Ethiopia :Lifahamu taifa ambalo mwaka una miezi 13

A woman blows a trumpet ahead a procession to mark the victory at the Battle of Adwa - March 2021, Addis Ababa, Ethiopia

Chanzo cha picha, Getty Images

Taifa la Ethiopia limekaribisha mwaka mpya hivi karibuni, licha ya kuwepo kwa baadhi ya madhila ya vita na njaa hasa upande wa mashariki wa taifa hili. Fahamu zaidi kuhusu kalenda ya mwaka wa kipekee wa Ethiopia kama urithi wa nchi hiyo.

1) Mwaka ambao una miezi 13

Sio jambo hilo tu la miezi, mwaka huu wa Ethiopia upo miaka saba nyuma na miezi nane ukilinganishwa na kalenda inayotumika ulimwenguni, Jumamosi mwezi huu waliukaribisha mwaka 2014.

Hii inatokana na kwamba wanahesabu mwaka aliozaliwa Yesu kristu tofauti, Kanisa katoliki lilipokuwa limefanyia marekebisho mwaka wa kuzaliwa kristo miaka ya 500 AD, Kanisa la Orthodox halikufanya marekebisha upande wao.

People from the Oromo community celebrate Irreecha in Bishoftu, Ethiopia - 2017

Chanzo cha picha, AFP

Mwaka wao mpya huadhimishwa kila ifikapo Septemba 11 na siku nyingine huangukia tarehe 12 mwezi huo huo.

Tofauti na watoto wanaokua mahali pengine duniani, kuna haja pia kwa vijana wa Ethiopia kujifunza kuwa kuna siku ngapi katika mwezi.

Kwa upande wa Ethiopia ni rahisi, katika miezi 12 kuna siku 30 kila mwezi na mwezi wa 13- Mwezi wa mwisho ukiwa na siku tano mpaka saba tu inategemea zaidi na inapoangukia.

Muda nao uhesabiwa tofauti

Muda unahesabiwa tofauti -ambapo siku ikiwa imegawanywa sehemu mbili za masaa 12 kuanzia 06:00, ambayo inafanya mchana na usiku wa manane saa sita kwa wakati wa Ethiopia.

Kwahiyo ukipanga kikao na mtu aliyeko Addis Ababa saa nne asubihi kwaajili ya kahawa-usishangae ukamuona huyo mtu akitokea saa sita.

2)Nchi pekee barani Afrika ambayo haijatawaliwa

Italia ilijaribu kuivamia Ethiopia au Abyssinia kama ilivyokuwa ikitambulika katika miaka ya 1895, kipindi ambacho nchi nyingi za Afrika zilianza kugawaiwa kwenye makoloni, lakini kwa upande wa nchi hiyo Italia ilipata shida kuimiliki.

Italia ilifanikiwa kuweka koloni lake nchi jirani ya Eritrea baada ya kampuni kubwa ya kiitalia kununua bandari ya Assab.

Yote yalianza kujitokeza mwaka 1889 pale tu kilipotokea kifo cha Mfalme wa Ethiopia Yohannes wa nne, iliwapa fursa Italia kuingia katika pwani.

Horsemen at a parade to mark the anniversary of the Battle of Adwa in Addis Ababa, Ethiopia - March 2021

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini miaka michache baadaye wakati Italia ikaanza kushinikiza kuingia Ethiopia, ilishindwa mapema kwenye Vita vya Adwa.

Vikosi vinne vya askari wa Italia vilihangaishwa kwa saa Machi 1,1896 na Waethiopia waliokuwa wakimtii Mfalme Menelik II.

Italia ililazimishwa kusaini mkataba wa kuitambua Ethiopia kama nchi huru-ila miaka kadhaa baadaye kiongozi wa kifashisti Benito Mussolini alitupilia mbali makubaliano hayo.

Mmoja wa warithi wa Menelik, Mtukufu Hale Selassie, alipigilia msumari wa uhuru wa taifa lake baada ya kuyaunganisha mataifa ya Afrika kupitia uanzishwaji wa Umoja wa Afrika ambapo makao makuu yake yapo katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

People marching with Ethiopia's flag on flag day

Chanzo cha picha, Getty Images

"Uhuru wetu hauna maana isipokuwa Waafrika wote wako huru," Selassie alisema wakati wa uzinduzi wa OAU mnamo 1963, wakati ambapo bara kubwa bado lilikuwa likitawaliwa na mamlaka za Ulaya.

Aliwaalika wale wanaoongoza vita dhidi ya ukoloni na kuendesha mafunzo - pamoja na Nelson Mandela wa Afrika Kusini - ambaye alipewa pasipoti ya Ethiopia, ambayo ilimruhusu kuzunguka Afrika nzima mwaka 1962.

3) Marasta wanamuabudu Mfalme Haile Selassie

Jambo hili lilianza mwaka 1920 baada ya kunukuliwa kwa kiongozi mashuhuri wa Jamaica Marcus Garvey, ambaye alikuwa nyuma ya harakati ya Kurudi Afrika:

"Angalia Afrika, wakati mfalme mweusi atakapotawazwa taji, kwani siku ya ukombozi imekaribia."

Muongo mmoja baadaye, Ras Tafari (au Chifu Tafari) mwenye umri wa miaka 38 alipotawazwa Haile Selassie wa Ethiopia, wananchi wengi nchini Jamaica waliona hii kama unabii umetimia na harakati ya Rastafari ilizaliwa.

