Wanahabari wazuiwa kwenye vikao vya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 Tanzania

Kutengwa kwa waandishi wa habari kunaashiria mabadiliko katika mbinu ya uchunguzi na kumezua maswali kuhusu uwazi.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi & Elizabeth Kazibure

  1. Van Dijk anataka Robertson kusalia Liverpool

    Robertson ameshinda mataji tisa wakati alipokuwa Liverpool

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Robertson ameshinda mataji tisa Liverpool

    Mahodha waLiverpool, Virgil van Dijk, amesema anataka mchezaji mwenzaje na makamu wake Andy Robertson, kusalia katika klabu hiyo akimuelezea kuwa ni “mchezaji muhimu sana”.

    Tottenham imeanza mazungumzo na Liverpool ya kumsajili beki huyo wa kushoto, ambaye mkataba wake unamalizika msimu wa joto.

    “Robbo ni mchezaji muhimu sana na nataka abaki, lakini tutaona yatakayojiri,” alisema Van Dijk.

    Robertson alisajiliwa kutoka Hull City mwaka 2017 kwa £8m na amecheza mechi 364, akishinda mataji 9 ikiwa ni pamoja na mataji mawili ya Ligi Kuu ya England na Kombe la Klabu Bingwa Ulaya.

    Ingawa si chaguo la kwanza sasa, Robertson anataka kucheza mara kwa mara na anazingatia chaguo zake.

    Alichukua nafasi ya Milos Kerkez katika kipindi cha mapumziko katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Bournemouth, lakini amecheza mechi nne tu za Ligi Kuu msimu huu.

    Kocha wa Liverpool, Arne Slot, alikataa kutoa maoni kuhusu uhamisho wowote, akisisitiza kuwa uhamisho haujadiliwi hadharani.

    Wataalamu wanasema kuwa kumruhusu Robertson kuondoka Januari hii kutadhuru Liverpool, hasa na mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA zijazo.

    Wakati Robertson anataka kucheza mara kwa mara, uamuzi wowote utazingatia maslahi ya mchezaji na klabu.

    Slot alisisitiza umuhimu wa kuhitaji wachezaji wote, huku mechi za kati ya wiki zikitolewa kama fursa ya mizunguko ya kikosi.

    Maelezo zaidi:

  2. Watanzania wawili wakamatwa Namanga Kenya kwa tuhuma za kuuza pembe za tembo

    ,

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Raia wawili wa Tanzania wakamatwa katika mpaka wa Namanga baada ya kuhusishwa na biashara haramu ya pembe za tembo

    Kwa mujibu wa Idara ya Upelelezi wa Makosa (DCI), washukiwa Imani Manasi Msumbwa na Justin Mwalima, wote raia wa Tanzania, walikamatwa pamoja na Mkenya mmoja, Alton Jilaoneka, ndani ya hoteli ya Mufasa ambapo walikuwa wanaripotiwa kujadili mauzo ya pembe hizo.

    Operesheni hiyo ilifanywa na kikosi cha pamoja cha Huduma ya Polisi ya Taifa (NPS) na Huduma ya Wanyamapori Kenya (KWS) baada ya kupata taarifa za kiintelijensia.

    DCI ilisema maafisa walitekeleza operesheni katika Hoteli ya Mufassa, ambapo washukiwa hao watatu walikuwa wakiandaa kufanikisha biashara ya siri na mnunuzi. Hata hivyo, mmoja wa washukiwa, Justin Mwalima, alitoroka wakati wa operesheni, huku wengine wawili wakikamatwa mara moja.

    Wakati wa uchunguzi, washukiwa walionyesha maafisa magari mawili yaliyojiandikisha Tanzania, ambayo yaliaminika kutumika kusafirisha pembe za tembo.

    Uchunguzi wa Toyota Mark X, nambari ya usajili T476 DHS, uligundua pembe 20 za tembo zenye uzito wa kilo 110 zilizofichwa kwenye buti za magari hayo. Pia Nissan Fairland, nambari ya usajili T305 EFM, ilipatikana na kipimo cha uzito.

