Harar - mji wa Ethiopia unaojulikana kama 'Mecca ya Afrika'

Harar street scene

Mji wa Harar uliopo Ethiopia unaotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, umekuwepo kwa Zaidi ya miaka 1,000 mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza, anaeleza upekee wa urithi uliopo hapo.

Usiku unapoingia katika jiji la kale la Harar, na ninashuhudia mambo ya kushangaza, ingawa kwa wenyeji ni kawaida.

Kijana mmoja akiwa amebeba vipande vya nyama kwenye vijiti , na kuweka kijiti mdomoni mwake na kisha anawalisha fisi kadhaa ambao hutoka gizani, macho yao yaking'aa wakati wanaingia kwenye mwanga.

Mbinu hiyo ikitumika kuwavutia watalii.

"Nafanya hivi kwasababu napenda wanyama," Biniam Ashenafi anaeleza. Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 ni miongoni mwa wakazi wanaojitolea kuwalisha wanyama.

"Hatuwaiti fisi. Huwa tunawaita mapadre wadogo.Kila mwaka katika kalenda ya Urabuni, huwa tunauji wa kuwapa katika pembezoni mwa kona nne za mji.

"Kama watakuja na kukubali kile tunachowapa, ina maanisha kuwa siku zijazo zitakuwa nzuri. Kama wakikataa, itakuwa ishara mbaya."

Kwa karne kadhaa, watu wa Harar wamekuwa wakiishi karibu na fisi kwa karibu sana - mnyama ambaye ni miongoni mwa wanyama hatari sana duniani.

line

Historia ya Harar:

  • Karne ya 7: Baadhi ya maeneo ya Kikristo yalianza kukubali Uislamu
  • 1007: Mji wa Harar ulianzishwa
  • Karne ya 16: Mji wa kifalme wa Harari , kituo kikuu cha biashara na kujifunza Kiislamu , ilitajwa kuwa waislamu walihama kutoka Uarabuni
  • 1887: Ikawa sehemu ya Ethiopia
  • 2006: Ulitajwa kuwa mji wa urithi wa dunia na Unesco
line

Kuta za mji huo zilizojengwa kati ya Karne ya 13 na 16, ambazo hata zina mashimo madogo ndani yake ili kuruhusu fisi kuingia mjini usiku.

Suala la kulisha fisii kila siku ni mfano mmoja wa kuonesha upekee wa mji huo wa urithi.

"Huu ni miongoni mwa utamaduni wa kale duniani," mwanahistoria wa eneo hilo Abdulswamad Idris ananiambia.

"Baadhi ya misikiti unayoiona hapa , ilijengwa karne ya 10."

Waliobadilisha dini na kuwa waislamu

Harar ni mji ambao unaenda na majina mengi , kutoka kwa mji mtakatifu mpaka mji wa utalii, wakati baadhi ya Waethiopia wanautaja kuwa mji wa nne kwa utakatifu baada ya Mecca, Jerusalem na Medina, ingawa wazo hilo halijasemwa na waislamu wengi.

Umekuwa mji wa amani , jina ambalo limewekewa saini kubwa wakati ninapoingia mjini.

Sign saying City of Peace
map

Maelfu ya watu kutoka nchini humo na hata watalii wa kimataifa, wamekusanyika kwa ajili ya sherehe za Harar Jugol -jinarasmi za mji huo wa kale ambao ulikuwa unatimia miaka 1,010.

"Unataka kuanza kutalii kuanzia wapi ?" aliuliza muongozaji wangu , Dagnachew.

"Msikiti kwanza," nilijibu kwa haraka.

"Lakini upi huo?" alijibu kwa kucheka. "Maana ipo kama 100 hivi."

Harar ni sawa na Mecca ya Afrika, na wakazi wa hapa wanadai kuwa wakazi wa eneo hili walikubali Uislamu miaka nane kabla ya watu katika mji mtakatifu wa Medina katika peninsula ya Uarabuni..

People walk in front of the Jimma Mosque, the largest mosque in Harar, especially reserved for Friday prayers, on August 3, 2014

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jimma ndio msikiti mkubwa zaidi Harar

Wafuasi wa mtume Muhammad walisemekana kuwa walikimbia mateso huko Mecca katika miaka ya 600 AD na kupata eneo la kifalme la Axum, eneo linalojumuisha Ethiopia ya leo na Eritrea.

"Harar na watu wa Harlaa wapo miaka 7,000 . Lakini mji wenyewe ulianzishwa muongo uliopita," alisema bwana Abdulswamad.

Zaidi ya miaka 40 wakati wa karne ya 16, mji mkubwa wa Harari , kabla ya kuwa sehemu ya Ethiopia mwaka 1887.

'Hisia ya kifamilia'

Leo katika mji wa Harari ambao ni - mji mdogo zaidi wa Ethiopia.

Mwaka 2006, Harar ulitajwa na Unesco kuwa eneo la Urithi wa dunia kwa kuainisha upekee wake na jinsi majengo yake yalivyojengwa, ambayo yameangazia Uafrika na utamaduni wa mwafrika.

Nikiwa natembea katika mitaa mbalimbali ya mji huo mkongwe , Ninaona kile kinachowavutia watu kuja katika eneo hili.

Ni kidogo sana kimebadilika katika miaka.

Harar alleyway

Nikipita kona hii, nakutana na milio ya mashine kadhaa za kushona.

"Mtaa huu ni maarufu sana kwa utengenezaji wa nguo ," muongozaji wangu Dagnachew anasema, huku akinyoosha mkono kwa gauni lenye rangi za kung'aa na shati ambalo limetundikwa katika maduka madogo.

Kivutio kingine ni makumbusho hiyo ambayo iilanzishwa karne ya 19 na mshairi wa Ufaransa Arthur Rimbaud, ambaye aliwahi kuishi na kufanya kazi katika mji wa kibiashara wa Harar.

Picha ya rangi nyeusi na nyeupe - ya bwana Rimbaud mwenyewe ilipigwa miaka ya 1900.

Picha za wageni na viongozi wa mji huo na ukumbusho wa picha za masoko na makanisa.

Exhibition of ancient Harar

Miongoni mwa wageni wanaotembelea hapo mara kwa mara ni Ethiopia wanaishi ughaibuni.

"Sidhani kama kuna watu wengine duniani wanapenda ," alisema Sayo Addous, ambaye alizaliwa Harar na sasa anaishi Uingereza.

"Ina uhusiano mkubwa sana na familia, hisia ambazo hawazipati katika karne hii ya 21 ."

Unesco inautangaza mji huo kuwa wa kipekee wenye mifano iliyohifadhiwa kihistoria na mila za watu wa mji huo, vitambaa vya mjini, na utajiri mkubwa wa utamaduni wa kiislamu kwa wakati wa sasa.

Hii ndio sababu inafanya mji huu kuwa wa kipekee kwa kujivunia historia yao ya muda mrefu, huku wakazi wa hapo wanaamini kuwa kuna mengi ya kuyatoa kwa Afrika nzima kama ishara ya utamaduni na uhifadhi wa kihistoria.