Kuzimwa kwa intaneti: Nini kitatokea iwapo mtandao utazimwa?

Chanzo cha picha, Reuters
Kutoka chumba cha ofisi yake kilichopo ghorofa ya juu ambacho kinamwezesha Markos Lemma kuona vizuri mji wa Addis Ababa,
Mwanzilishi wa teknolojia ya IceAddis, mazingira yake ya kazi huwa yana shughuli nyingi kutokana na wajisiriamali wa kahawa wenye ndoto kubwa wanapofurika katika eneo hilo.
Lakini intaneti inapofungwa, kila kitu kinakwama.
Taarifa ambayo BBC ilipewa na shirika la kutetea haki mtandaoni, Access Now, inaonesha kuwa mwaka jana huduma hizo za mtandao zilikuwa zinafungwa kimakusudi mara 200 katika nchi 33 tofauti.
"Msongamano wa magari hapa huwa unaisha. Hakuna mtu anayekuja , au wakija hawakahi sana kwa sababu kama hakuna mtandao, wanakuwa hawana kitu cha kufanya hapa," Markos alisema.
"Tulikuwa na programu ya maendeleo ambayo mkataba wake ulifutwa kwa sababu haukukamilika kwa wakati... Mtandao ulikuwa unazimika kila wakati.
Wateja wetu wa nje ya nchi walidhani kuwa hatuko makini katika biashara zetu lakini tulikuwa hatuna cha kufanya. "

Chanzo cha picha, Markos Lemma
Waendesha pikipiki huwa wanasubiri maeneo haya, kwa ajili ya kusambaza chakula.Bila mtandao, watu hawawezi kuagiza vitu mtandaoni au kutumia programu yeyote.
"Kufungwa kwa mtandao huwa kunaathiri biashara zao moja kwa moja na kuathiri watu wa hapa".
Tatizo la kufungwa kwa tovuti
Hili sio tatizo kwa Ethiopia peke yake na athari zake hazipo kwenye uchumi peke yake.
Utafiti unaonyesha kuwa kuzimwa kwa mitandao kunaathiri makumi ya mamilioni ya watu duniani kote kwa namna mbalimbali.
Maafisa wa serikali wana uwezo wa kuzima mtandao kwa kutoa agizo kwa watoa huduma hiyo kuzima intaneti katika baadhi ya maeneo au mara nyingine, huwa wanafungia upatikanaji wa huduma za tovuti.
Makundi ya haki za binadamu wanaona kuwa hiyo ni mbinu ambayo serikali inatumia kuwanyima watu haki zao katia maeneo mbalimbali duniani.
Taarifa mpya za utafiti zilizochambuliwa na BBC zinasema kuwa hali hiyo huwa inazidi haswa wakati wa maandamano.
Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2019 , intaneti ilizimwa wakati ambao watu zaidi ya 60 walipokuwa wanaandamana, na kesi 12 zilionyesha kuwa hali hiyo ya kuzima mitandao huwa inatokea kipindi cha uchaguzi.
Serikali ndio huwa inatoa agizo la kuzimwa kwa mitandao ili kuhakikisha kuwa kuna usalama na kuzuia kwa taarifa ghushi.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa kuzimwa kwa taarifa mtandaoni huwa kuna athiri shughui nyingi muhimu.

Umoja wa mataifa umesema kuwa upatikanaji wa intaneti ni haki ya binadamu mwaka 2016 na kuwa miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu.
Licha ya kamba viongozi wote walikubaliana na wazo hilo lakini, Agosti,2019, Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza uwa intaneti sio maji wala hewa na kuzima mtandao na kusema kuwa kuzima mtandao ni muhimu kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi.

Chanzo cha picha, EPA
Markos Lemma bado ana hasira na madai hayo.
"Serikali haioni kama intaneti ni muhimu.Wanadhani intaneti ni kwa ajili ya mitandao ya kijamii,na hawaoni kuwa ina thamani katika uchumi na inasaidia uchumi."
India inaongoza kwa kuzima mtandao
Taarifa mpya za mwaka 2019 zinaonyesha kuwa India inaongoza kwa kuzima mtandao kuliko nchi nyingine yeyote duniani kwa mwaka jana.
Mtandao wa simu za mkononi ulizimwa mara 21 nchini humo ambayo ni sawa na 67%.
Na maandamano yaliyotokea Sudan na Iraq yalifanya serikali za mataifa hayo kuzima mtandao.

Chanzo cha picha, AFP