    Uchunguzi wa awali unaashiria kuwa pembe hizo zilitoka Malawi na zina uhusiano na kundi haramu la biashara ya pembe katika eneo la kikanda. Mamlaka zinaamini washukiwa walikuwa wanatafuta wanunuzi nje ya kanda kabla ya kujaribu kuingiza pembe hizo kupitia Kenya.

    Washukiwa waliokamatwa, pamoja na magari na pembe zilizokamatwa, walichukuliwa hadi Kituo cha Polisi cha Namanga na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Kajiado siku ya Jumatatu.

    Mamlaka zimesema operesheni hii inaonyesha dhamira ya serikali ya kupambana na biashara haramu ya wanyamapori kupitia ushirikiano wa mashirika mbalimbali na matumizi ya taarifa za kiintelijensia, ili kulinda spishi zilizo hatarini na rasilimali asili za Kenya.

  3. 'Kikosi cha wauaji kilitumwa kuniangamiza' adai Gachagua

    Rigathi Gachaga

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Naibu wa rais wa zamani wa Kenya Rigathi Gachaga

    Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua anasema yuko salama nyumbani kwake Wamunyoro, Kaunti ya Nyeri, eneo la Kati mwa Kenya, baada ya saa kadhaa za sintofahamu kuhusu aliko kufuatia tukio la Jumapili.

    Hapo awali, Gachagua alidai kuwa "kikosi cha wauaji kikiungwa mkono na polisi wa eneo hilo," kilitekeleza agizo la Rais William Ruto, kwa kuvamia na kuvuruga ibada ya kanisa ambayo yeye na washirika wake walikuwa wakihudhuria.

    Gachagua alisema kupitia mtandao wa X kuwa yeye na wafuasi wake walikwama ndani ya kanisa baada ya polisi kurusha mabomu ya machozi, akidai kuwa lilikuwa jaribio la mauaji. Alidai kuwa magari yake yaliteketezwa na kuiomba umma iwaombee.

    “William Ruto ametuma kikosi cha wauaji kutuua ndani ya kanisa. Tumekwama tukishambuliwa kwa risasi na mabomu ya machozi,” aliandika.

    Gachagua amekuwa mmoja wa wakosoaji wakuu wa Rais Ruto tangu alipoondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye mwaka 2024.

    Wasiwasi kuhusu usalama wake ilitanda mitandaoni baada ya ripoti kuwa maafisa wa usalama na watu wasiojulikana walivamia ibada ya Jumapili katika Kanisa la Wairima ACK, Othaya, Kaunti ya Nyeri, katika tukio ambalo lilisababisha Gachagua kuondolewa ghafla kanisani hapo na walinzi wake.

    Waumini wanasema waliona ganda la risasi ndani ya eneo la kanisa.

    Watu waliodhaniwa kuwa polisi waliovalia kiraia walirusha mabomu ya machozi na kupiga risasi wakati Gachagua alipofika kuhudhuria ibada.

    Mamlaka ya Kenya inasema uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Kipchumba Murkomen amesema, "Vurugu popote pale, na hata hasa katika sehemu ya ibada, haikubaliki...nimezungumza na Inspekta Jenerali wa Polisi, Bw Douglas Kanja, ambaye amenihakikishia kuwa uchunguzi unaendelea na kwamba wahusika watafikishwa mahakamani."

    Hii sio mara ya kwanza Gachagua kushambuliwa kanisani; wiki mbili zilizopita shambulio la aina hiyo lilitokea nje ya Kanisa la Independent Pentecostal Church of Africa (AIPCA) Kiamworia, baada ya majibizano kati ya makundi mawili ya vijana na kupelekea polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

    Mvutano huo ulisababisha msongamano wa magari katika barabara ya Kiamworia-Gatundu South, huku mabomu hayo yakiwaathiri waumini kadhaa kwa kushindwa kupumua vizuri.

