Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 18.10.2021: Ole, Pogba, Barkley, Bale, Lewandowski, Haaland, Mbappe

Erling Braut Halaand

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwaka 2022 klabu ya Paris St-Germain watatupa ndoano yao kwa mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 33, au mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, kama mbadala wa mfaransa Kylian Mbappe. (Le 10 Sport)

Mazungumzo ya mkataba mpya wa shambuliaji wa Barcelona na Hispania Ansu Fati yamekwama baada ya wakala wa kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 Jorge Mendes kutaka mchezaji wake apewe mkataba wa miaka na kukataa kuwekwa kwa kipengele cha mkataba kinachomfunga mchezaji huyo kwa thamani ya £844m. (El Nacional - in Catalan)

Ole

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer hatatimuliwa licha ya Mnorway huyo kushinda mechi 4 tu kati ya 8 za ligi kuu England msimu huu. (The Athletic)

Barcelona haitamshawishi Paul Pogba wa Manchester United wakati mkataba wa kiungo huyo mfaransa utakapomalizika mwishoni mwa msimu kwa kuwa klabu hiyo ya Hispania haitaweza kumudu mshahara wa nyota huyo mwenye miaka 28 (AS)

Kiungo wa zamani wa Chelsea na England Ross Barkley, 27, anawaniwa kusajiliwa na klabu ya Burnley katika dirisha la mwezi Januari. (Sun)

Bale

Chanzo cha picha, Gareth Everett/Huw Evans Agency

Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 32, atapokea ofa ya usajili kutoka Arsenal katika dirisha la mwezi Januari. (Defensa Central - in Spanish)

Wakala wa mlinzi wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, Mino Raiola amezungumza na klabu za Manchester City na Chelsea kwa matumaini ya kuchagiza uhamisho wa mlinzi huyo wa kati mwenye umri wa miaka 22. (Calciomercato - in Italian)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkurugenzi wa michezo wa Liverpool Michael Edwards anawaniwa na Real Madrid ili kuisaidia klabu hiyo ya Hispania kwenye masuala ya uhamisho wa wachezaji. (Sun)

Klabu za Tottenham Hotspur na Newcastle United zinamuania mshambuliaji wa Fiorentina na Serbia Dusan Vlahovic, 21. (Sun)

Aston Villa imemuweka katika orodha ya wachezaji inayowataka mlinzi wa kushoto wa Bologna Aaron Hickey baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye Serie A form, lakini mlinzi huyo Mscotland mwenye umri wa 19 hana haraka ya kuondoka Italia. (Sun)