Cruz azomewa kwa kutomuunga mkono Trump

Cruz

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Cruz amesema anataka maadili ya Republican yashindee

Wajumbe katika kongamano kuu la chama cha Republican nchini Marekani wamemzomea seneta wa Texas, Ted Cruz, baada yake kukosa kumuidhinisha Donald Trump kuwa mgombea wa chama hicho.

Bw Cruz alikuwa amesalia kuwa mpinzani pekee wa Bw Trump lakini akajiondoa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mchujo jimbo la Indiana mapema mwezi Mei.

Bw Cruz, akihutubu katika kongamano hilo linalotumiwa kuamua mgombea wa chama hicho kwenye uchaguzi mkuu Novemba, amesema tu kwamba anataka maadili ya chama cha Republican yashindwe kwenye uchaguzi huo.

Waandishi wa habari wanasema hatua ya Bw Cruz kukataa kumuunga mkono wazi bw Trump inatokana na migawanyiko ambayo imeendelea katika chama hicho kuhusu ugombea wa Bw Trump.

  • <link type="page"><caption> Ted Cruz ajitoa kwenye kinyang'anyiro Marekani</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/05/160503_teddycruz_usindiana" platform="highweb"/></link>
  • <link type="page"><caption> Mke wa Trump adaiwa kumuiga Michelle Obama</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/07/160719_trump_plagiarism" platform="highweb"/></link>

Gavana wa Indiana Mike Pence alikubali rasmi kuwa mgombea mwenza wa Bw Trump kwenye kongamano hilo.

Chanzo cha picha, Getty

Ameeleza maadili yake ya kihafidhina na akashambulia maadili na historia na sifa za Hillary Clinton, mgombea wa chama cha Democratic.

Baada yake kumshutumu Bi Clinton, wajumbe wamerudia kuimba "Lock Her Up" (Afungwe) kwa siku ya tatu mfululizo.

Bw Trump anatarajiwa kuhutubia kongamano hilo Jumatano.