    Unaweza pia kusoma:

  4. Mwanamke agundua kamera ya siri chooni, Uingereza

    Mgahawa wa Giggling Squid ulisema wafanyakazi waliripoti "kitu kinachotiliwa shaka"

    Chanzo cha picha, Supplied

    Mwanamke wa miaka 32 alisema alihisi “kudhulumiwa” baada ya kugundua kamera inayorekodi moja kwa moja iliyofichwa katika choo cha mgahawa wa Kithai, Giggling Squid, St Martin's Square, Leicester, Uingereza, wakati alipokuwa kwenye miadi na mwenzi wake kati ya Krismasi na Mwaka Mpya. Aliwajulisha mara moja wafanyakazi wa mgahawa huo.

    Mfanyakazi huyo wa NHS alipata kamera hiyo nyeusi, iliyofunikwa sehemu na karatasi ya jikoni, chini ya kiti cha choo Alisema: "Wazo la kuwa kuna mtu anaangalia, hasa katika eneo la siri ambalo mtu anakuwa mwenyewe, liliniogopesha sana… lazima kulikuwa na watu wengi waliotumia choo hicho."

    Polisi wa Leicestershire waliripewa taarifa siku iliyofuata na kukikamata kifaa hicho. Maafisa walichunguza video za CCTV na kuzungumza na wafanyakazi ili kutambua mshukiwa anayehusika, huku wakiwaonya wafanyakazi kuwa makini.

    Mgahawa wa Giggling Squid ulisema wafanyakazi waliripoti "kitu kinachotiliwa shaka" mara moja na wanashirikiana kikamilifu na polisi.

    Mwanamke huyo anatumai kuwa tukio hili litaongeza uelewa: "Angalia kila sehemu, hata zile ambazo huwezi kufikiria kuwa hatarishi… kama tukio hili litaweza kumsaidia mtu kugundua kabla hajajisaidia, basi ni litakuwa jambo zuri."

  5. Maafisa wa uhamiaji wamuua raia mwingine wa Marekani mjini Minneapolis

    .

    Chanzo cha picha, Michael Pretti/AP

    Maafisa wa uhamiaji wa Marekani wamempiga risasi na kumuua raia wa Marekani mjini Minneapolis siku ya Jumamosi, tukio lililosababisha maandamano na ukosoaji mkali kutoka kwa viongozi wa eneo hilo.

    Hili ni tukio la pili la aina hiyo ndani ya mwezi huu.

    Idara ya Usalama wa Ndani (DHS) ilisema afisa wa usalama anayehusika na kulinda mipaka ya nchi, kuzuia uingiaji katika nchi kwa njia haramu, magendo na uhalifu wa mipakani, alifyatua risasi kama hatua ya kujilinda baada ya mwanaume huyo kumkaribia akiwa na bastola na kupinga kunyang’anywa silaha.

    Hata hivyo, video za mashuhuda zilizothibitishwa na Reuters zinaonyesha mwanaume huyo, aliyetambulika kama Alex Pretti mwenye umri wa miaka 37, akiwa ameshika simu, na si bunduki, alipokuwa akijaribu kuwasaidia waandamanaji waliokuwa wamesukumwa chini na maafisa.

    Video zinaonyesha afisa huyo akiwafukuza wanawake wawili kabla Pretti kuingilia kati na kunyunyiziwa dawa ya kuwasha macho inayotumika kutuliza watu. Maafisa kadhaa kisha wakamdhibiti na kumwangusha chini. Baada ya sauti kusikika ikionya kuhusu uwepo wa bunduki, inaonekana afisa mmoja anaondoa silaha kutoka kwa Pretti. Muda mfupi baadaye, afisa mmoja mwingine anampiga Pretti risasi mgongoni, ikifuatiwa na risasi zaidi.

    Pretti, ambaye alikuwa muuguzi wa wagonjwa mahututi, alifariki dunia. Kifo chake kilichochea mamia ya waandamanaji kuandamana, huku maafisa wakitumia mabomu ya machozi na mabomu yanayo sababisha upofu wa muda mfupi, kutokusikia kwa muda fulani, na usumbufu wa ndani ya sikio hapo hapo. Maandamano pia yaliripotiwa New York, Washington DC na San Francisco.

    Tukio hilo limeongeza mvutano mkali kati ya serikali ya jimbo na serikali ya shirikisho, mvutano uliokuwepo tayari kufuatia kuuawa kwa raia mwingine wa Marekani, Renee Good, Januari 7. Maafisa wa shirikisho wamekataa kuruhusu mamlaka za eneo kushiriki katika uchunguzi.

    Waziri wa Usalama wa Ndani, Kristi Noem, alisema Pretti aliwashambulia maafisa wakati wa oparesheni ya uhamiaji, kauli iliyopingwa na Gavana wa Minnesota, Tim Walz, aliyesema video za tukio hilo ni “za kutisha” na kwamba jimbo litaongoza uchunguzi.

    Mkuu wa Polisi wa Minneapolis, Brian O’Hara, alisema Pretti alikuwa mmiliki halali wa silaha na hakuwa na rekodi ya uhalifu isipokuwa makosa ya barabarani. Maandamano yalitulia baada ya maafisa wa shirikisho kuondoka eneo hilo, huku viongozi wa eneo wakitoa wito wa utulivu.

    Walz na Meya wa Minneapolis, Jacob Frey, wametaka kusitishwa mara moja kwa oparesheni za utekelezaji wa sheria za uhamiaji za serikali ya Trump.

    Rais Trump aliwatuhumu viongozi wa eneo hilo kwa kuchochea machafuko, huku Makamu wa Rais JD Vance akiwalaumu kwa kushindwa kuwaunga mkono maafisa wa shirikisho.

    Soma pia:

  6. Trump atishia kuitoza Canada ushuru wa 100%

    Trump na Carney wakiwa katika Mkutano wa Kilele wan G7 nchini Canada.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Trump na Carney wakiwa katika Mkutano wa Kilele wan G7 nchini Canada.

    Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kutoza ushuru wa asilimia 100 bidhaa za Canada nchi hiyo ikifikia mkataba wa kibiashara na China.

    "Ikiwa Canada itafikia makubaliano na China, tutatoza ushuru wa 100% dhidi ya bidhaa zake zote zinazoingia Marekani.," Trump alisema kwenye mtandao wa Truth Social.

    Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa Canada Carney alitangaza "ushirikiano wa kimkakati" na China, na kukubaliana kupunguza ushuru.

    Wakati huo, Trump alitaja hatua hiyo kuwa "jambo zuri". Lakini mvutano kati ya Marekani na Canada umeongezeka katika siku za hivi karibuni, baada ya Carney kusema katika hotuba yake huko Davos kwamba utaratibu wa dunia unaoongozwa na Marekani umevunjwa.

    Carney pia aliyahimiza "mataifa mengine yaliyo na uwezo wa kadri" kuungana dhidi ya shurutisho la kiuchumi na "mataifa makubwa", ingawa hakumtaja Trump kwa jina.

    Trump alijibu tamko hilo katika hotuba yake siku iliyofuata, akisema: "Canada inaishi kwa sababu ya Marekani."

    Rais huyo wa Marekani pia alitupilia mbali ombi la Canada kujiunga na Bodi yake mpya ya Amani.

    Siku ya Jumamosi, Trump alisema katika mtandao wa kijamii kwamba ikiwa Carney "anadhani ataifanya Canada 'kituo' cha China kutuma bidhaa nchini Marekani, amekosea sana".

    Soma pia:

  7. Syria yaongeza muda wa kusitisha mapigano na SDF

    ..

    Chanzo cha picha, Reuters

    Serikali ya Syria imetangaza kuongeza muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano na vikosi vya Wakurdi kwa siku 15, ili kuruhusu kukamilika kwa operesheni ya Marekani ya kuwahamisha wafungwa wa kundi linalojiita Islamic State hadi Iraq.

    Vyanzo kadhaa hapo awali vimehibitisha kwamba serikali ya Syria na vikosi vya Syrian Democratic Forces (SDF) imekubali kuongeza muda wa makubaliano hayo, kwa mujibu wa Agence France-Presse, ili kuipa Marekani muda wahamisha wafungwa kutoka shirika hilo.