A mural depicting Ethiopian Emperor Haile Selassie I, Jamaican Reggae legend Bob Marley and his sons at grounds of the Bob Marley Museum in Kingston, Jamaica, on May 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Haile Selassie (kushoto)

Mwanamuziki maarufu wa Rege Bob Marley alikuwa mahiri kueneza imani ya kirasta, na mashairi yake yalinukuliwa na Mfalme kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mwaka 1963 akihubiri zaidi amani duniani.

Crowds at the airport to welcome Haile Selassie in 1966

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maelfu ya Rastafarians walivyomlaki Haile Selassie alipoenda Jamaica mwka 1966

Mpaka hii leo jamii ya Rastafarian ipo nchini Ethiopia katika mji wa Shashamene, kilomita 225 kutoka kusini mwa mji wa Addis Ababa kwenye eneo ambalo walipewa kama zawadi na Haille Sellasie kama shukrani baada ya kumuunga mkono katika vita dhidi ya Mussolini.

Sellasie ambaye alikuwa muumini wa Ki'orthodox, haijatambulika bado kama alikuwa akiamini katika Rasta na vilevile aliwahi kuwaambia watu wake kuwa yeye sio kiumbe cha kipekee lakini jamii ya rastafarian waliendelea kumuabudu na kumuita simba wa yuda.

Jambo hili limefanya watu wengi nchi Ethiopia waamini kuwa huenda ni zao la Mfalme Suleiman kwenye maandiko ya Biblia

4) Nyumba ya Sanduku la Agano

Kwa Waethiopia wengi, wanaamini kuwa sanduku takatifu lililokuwa limehifadhi mawe mawili ya Amri Kumi ambayo biblia inasema alipewa Musa na Mungu hazijapotea.

Kanisa la kikristo la Orthodox limesema kuwa sanduku hilo la agano limehifadhiwa kwenye ardhi ya Aksum lilipo kanisa la "Our Lady Mary of Zion" na hakuna mtu anayeruhusiwa kuliona.

Katika tamaduni za kanisa hilo, sanduku hilo limehifadhiwa kisiri ikiwa ni ishara ya heshima kwa Malikia Shiba, ambaye anatajwa kwenye historia.

Wanaamini kuwa alitumia iliyopita kwenye mji wa Aksum akielekea Aksum kwa mfalme Suleiman katika miaka ya 950 BC.

Historia ya safari yake na kutongozwa na Sulemani imeelezewa katika hadithi ya Kebra Nagast (Utukufu wa Wafalme) - kazi ya fasihi ya Ethiopia iliyoandikwa katika lugha ya Ge'ez katika karne ya 14.

Inasimulia jinsi Makeda, Malkia wa Sheba, alivyozaa mtoto wa kiume - Menelik (maana yake Mwana wa Hekima) - ambaye baadae alisafiri kwenda Yerusalemu kukutana na baba yake.

Sulemani alimtaka abakie ili arithi ufalme wake pale tu atakapokuwa amekuwa, lakini alimruhusu kurudi nchini kwake ambapo ni Ethiopia huku akisindikizwa na wanajeshi wa ki'Israeli mmoja wapo aliiba sanduku hilo la aganoi huku akiliachia ambalo linafanania.

Menelik alipogundua aliamua kuhifadhi sehemu maalumu, huku akisema kuwa ni mpango wa Mungu sanduku hilo kufika Ethiopia .

5) Makao ya waislamu wa kwanza nje ya Uarabu

"Kama unataka kwenda Abyssinia, utakutana na mfalme ambaye hawezi kuvumilia uminywaji wa haki ,"Mtume Muhammed aliwaamibia wafuasi wake wakati alipokutana na unyanyasaji kwa mara ya kwanza karne ya saba huko Mecca, ambayo ni Saudi Arabia.

An Ethiopian Muslim stands inside a damaged mausoleum at the al-Negashi Mosque, one of the oldest in Africa and allegedly damaged by shelling, in Negash - March 2021

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Msikiti wa kihistoria wa al-Negashi Mosque uliharibiwa wakati wa mgogoro wa Tigray

Huu ulikuwa wakati ambao mahubiri ya Mtume yalianza kuwa maarufu na kuonekana kuwa tishio kwa watawala ambao si waislamu.

Akichukua ushauri wake, kundi dogo la ufalme wa Aksum, ambao wakati huo uliangazia zaidi Ethiopia na Eritrea ya sasa, ambako walikaribishwa vizuri kufanya shughuli zao za dini na mfalme wa kikristo wa Armah - jina lake la kifalme ni Ge'ez wa Negus, au Negashi Uarabuni.

Kijiji cha Negash,ndicho kinaitwa Tigray sasa, ni ambapo wahamiaji walidaiwa kuishi hapo kwa kujenga baadhi ya misikiti ya kale zaidi barani Afrika.

Mwaka jana, msikiti wa al-Negashi uliharibiwa Tigray.

Waislamu wa hapo wanaamini kuwa walikuwa na mitume 15 ambao walizikwa Negash.

Katika historia ya Kiislamu hatua hii ya Aksum ilianza kufahamika kama Hija ya kwanza.

Kwa sasa Waislamu wanakaribia kufika 34% ya Waethiopia na zaidi ya milioni 115 wakiwa wenyeji.