Mzozo wa Ukraine: Waziri wa Ulinzi wa Uingereza asema Ukraine inaweza kutumia silaha zake kushambulia Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa ulinzi wa Uingereza amesema itakubalika kwa vikosi vya Ukraine kutumia silaha za Magharibi kushambulia maeneo ya kijeshi yanayolengwa katika ardhi ya Urusi,
James Heappey alisema mashambulizi ya kuharibu njia za usambazaji ni sehemu "halali" kabisa ya vita.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ameishutumu Nato kwa kuhusika katika vita hiyo na kusema silaha zitakazowasilishwa na nchi za Magharibi kwa Ukraine zitakuwa shabaha za haki.
Uingereza ilitangaza kuwa itaipa Ukraine idadi ndogo ya magari ya kuzuia mashambulizi ya anga.
Nchi za Magharibi zimetoa msaada wa mamia ya mamilioni ya pauni za kijeshi kwa Ukraine tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake mwezi Februari na maafisa wa Nato na Umoja wa Ulaya wanakutana nchini Ujerumani kujadili msaada zaidi wa kijeshi.
Haya yanajiri huku Urusi ikiwa imeelekeza nguvu zake katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine, huku Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ikiripoti kuwa mji wa Kreminna, huko Luhansk, umeanguka.
Urusi imeishutumu Ukraine kwa kushambulia maeneo ndani ya ardhi yake, ikiwa ni pamoja na ghala la mafuta huko Belgorod, lakini vikosi vya Ukraine havijathibitisha mashambulio yeyote.
Alipoulizwa kuhusu hili katika kipindi cha BBC Radio 4, Heappey alisema: "Swali ni je, inakubalika kwa Waukraine kutumia silaha zetu dhidi ya meoneo halali ya kijeshi yanayolengwa ya Urusi?
"Kwanza, ni Waukraine wanaochukua uamuzi wa shabaha gani, sio watu wanaotengeneza au kuuza nje vifaa hivi mara ya kwanza. Na pili, ni halali kabisa kufuata shabaha katika kiini cha wapinzani wako ili kuvuruga usafirishaji wao na laini za usambazaji. "
Waziri wa vikosi vya jeshi ameongeza kuwa pia ni sehemu "halali kabisa" ya vita kwa vikosi vya Urusi kulenga shabaha magharibi mwa Ukraine ili kuvuruga laini za usambazaji wa Ukraine mradi tu wasilenge raia - "ambapo kwa bahati mbaya hawajazingatia sana mpaka kufikia sasa".

Chanzo cha picha, PA Media

Ukraine inapigana vita vilivyopo na Urusi kwa hivyo haishangazi kwamba vikosi vya Ukraine vinapaswa kulenga mstari wa usambazaji kwenye mpaka wa Urusi.
Vile vile haishangazi mataifa ya Magharibi yametulia kwamba baadhi ya silaha zao hutumiwa katika mashambulizi kama hiyo.
Kinachovutia kuhusu matamshi ya James Heappey ni ukweli wao.
Katika migogoro mingine, kama vile Yemen, mawaziri wa Uingereza huwa na wasiwasi kuhusu matumizi ya silaha za Uingereza.
Katika hatua nyingine, Waziri wa ulinzi anaweka wazi kwamba Mara nyingi huzungumza zaidi kama mwanajeshi wa zamani kuliko mwanasiasa.
Lakini matamshi yake yanaakisi ushiriki wa Nato katika mzozo huu.
Silaha zinazotolewa na mataifa ya magharibi zinazidi kuwa kubwa na kuwa na nguvu zaidi.
Ni jambo moja kuipatia Ukraine silaha aina ya bazooka ya masafa mafupi za kupambana na vifar. Mwingine kuwapa ndege zisizo na rubani na silaha zinazoweza kuvuka mipaka.
Mstari kati ya kuilinda Ukraine na kuishambulia Urusi unazidi kuwa finyu.

Chanzo cha picha, Reuters

Siku ya Jumatatu Bw Lavrov alidai nchi za Magharibi "zinamwaga mafuta kwenye moto" kwa kuipatia Ukraine nguvu ya moto na kuonya mara kwa mara kwamba mzozo huo unaweza kusababisha vita vya tatu vya dunia.
Lakini Bw Heappey alisema nchi za Magharibi zimekuwa makini sana kuhusu kuwapatia silaha Ukraine kitendo ambacho sio "juhudi za Nato".
Alisema Urusi imekuwa ikisema ilikuwa katika mzozo na Nato kabla ya vita kuanza - "ni upuuzi na [Bwana] Lavrov anajua".
Bw Heappey aliongeza kuwa anafikiri uwezekano wa vita vya nyuklia ni "mdogo sana", na hakuna anayetaka matokeo kama hayo kwenye mzozo huo.

Kwa miezi kadhaa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa akiomba washirika wa Magharibi silaha zaidi ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi.
Siku ya Jumatatu, Waziri wa Ulinzi Ben Wallace alitangaza kuwa Uingereza itatoa zawadi ya idadi ndogo ya magari ya Stormer yaliyowekwa kurushia makombora ya kutungulia ndege ya Starstreak ili kuwapa vikosi vya Ukraine "uwezo ulioimarishwa wa masafa mafupi wa kuzuia mashambulizi ya anga mchana na usiku".
Pia aliliambia Bunge kuwa takriban wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa tangu Urusi ilipofanya uvamizi kamili wa Ukraine, huku magari yake ya kivita 2,000 yakiwa yameharibiwa au kutekwa.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin ameongoza mkutano wa mawaziri wa ulinzi katika kambi ya Jeshi la Wanahewa la Marekani huko Ramstein nchini Ujerumani siku ya Jumanne.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine















