote za kufunga kwa muda.
Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika Jarida la Marekani la Lishe na Kliniki uliuhusisha kufunga kwa Ramadhani kwa mabadiliko mazuri ya kimetaboliki na kupunguza hatari ya ugonjwa sugu.
Matokeo ya utafiti huo yalibaini kuwa mfungo wa Ramadhani ulipunguza kwa kiasi kikubwa hatari za saratani ya mapafu, utumbo na matiti.
Mtaalamu wa lishe Bridget Benelam anasema kuwa kwa ujumla watu huwa wanapoteza uzito wa kilo moja wakati wa Ramadhani, lakini pia wana neno la tahadhari: unaweza kupata uzito ikiwa utaizidisha chakula kwenye iftar.
"Kama binadamu tuna tabia ya asili ya kula zaidi. Aina zaidi tunayopewa zaidi tunayokula, na bila shaka, meza kubwa ya iftar na sahani nyingi ni mfano mzuri wa hilo, "anasema.
"Huna haja ya kula kila kitu unachopewa. Kwa hivyo chagua na ule polepole."
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