    Wizara ya Ulinzi ya Syria ilisema katika taarifa yake, "Tunatangaza kuongezwa kwa muda wa mwisho wa kusitisha mapigano katika sekta zote za Operesheni za Jeshi la Syria kwa muda wa siku 15, kuanzia saa tano usiku saa za ndani (20:00 GMT)."

    Alithibitisha kuwa hatua hiyo inakuja "kuunga mkono operesheni ya Marekani ya kuwahamisha wafungwa wa ISIS kutoka magereza ya SDF (Syrian Democratic Forces) hadi Iraq."

    Makubaliano ya kusitisha mapigano yamekuwa yakitekelezwa kwa siku kadhaa kama sehemu ya maelewano mapana kati ya serikali na Wakurdi, ambayo yanasisitiza kukamilishwa kwa majadiliano juu ya ushirikiano wa siku zijazo wa taasisi za Kikurdi katika Jimbo la Hasakah katika mfumo wa taasisi za serikali, kufuatia kujiondoa kwa Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria kutoka maeneo ya kaskazini na mashariki mwa nchi, huku kukiwa na makabiliano kati ya vikosi vya Syria na serikali ya Syria.

  8. Wanahabari wazuiwa kwenye vikao vya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 Tanzania

    ,

    Waandishi wa habari nchini Tanzania wamezuiwa kuhudhuria vikao vya Tume ya Rais ya Uchunguzi, huku wahanga wa machafuko ya uchaguzi wa Oktoba 2025 wakitoa ushuhuda.

    Tume hiyo iliyoundwa na Rais Samia Suluhu, inachunguza vurugu hizo kwa lengo la kubaini sababu zake na kupendekeza njia za kuendeleza maridhiano ya kitaifa.

    Vikao vya awali vilikuwa wazi kwa vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa kuripoti juu ya ushuhuda wa waathiriwa.

    Hata hivyo, wanahabari na baadhi ya vyombo vya habari vilisema hawakuruhusiwa kuhudhuria vikao vya ufuatiliaji siku ya Jumamosi.

    Siku ya Ijumaa waathiriwa walitoa maelezo ya kina kuhusu ghasia za siku ya uchaguzi.

    Taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na gazeti la The Citizen ilisema wanahabari waliruhusiwa kuripoti vikao vya Ijumaa, ambapo waathiriwa walitoa ushuhuda wao.

    Hapo jana Mwananchi liliandika: "Leo Januari 24, 2026 tume ilikutana katika Wilaya ya Ubungo. Tofauti na vikao vya awali, waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia ukumbini wakati wa kutoa ushahidi."

    Profesa Ibrahim Juma, anayeongoza uchunguzi huo aliwaambia waliohudhuria Jumamosi kuwa waandishi wa habari hawataruhusiwa wakati wa kutoa ushahidi. Alisema uamuzi huo ulifanywa ili kulinda faragha ya mashahidi.

    Wakazi walitoa maelezo ya matukio waliyoshuhudia au uzoefu siku ya uchaguzi, wakielezea athari za kibinafsi za machafuko hayo.

    Kutengwa kwa waandishi wa habari kunaashiria mabadiliko katika mbinu ya uchunguzi na kumezua maswali kuhusu uwazi.

    Mwandishi wa habari wa ndani aliiambia BBC kwamba uamuzi huo unatia wasiwasi.

    "Inasikitisha kwamba waandishi wa habari wananyimwa nafasi ya kuripoti. Baadhi ya shuhuda hizi tayari zimetolewa. Wanajaribu kuficha nini? ... Je, hii ni kwa sababu ya habari za hivi majuzi? au amri kutoka kwa mamlaka? Tunaheshimu faragha, lakini si kila shahidi ameomba faragha juu ya ushuhuda wao," mwandishi wa habari alisema.

    Bado haijabainika ikiwa wanahabari wataruhusiwa kuhudhuria vikao vijavyo vya tume hiyo.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Karibu katika taarifa zetu za moja kwa moja.