Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 19.10.2021: Sterling, Salah, Icardi, Aguero, Mbappe, Isak, Solskjaer

Raheem Sterling

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City inataka euro 80m kwa ajili ya mshambuliaji wake mwenye miaka 26 Raheem Sterling, ambaye anatakiwa na Barcelona. (Marca)

Meneja wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez, kocha wa Rangers Steven Gerrard na kocha wa Villarreal Unai Emery wanatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa kumrithi kocha Steve Bruce wa Newcastle United. (Times - subscription required)

Manchester United itachuana na Manchester City katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Real Sociedad na Sweden Alexander Isak, 22. (Fichajes - in Spanish)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 29, anataka mshahara wa karibu £400,000 kwa wiki ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Anfield. (Telegraph)

Liverpool imetaarifiwa na Lazio kwamba bei ya kiungo Mserbia Sergej Milinkovic-Savic, 26, inaanzia £67m. (Calciomercato - in Italian)

Paris St-Germain huenda ikamtoa mshambuliaji wake Mauro Icardi, 28, kubadilishana na mshambuliaji muargentina Sergio Aguero, 33 aliyejiunga Barcelonakitokea Manchester City. (El Nacional)

Leeds United na Newcastle United vyote vinamtaka kiungo wa zamani wa Chelse na England Ross Barkley, 27 ambaye pia anawaniwa na Burnley. (90 Min)

Arsenal na Leicester City vinamfuatilia winga wa Southampton na Norway Mohamed Elyounoussi baada ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 kuonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu. (Sun)

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer hajafurahishwa na klabu hiyo kushindwa kusajili kiungo katika dirisha lililopita la usajili. (Manchester Evening News)

gg

Chanzo cha picha, Getty Images

Hamasa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo iko chini baada ya kipigo dhidi ya Leicester City kukiacha kikosi hocho cha Solskjaer kutoshinda mechi yoyote kati ya tatu zilizopota za ligi kuu. (Times - subscription required)

Mshambuliaji Mfaransa Kylian Mbappe, 22, ambaye anawaniwa na Real Madrid, amegusia kwamba ana furaha PSG. (Marca)

Everton inamfuatilia mlinzi wa kushoto wa Morecambe ya League One Connor Pye baada ya kinda huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 17 kuwavutia wasaka vipaji wa klabu hiyo. (Football Insider)